To provide the best experiences, we use technologies like cookies to store and/or access device information. Consenting to these technologies will allow us to process data such as browsing behavior or unique IDs on this site. Not consenting or withdrawing consent, may adversely affect certain features and functions.
The technical storage or access is strictly necessary for the legitimate purpose of enabling the use of a specific service explicitly requested by the subscriber or user, or for the sole purpose of carrying out the transmission of a communication over an electronic communications network.
The technical storage or access is necessary for the legitimate purpose of storing preferences that are not requested by the subscriber or user.
The technical storage or access that is used exclusively for statistical purposes.
The technical storage or access that is used exclusively for anonymous statistical purposes. Without a subpoena, voluntary compliance on the part of your Internet Service Provider, or additional records from a third party, information stored or retrieved for this purpose alone cannot usually be used to identify you.
The technical storage or access is required to create user profiles to send advertising, or to track the user on a website or across several websites for similar marketing purposes.
Madawa ya Kulevya
Utangulizi
Madawa ya kulevya ni hatari sana katika maisha ya binadamu. Madawa haya yanaathiri maisha ya watu wanaoyatumia na wasioyatumia. Kila sehemu unakokwenda kila jamii yaelekea kupiga marufuku matumizi ya madawa ya kulevya. Hata hivyo kuna watu wanaoshikilia kwamba madawa haya yakubaliwe
ili wanaoyataka, wayatumie.
Je, wewe umewahi kuona madawa yoyote ya kulevya? Ni watu gani katika jamii wanaotumia madawa haya? Unajua namna madawa haya yanaathiri jamii? Unaweza kupendekeza mikakati ya kusimamisha matumizi ya madawa ya kulevya? Mada hii itakuwezesha kukuza na kutumia msamiati unaohusiana
na madawa ya kulevya pamoja na kutumia vipengele vya lugha vilivyoteuliwa ili kuimalisha mawasiliano yako.
stadi za lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo a: Kutambua msamiati wa Madawa ya Kulevya
Utangulizi
Madawa ya kulevya ni mengi katika jamii zetu. Kuna yale yanayopandwa na mengine yanayonunuliwa madukani. Je, unaweza kutambua baadhi ya madawa hayo ya kulevya? Ni madawa gani ya kulevya ambayo ni rahisi kupatikana katika jamii yako? Ni madawa gani ambayo hutumika zaidi miongoni mwa
watumizi katika jamii yako? Umekuwa ukitembea aidha dukani, au kutazama filamu na mazingira yako. Je, ni madawa gani ambayo umekuwa ukiyaona k wingi na ambayo ni rahisi kupatikana?
Shughuli 1.1
Kutambua msamiati wa madawa ya kulevya
Taz: Katika mada ndogo hii, umetambua msamiati wa madawa ya kulevya ambayo huuzwa madukani na hata kupandwa nyumbani. Msamiati huu, ukiutumia daima, utakuwezesha kuwasiliana kwa ufasaha katika maisha ya kila siku.
Stadi za lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo b: Kutambua na kuigiza athari za madawa ya kulevya
Utangulizi
Kwa kawaida, tunaweza kutambua kitu au hali kupitia kwa maigizo au kutazama filamu au kusikiliza maigizo katika redio kuhusu jambo. Je, umewahi kutazama waigizaji wakiigiza matumizi ya madawa ya kulevya? Ni athari gani ulizowahi kutambua kulingana na mtazamo wa waigizaji wa matumizi ya madawa ya kulevya? Umewahi kukutana na watu ambao wanatumia madawa ya kulevya? Kama umewahi kukutana nao, ni athari gani ulioweza kutambua kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya. Umekuwa ukisikia watu au maonyo kuhusiana na matumizi ya madawa ya kulevya. Je unaweza kutambua baadhi ya athari
ulizoweza kuona na kusikia kutoka kwa watu?
Taz:Katika funzo hili, umetambua aina mbalimbali za madawa ya kulevya na kutambua athari za matumizi ya madawa ya kulevya. Kwa kutumia tajiriba uliyo nayo katika hali halisi ya maisha yako, umetambua kuwa madawa ya kulevya ni hatari katika afya yetu. Ni muhimu kuepukana nayo ili kuwa na afya nzuri ili kujenga jamii mpya yenye maendeleo.
Stadi za lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo c: Kueleza njia mwafaka za kuzuia athari za
matumizi ya madawa ya kulevya
Utangulizi
Katika jamii zetu, kuna watu hasa vijana ambao hupenda kutumia madawa ya kulevya. Matokeo yamekuwa kwamba vijana hawa hudhoofika kiafya na wengine kupoteza maisha yao. Hali hii imesababisha jamii kupoteza watu ambao wangezalisha mali kwa jamii hizo. Katika mada ndogo hii, utaweza kupendekeza njia mwafaka za kuzuia athari za madawa ya kulevya.
Kutaja na kuigiza athari za madawa ya kulevya
Kueleza njia za kuzuia athari za madawa ya kulevya
Taz: Kwa kuhitimisha, funzo hili limekupa mwangaza kuwa madawa ya kulevya yana madhara makubwa kwa afya ya mtu, jamii na uchumi wa nchi. Ni muhimu kuepukana na matumizi ya madawa ya kulevya kwa ajili ya afya zetu na jamii zetu.
Stadi za lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo d: Kusoma shairi kuhusu madawa ya kulevya
Utangulizi
Shairi ni kipengele cha fasihi ambacho hutumiwa kuelimisha jamii. Hutumiwa kuonya watu na kukashifu vitendo vibaya katika jamii. Mashairi husomwa, hukaririwa, hughaniwa na kuimbwa. Hata hivyo uhondo wake umo katika ujumbe unaojitokeza. Je, umewahi kusikia shairi likisomwa, likighaniwa, kukaririwa au kuimbwa? Ni mambo gani ambayo unaweza kutambua katika mashairi? Je,
unajua kwamba shairi hutumiwa kuonya kushauri, kuelimisha hata kueleza hali ya jamii? Ukisikia shairi lenye kichwa “Madawa ya Kulevya” unafikiri shairi hilo linahusu mambo yapi?
2.
Kusoma na kukariri shairi la madawa ya kulevya
Shughuli 1.5
1 . Soma na kukariri shairi hili
Mbeje kofia navua, ili nipate kunena,
Mengi moyoni mejaa, ya madawa ya kulevya,
Mengi moyoni mejaa, ya madawa ya kulevya,
Ulimi wanichochea, kushaurini vijana,
Madawa yanayolevya. yaathiri afya yako,
Si vijana si mababu. wengi wavuta sigara,
Wamesahau wajibu, bangi yawateka nyara,
Kama vile uraibu, na mengineyo madhara,
Madawa yanayo/evya, yaathiri afya yako.
Vijana miraa raha, wamekuwa vibogoyo,
Hamu ya kula hawana, nguvu kazi hakunayo,
Tumbaku huleta pigo, kensa kwao wavutayo,
Madawa yanayo/evya, yaathiri afya yako.
Waraibu husifia, wao ni waungwana,
Na mali yakosa njia, wafuja hata mchana,
hasara hutumbukia, na uchafu hukumbana,
Madawa yanayo/evya, yaathiri afya yako.
Shisha nyumbani majukumu, ndoa watupia mbali,
wote shika heshimu, sikia madhara kali,
yamejaa mengi sumu, Siposikia sijali,
Madawa yanayo/evya, yaathiri afya yako.
Madawa yanayolevya, ni hatari kwa maisha,
Yafaa kutoyachovya, katu katika maisha,
Vijana tuchunge afya, madawa kujiepusha,
Hii ni ndiyo nasaha, kujibari na madawa.
2.Katika vikundi, jibuni maswali yafuatayo:
a) Shairi hili ni shairi zuri sana kuhusu madawa ya kulevya. Elezeni
sababu tatu.
b) Mwandishi anaijali sana jamii yake. Mnafikiria shairi hili lina wahUsu watu wa aina gani?
c) Kuna mengi ambayo yamesemwa katika shairi hili.
Toeni ripoti kamili kuhusiana na ujumbe wa shairi.
d) Shairi hili lilidhamiria kufanya nini kulingana na mwandishi?
e) Mwenye sikio amesikia, asiyesikia aibLJ. Elezeni kauli hii kulingana na shairi.
Taz: Kwa kuhitimisha, umelisoma na kulikariri shairi hili. Umetambua mengi kuhusu madawa ya kulevya. Unaweza kulikariri shairi hili kwa wale wanaopenda kutumia madawa ya kulevya. Unaweza kusoma au kutafuta mashairi mengine kuhusu madawa ya kulevya kutoka mtandaoni au hata kubuni mashairi yako kuhusu madawa ya kulevya, kushauri walanguzi na wanaotumia madawa ya kulevya.
Stadi za lugha: kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika
Funzo e: Sarufi -Kutunga sentensi kuonyesha matumizi
bora ya “kwa”
“Kwa” ni kipengele cha sarufi ambacho kina maana nyingi. Kwa kawaida, huwa tunatumia “kwa” bila kutambua au bila kujali matumizi yake. Ikiwa unakula chakula ukitumia mikono yako, utasemaje kwa kutumia kwa? Aidha, ikiwa unasafiri kwenda Sheema kwa kutumia gari, utasemaje kwa kutumia kwa?
kama umeenda shuleni ukiwa umechelewa na kisha mwalimu akakuaadhibu kwa kuchelewa, utatumia kwa kuelezea hali iliyokufanya kuadhibiwa. Pia, ukienda kumtembelea rafiki yako nyumbani kwao bila kutoa taarifa kwa mzazi wako, kisha mzazi akupigie simu na kukuuliza uko wapi, utamjibuje? Jadiliana
zaidi kuhusu matumizi ya “Kwa” kulingana na jinsi umekuwa ukiitumia.
1.
Kutunga sentensi kwa kutumia “kwa”
Katika vikundi, jadiliana kuhusu kinachotendeka katika kila picha.
3.
Kila kikundi kitunge na kuwasilisha sentensi kwa kuonyesha kifaa kinachotumika katika kila picha.
a) Mkiwa katika vikundi vyenu, elezeni maana ya kila sentensi kama ilivyotumika;
i) Shangazi alikuja kwa ajili ya sherehe
ii) Wanafunzi walikula chakula kwa furaha
iii) Wazee kwa vijana walishiriki katika hafla ya mahafali.
b) Andikeni na kuwasilisha sentensi mbili kuonyesha “kwa ya kumiliki”
c) Jadilianeni juu ya matumizi ya “kwa ya kuuliza.”
Taz: Umejifunza mengi kuhusu matumizi ya “kwa,” na unaweza kutoa ripoti ya jumla kuhusu “kwa.”lkiwa umekuwa ukitumia “kwa” kwa njia ambayo sio sahihi katika mawasiliano yako ya kila siku, sasa umejifunza namna ya kuitumia kwa usahihi. Pia, baada ya funzo hili, unaweza kuandika sentensi mbalimbali ukitumia “kwa” bila tatizo. Vilevile kufikia sasa unaweza kuwasiliana ukitumia “kwa” mbalimbali bila makosa katika sentensi zako.
Stadi za Lugha: Kusoma na Kuandika
Funzo f: Kuandika sentensi sahihi kutumia masharti ya
“-nge-” na “-ngali-” na kuzikanusha
Matumizi ya “-nge-“
Utangulizi
Una njaa na unaenda nyumbani ukitegemea kupata chakula. Unaacha kula chakula shuleni, lakini unapofika nyumbani unakuta mlango umefungwa na hakuna hata harufu ya chakula. Unaanza kujilaumu kwa kukataa kula chakula shuleni. Katika hali kama hii, unatumia -nge- kuonyesha majuto yako.
Taz: ‘-nge-‘ hutumika kuonyesha masharti. Maana yake ni kwamba kuwepo kwa hali moja kulisababisha hali nyingine au kulitegemea hali nyingine.
Kutumia “-nge-” katika kutunga sentensi
a) Ningejua, singeiba mbuzi wa jirani yetu.
b) Tungekuja mapema hatungechelewa hivi.
c) Tungechezea mbali na moto, nyumba hii haingeteketezwa.
a) Mama alienda sokoni kununua nyama lakini alikosa pesa za kutosha kununua nyama.
b) Kengele ya chamcha imegonga ninahisi njaa lakini mwalimu yu ngali darasani.
c) Sikuweka bidii katika masomo yangu kwa hiyo sikupita vizuri.
Stadi za Lugha: Kusoma na Kuandika
Matumizi ya “-ngali-“
Utangulizi
-ngali- ni kipengele cha kisarufi ambacho hutumika peke yake katika sentensi. N afikiri umekuwa ukitumia ‘ngali’ katika mawasiliano ya kila siku. Umekwenda duk ani ukanunua maziwa lakini ukasahau kuyachemsha ili kuyahifadhi. Unapopatwa na njaa na kutaka kunywa chai, unapata maziwa ya chai yameshaharibika. Unaj uta kwa kutoyahifadhi vizuri. Je, utasemaje kwa kutumia ‘-ngali-‘kuelezea hali hii.
Matumizi ya “-ngali-” katika sentensi
a) Mtoto anachezea kisu. Unamwonya lakini hasikii. Kisha anajikata kidole chake. Je, mtoto atasemaje kuonyesha kwamba alikuwa
ameonywa dhidi ya kuchezea kisu.
b) Shalwa aliitiwa kazi lakini aliamua kwenda siku iliyofuata. Alipofika kazini, nafasi yake ilikuwa imechukuliwa na mtu mwingine. Shalwa anasemaje kwa kutumia “ngali”kuonyesha kwamba anajuta
kutoenda kazini siku hiyo?
2.Katika daftari lako, tunga sentensi mbili sahihi ukitumia “ngali” ya masharti.
3.Katika vikundi, elezeni maana ya sentensi hizi:
i) Baba angalinikuta, angaliniadhibu vikali.
ii) Karo ingalikuwepo ningalisomea Marekani.
iii) Chakula kingalikuwepo, tungalishinda huku wiki nzima.
Taz: Kile ambacho unastahili kutambua ni kuwa -ngali- hutumika kuonyesha ukosefu wa uwezekano wa kutendeka kwa jambo. Kufikia sasa, unaweza kutofautisha “-nge-” na “-ngali-” kimatumizi. Aidha, inafaa ikumbukwe kuwa unapotumia hali hizi za masharti ya nge na ngali/ngeli, unastahili kuitumia moja baada ya nyingine. Ni uvunjaji wa kanuni za kisarufi kutumia -nge- na -ngali- kwa pamoja katika sentensi moja kwa sababu utakuwa unaonyesha hali tofauti katika nyakati tofauti. Kile ambacho unastahili
kutambua ni kuwa -ngali- hutumika kuonyesha ukosefu wa uwezekano wa kutendeka kwa jambo. Kufikia sasa, unaweza kutofautisha’-nge-‘ na -ngali-‘ kimatumizi. Aidha, inafaa ikumbukwe kuwa unapotumia hali hizi za masharti ya nge na -ngali-/-ngeli-, unastahili kuitumia moja baada ya nyingine. Ni uvunjaji wa kanuni za kisarufi kutumia -nge- na -ngali- kwa pamoja katika sentensi moja kwa sababu utakuwa unaonyesha hali tof auti katika nyakati tofauti.
Stadi za Lugha: Kusoma na Kuandika
Ukanushaji wa -nge- na -ngali-
Utangulizi
Tunafahamu kuwa katika jamii nyingi, kuna mambo ambayo tunakubali yatendeke na yale mengine ambayo huwa hatukubaliani nayo. Hali hii husababisha hali ya kukubali au kukataa kutendeka kwa jambo au kitendo fulani. Je, umewahi kujuta kwa kukosa kufanya kitu hivyo ukakosa mafanikio?
Hali hii ilipokupata ulimweleza mwenzako kwa kutumia maneno yapi? Mkulima anaposema, “ningepanda mapema ningevuna mazao mengi.” Anamaanisha nini? Ikiwa mkulima alipanda mapema na akavuna mazao mengi, ataelezaje hali hii kwa kutumia “-nge-” au -ngali-? Mada ndogo hii itakuwezesha kukanusha hali za masharti za -nge- na -ngali- kwa usahihi.
Shughuli 1.9
Kukanusha “-ngali-” na “-nge-“
a) Ningefika mapema, ningewapata
b) Angalijaribu kukuibia angeshikwa na polisi
c) Ungalikumbuka ungalibeba mwavula
d) Karatasi zingeletwa, tungelifanya mtihani
a) Jadilianeni kuhusu sentensi ambazo mmekanusha katika 1 hapo juu. Mmegundua mabadiliko gani ya maneno katika ukanushaji wa sentensi hizo?
b) Tungeni sentensi tano sahihi kwa kutumia “-nge-” na “-ngali-” na kisha mzikanushe ifaavyo.
c) Elezeni maana ya sentensi hizi:
i) Nyumba isingalianguka, isingaliwauwa watu.
ii) Pahali hapa pasingalisafishwa, pasingalipendeza.
iii) Tusingetumia kompyuta, tusingefanikiwa.
Taz:Tumetambua kuwa kukanusha ni kukataa jambo. Hata hivyo, kuna anu ni zinazoongoza ukanushaji wa ‘-nge-‘ na’-ngali-‘. Umegundua kwamb a ukanushaji wa nge na ngali katika sentensi huchukua muundo huu•. Nomino/ Kiwakilishi + si + nge/ngali + kitenzi.
Stadi za lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo g: Fasihi simulizi- Kusimulia hadithi juu ya mihadarati
Utangulizi
Unapotembea mjini, barabarani au kijijini umewahi kuona watu ambao wameharibika kitabia; wenye nywele zilizochakaa, wanaotembea wakitafunatafuna na miili yao inaonekana vibaya? Umewahi kusimuliwa au kusikia visa au kushuhudia matukio kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya? Je, umepata kusikia taarifa za habari au kutazama taarifa kwenye runinga kuhusu athari na hatari za matumizi ya madawa ya kulevya? Je, unaikumbuka hadithi au kisa chochote kuhusu madawa ya kulevya?
Mada ndogo hii itakuwezesha kusikiliza na kusimulia hadithi kuhusu madawa ya kulevya ili watakaosikiliza hadithi yako, wajiepushe na kutumia madawa ya kulevya.
Hadithi kuhusu madawa ya kulevya
Shughuli 1.10 Kusimulia hadithi kuhusu madawa ya kulevya.
2.Mkiwa katika vikundi, simulia wanakikundi chako hadithi au kisa ulichowahi kushuhudia au kusikia kuhusu madawa ya kulevya.
3.Baada ya kuwasimulia hadithi au kisa hicho, waulize maswali nao wakujibu kwa usahihi kuthibitisha kuwa wamekuwa wakikusikiliza kwa makini.
Taz: Umejifunza mengi kuhusiana na madawa ya kulevya. Umetambua majina, aina na athari za matumizi ya madawa ya kulevya. Umetambua kwamba matumiziya madawa ya kulevya hayafai kabisa; ni kinyume cha sheria na ni hatari sana kwa maisha yako. Hivyo, inafaa kuyaepuka na kutoyatumia kabisa.
Stadi za lugha: Kuandika
Funzo h: Kutambua hatua mwafaka za kuandika insha ya hotuba
Utangulizi
Hotuba ni maneno au taarifa ambayo hutolewa mbele ya watu au hadhira. Je, mewahi kuhudhuria mkutano wowote? Je, umewahi kusikiliza hotuba ya Rais au mtu mashuhuri katika runinga, redio au mtandaoni? Je, hotuba hiyo ilihusu nini? Je, hotuba hiyo ilianza Vipi na ikaisha vipi? Je, unaweza kutambua hatua ambazo unaweza kuzingatia ikiwa umepewa nafasi ya kutoa hotuba kwa wanafunzi wenzako
kuwaonya kuhusu madhara ya madawa ya kulevya?
1Hatua za kuandika insha ya hotuba
Katika vikundi, jadiliana na kuorodhesha hatua za kuzingatia wakati wa kuandika hotuba.
2.Wasilisheni hatua hizo mbele ya darasa, kisha mfanye marekebisho.
3.Kila mwanafunzi afanye utafiti na kuandika hotuba kuhusu athari za madawa ya kulevya. Linganisha hotuba yako na zile za wanakikundi chako. Pamoja, andikeni hotuba moja kutoka kwa zile mlizoandika na
muiwasilishie wanafunzi wote darasani.
Funzo i: Kuandika insha ya hotuba
Stadi za lugha: Kuandika
Utangulizi
Kuandika insha ni njia mojawapo ya mawasilano katika jamii zetu. Insha inastahili kueleza wazo, maoni au mapendekezo kuhusu kitu fulani. Je, umewahi kuandika insha? Mada ndogo hii itakuongoza na kukuwezesha kubuni na kuandika insha.
Kuandika Insha
Katika vikundi,
wengine kulinganisha na ile yao.
Taz: Funzo hili limekuwa muhimu sana kwetu. Tumejifunza kuhusu hotuba, tukatambua hatua za kuzingatiwa katika uandishi wa hotuba na mwisho kuandika mfano wa hotuba juu ya “Athari za madawa ya kulevya kwa vijana wa leo.” Naamini umenufaika na somo hili na utazidi kufanya mazoezi ya kuandika hotuba ukiongozwa na mwalimu ili kukuza stadi zako za mawasiliano.
Muhtasari wa mada
Katika mada hii, umejifunza juu ya:
Msamiati wa madawa ya kulevya
Athari za madawa ya kulevya
Njia mwafaka za kuzuia athari za madawa ya kulevya
Shairi kuhusu madawa ya kulevya
Sentensi zinazoonyesha matumizi ya kwa
Sentensi sahihi zenye hali za masharti za -nge na -ngali na
kuzikanusha kwa usahihi.
Hadithi fupi juu ya mihadarati
Hatua mwafaka za kutayarisha na kuandika insha yahotuba
Hatua mwafaka za kutayarisha na kuandika insha ya hotuba.
Jinsi ya kuandika inshaya hotuba.
Assignment
ASSIGNMENT : Mfano wa Shughuli Jumlishi juu Madawa ya Kulevya MARKS : 10 DURATION : 1 week, 3 days