To provide the best experiences, we use technologies like cookies to store and/or access device information. Consenting to these technologies will allow us to process data such as browsing behavior or unique IDs on this site. Not consenting or withdrawing consent, may adversely affect certain features and functions.
The technical storage or access is strictly necessary for the legitimate purpose of enabling the use of a specific service explicitly requested by the subscriber or user, or for the sole purpose of carrying out the transmission of a communication over an electronic communications network.
The technical storage or access is necessary for the legitimate purpose of storing preferences that are not requested by the subscriber or user.
The technical storage or access that is used exclusively for statistical purposes.
The technical storage or access that is used exclusively for anonymous statistical purposes. Without a subpoena, voluntary compliance on the part of your Internet Service Provider, or additional records from a third party, information stored or retrieved for this purpose alone cannot usually be used to identify you.
The technical storage or access is required to create user profiles to send advertising, or to track the user on a website or across several websites for similar marketing purposes.
Haki za Kibinadamu
Utangulizi
Kila binadamu katika ulimwengu huu ana haki zake ambazo zinastahili kuheshimiwa. Wewe unastahili kuheshimu haki za wengine na wengine wanastahili kuheshimu haki zako. Je, wewe unajua haki zako? Je, unajua haki za wengine? Ukikuta mtu, kwa mfano, akinyanyasa mtoto asiye na hatia, unajua anachostahili kufanya? Mada hii itakuwezesha kujifunza juu ya haki za binadamu na jinsi ya kulinda haki hizo. Pia, utanufaika na mafunzo haya ili kuheshimu haki zako na haki za watu wengeine kwa ajili ya kuishi
katika jamii kwa umoja na ushirikiano.
Stadi za lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo a: Kutambua msamiati unaohusiana na haki za binadamu
Utangulizi
Kila mtu duniani ana haki zake. Hastahili hata kamwe kunyimwa haki zake. Je, umewahi kuwa njiani unatembea na mtu bila kutarajia akakusukuma kando ya barabara? Unahisije baada ya kusukumwa? Je, umewahi kuhudhuria mikutano, kusikia au kusikiliza juu ya habari za haki za binadamu? Je,
unaweza kutambua baadhi ya mambo ambayo hutendeka kuonyesha ukuzaji au udunishaji wa haki za binadamu? Katika funzo hili, utajifunza msamiati unaohusiana na haki za binadamu ambao utakuwezesha kukuza, kuendeleza na kutetea haki zako na za wengine.
1.Shughuli 4.1
Kutaja maneno yenye uhusiano na haki za binadamuKatika makundi tambua misamiati angalu kumi inayohusiana na haki za kibinadamu.
2.Tungeni sentensi angalau tano kuonyesha matumizi ya misamiati inayohusiana na haki za binadamu
3.Tazameni kwa makini picha zifuatazo na kueleza kinachotendeka katika kila picha.
Stadi za lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo b: Kueleza njia mbalimbali za ukiukaji wa haki
za binadamu
Utangulizi
Watu wakubwa kwa wadogo, wasichana kwa wavulana mara nyingihukumbwa na janga la ukiukaji wa haki za binadamu. Je, umewahi kutambua njia mbalimbali ambazo husababisha haki za binadamu? Umewahi kupatwa na ukiukaji wa haki za binadamu? Je unaweza kutambua njia mbalimbali ambazo husababisha ukiukaji wa haki za binadamu? Funzo hili Iitakuwezesha kutambua na kueleza jinsi haki za binadamu zinavyokiukwa. Mwishoni, utakuwa mmoja wa wale watakaokuwa wanatetea haki za binadamu.
1.Shughuli 4.2
Kuorodhesha mifano ya njia mbalimbali za ukiukaji
wa haki za binadamu
1.Katika vikundi, orodhesheni njia mbalimbali za ukiukaji wa hakiza binadamu kwenye karatasi.
2.Wasilisheni matokeo yenu mbele ya wanafunzi darasani.
Kuorodhesha mifano ya njia mbalimbali za ukiukaji
Shughuli 4.3
wa haki za binadamu
Katika vikundi, elezeni njia mbalimbali za ukiukaji wa haki za binadamu.
2.Tambueni njia mbalimbali za ukiukaji wa haki za kibinadamu ambazouliwahi kushuhudia katika jamii yako.
3.Tazameni kwa makini picha hizi na kutambua ukiukaji wa haki zabinadamu unaotendeka.
Taz: Umetambua kuwa kila binadamu ana haki, wewe ukiwemo. Kwa hiyo, haki hizo zinafaa kulindwa. Ikiwa haki ni za Sisi sote basi sote tushiriki katika kuzilinda
Stadi za lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo c: kufafanuajinsihakizabinadamuzinavyokiukwa
kupitia kwa maigizo
Utangulizi
Njia mojawapo ya kuwasilisha ujumbe wowote ni kupitia maigizo. Je, wewe umewahi kushiriki katika maigizo yoyote? Ulikuwa unaigiza juu ya nini? Ni watu wa aina gani waliotazama maigizo yenu? Lengo la mchezo wenu lilikuwa ni nini hasa? Mada ndogo hii itakuwezesha kupitisha ujumbe wako wa haki
za binadamu kupitia maigizo. Utaigiza juu ya haki za binadamu ili jamii ipate kulinda haki za binadamu.
Kusimulia hadithi ya biashara ya watumwa
walionyimwa haki zao
Shughuli 4.4
Kuigiza mchezo juu ya ukiukaji wa haki za binadamu
idadi, vikundi viwili viungane viunde kikundi kimoja.
Taz: Umejifunza kuwa watumwa wengi wamenyimwa haki yao katika majukumuwanayopewa. Miongoni mwa watumwa hawa ni wafanyakazi manyumbani kwetu. Wengine ni wale ambao wanatoka nje ya nchi yetu na wanapofika huko wanauwawa, wananyimwa chakula, maji, vitu vyao kuchukuliwa, haki za kutembea n.k. Umejifunza kuwa ukiukaji wa haki za binadamu ni kinyume
na sheria. Umetambua kuwa ni jukumu letu kuthamini, kujali, kuwaheshimu na kuwajibika kuripoti ukiukaji wa haki za binadamu.
Stadi za lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo d: Kutambua mashirika ya utetezi wa haki za binadamu
Utangulizi
Kuna mashirika ya kijamii, kitaifa na kimataifa ambayo kazi yake ni kutetea haki za binadamu. Je, kuna watu au mashirika yoyote unayotambua katika jamii yako au nchi yako ambayo hujishughulisha na utetezi wa haki za binadamu? Je, unaweza kuyatambua mashirika hayo, mahali yanakopatiakana na hata nembo au alama ya kuliwakilisha shirika hilo? Mada ndogo hii itakuwezesha kutambua mashirika
yanayojihusisha na utetezi wa haki za binadamu na michango ya kila shirika.
Kutambua na kutaja mifano ya mashirikayanayotetea haki za binadamu
Tazama kwa makini nembo za mashirika yanayotetea haki za binadamu.
Stadi za lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo e: Kutathimini jinsi Mashirika yanavyotekeleza haki za binadamu
Utangulizi
Mashirika ya kuendeleza haki za binadamu ni mengi. Hata hivyo, unastahilikuelewa kuwa kila shirika huwa na dhima yake. Je, unaweza kutambua shirika la utetezi wa haki za binadamu katika nchi yako? ikiw unatambue, je unaweza kueleza dhima ya shirika hilo? Katika funzo hili, utaeleza dhima ya mashirika
ya utetezi wa haki za binadamu ili kujali, kuwajibika, na kuthamini majukumu ya mashirika haya katika jamii zetu.
Kueleza dhima za mashirika yanayotetea haki zabinadamu
2.Tathmini huduma zinazotolewa na mashirika ya utetezi wa binadamu,ukionyesha ikiwa yamefaulu au yameshindwa.
3.Katika vikundi vyenu, nendeni mtandaoni au maktabani na kufanya utafitizaidi ili kutambua jinsi mashirika yanavyotekeleza haki za binadamu.
Taz: Mashirika yanayopigania haki za binadamu pia yanahitaji kusaidiwa kwa kuyapasha habari. Kwa mfano, ukimkuta mtu ananyanyasa mwingine, ni jukumu lako kuwapasha ujumbe viongozi wa kijiji chako au polisi au shirika
jingine unalojua. Mashirika mengine huwa yanaacha nambari za simu ili tuwapigie simu tukishuhudia ukiukaji wa haki za binadamu. Kile ambacho unastahi kutambua ni kuwa kila shirika lina lengo lake na huweza kutoa huduma tofauti tofauti kutegemea malengo yake ya jumla. Huwezi kupata
shirika ambalo linafanya kila kitu.
Stadi za lugha: Kusoma
Funzo f: Kusoma makala yanayohusubinadamu na kujibu maswali
Utangulizi
Biashara ya utumwa ni biashara ambayo ilikuwepo kabla ya ukoloni. Hata hivyo,unatambua kuwa biashara hizi vimekuwa vikibadilika kila karne? Je unaweza kueleza baadhi ya mabadiliko hayo? Katika sehemu hii ya mada, utasoma makala ili kuweza kutambua mabadiliko yaliyotokea kuhusiana na biashara ya
utumwa kwa ajili ya kushauri, kujihadhari na kuripoti wahanga wa usafirishaji wa watumwa kiharamu na kulinda nchi yetu dhidi ya uvunjaji wa haki za binadamu.
Kusoma makala yanayohusu biashara vya utumwa
Shughuli 4.8
katika karne 19
Soma makala haya kwa makini na kujibu maswali yanayofuata.Biashara ya utumwa ni uuzaji na ununuzi wa watu kwa ajili ya masilahi ya kibinafsi. Biashara hii siku hizi ni tofauti sana na jinsi ilivyokuwa zamani. Katika kame hii, tunashuhudia utumikizi wa watu kama wafanyakazi. Biashara ya ngono, biashara ya kununua sehemu nyeti za miili ya binadamu kama vile figo, macho, maini, ubongo, na kadhalika. Idadi ya watumwa kote ulimwenguni haijulikani. Hata hivyo takwimu zinazojitokeza ni takwimu kati ya ilioni ishirini na moja na kuendelea.
Utumwa katika karne hizi hujitokeza zaidi pale ambapo kuna mtu hasa tajiri anamtumia mwenzake kumfanyia kazi kwa masharti, nguvu na uwezo wa kumiliki kwa lengo la kujinufaisha. Mara nyingi matendo haya hufanyika kwa njia haramu na iliyo ya Siri. Mashirika na kampuni zinazoshiriki katika biashara hii wakati mwingi huwa hazitambuliki wazi. Nyingine huwadanganya vijana kuwatafutia kazi na huishia kuwaua au kuwalazimisha mapenzi.
Mara nyingi watu wanaotekwa katika biashara hii ni watoto, vijana wa kike wa umri wa miaka kati ya 12 na 20. Watu wengine ambao wanajikuta wametekwa katika biashara hii ni kama vijana wa kiume wanaotaka kujipatia riziki ya maisha, watu walio maskini, wananchi wanaotoka katika nchi zenye mitafaruku au vita
vya ndani kwa ndani, raia wa nchi maskini kiuchumi na nchi ambazo masuala ya sheria na miundo mbinu ya kijamii bado inaendelea kukua. Zaidi ya yote ni suala la elimu wananchi walio nayo. Wananchi ambao hawakusoma au
kushindwa kusoma mara nyingi huhasirika sana. Wanalazimishwa kufanyakazi za sulubu na kwa sababu hawana uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa, utumwa unawapata katika hall ya kutojielewa; kati ya maisha na mahitaji. Katlka kame hii. wahanga wa usafirishaji haramu wa binadamu hutumia mbinu ambazo ni za kuvunja sheria za haki za binadamu kuwasafirisha binadamu. Wao hulipa hongo, kuwalazimisha binadamu kutembea kwa mwend0 hadi eneo fulani. kuwafiCha kwenye madhehewa, malori, kuwasafirisha usiku,
wakati wa mvua au baridi wakiepuka kushikwa na serikali au mashirika yanayohusika na haki za kibinadamu.
Usafirishaji haramu wa binadamu ni uhalifu unaohusisha unyonyaji wa haki za watoto kwa ajili ya biashara ya ngono, wa watu wazima kwenye biashara ya ngono kwa njia ya kulazimishwa, biashara haramu ya viungo vya binadamu. udanganyifu, au masharti, na wa mtu yeyote kwa kazi ya kulazimishwa. Watu wanaojihusisha na unyonyaji kama huo, kujumlisha wasafirishaji haramu wa watanyakazi, makuwadi na wanunuzi wa biashara ya ngono. Katika karne hii, kumetokea mashirika ya kibinafsi ambayo
hutumika katika nchi kama mashirika yasiyo ya kiserikali yenye kuto huduma kwa wananchi kwa niaba ya serikali.
Matokeo ni kuwa maiti ya miili ya wananchi, kupotea kwa wananchi kunaripotiwa kupdia katika mitandao ya isimu jamii. Tumekuwa tukiShuhudia ukatili amba*) wasichana wanalazimishwa kulala la zaidi ya mwanamme mmoja. Wanaume wenyewe wanaonyesha ukatili na wanataka kuwa na mapenzi kama watakavyo, kuwapiga na hata kuwauwa. Makosa ya jinai yanafanywa na hata hakuna mash’rika ya serikali inayojitokeza kutetea haki za watu wake.
Kuna mengi ya mashirika kuzungumzia juu ya biashara ya utumwa wa karne hii. Watu wanafanyishwa kazi kwa muda mrefu na kwa mshahara duni usioweza kumsaidla mtumwa kujikomtm kutoka katika hali yake. Huu ni mtano wa biashara ya utumwa wa wafanyikazi. Utumwa wa aina huu huhusisha hata
baadhi ya serikali kushirikiana na wadau wanaoomba watanyakazi kutoka katika nchi zao. Aidha ndoa ya kwa watoto wa kike. wafungwa kufanyishwa kazi za sulubu bila kama adhabu, kuhamishwa kwa lazima
kwenda kufanya kazi katika mazingira yenye ukatili nakadhalika. Kweli karne hii ni karne utumwa na bisahara vya utumwa ni vya
kisasa. Utumwa huu umetandawishwa na kila eneo la dunia utasikia watumwa wakilalamika kutokana na kutumikishwa na kunyonywa damu. Tunafaa kukaa macho na kujiuliza jinsi ya kuepukana na biashara ya aina hii. Ndiyo ninahitaji kazi lakini ni kampuni gani itakufaa? Fanya uchunguzi wa kina wa kibinafsi
wa mashirika na serikali unakokwenda kabla ya kukubali kuhamishwa au kuuzwa kwa miteni ya shilingi bila kutambua.
1.Shughuli 4.9 Jibu maswali haya baada ya kusoma makala
1.Katika makundi, jadiliana na wenzako kuhusu ujumbe wa makala haya.
2.Elezeni maana ya biashara ya utumwa
3.Je, biashara ya utumwa katika karne ya 19 ni biashara iliyo nalengo gani?
4.Ni watu wa aina gani wanaohasirika na biashara ya utumwa katikakarne ya 19?
5.Je, unaweza kutambua mbinu zinazotumika katika utekelezaji wabiashara ya utumwa katika karne ya 19?
6.Ni matokeo gani ambayo hujitokeza kutokana na biashara za utumwa katika karne 19?
7.Katika vikundi, eleza kwa kifupi kuhusu biashara ya utumwa katika karne ya 19.
Stadi za lugha: Kusoma na Kuandika
Funzo g: Sarufi – Kueleza unominishaji wa vitenzi na
kutumia katika sentensi
Utangulizi
Katika lugha ya Kiswahili, kuna hali ambapo maneno hüweza kuundwa kutokana na maneno mengine. Vitenzi vinaweza kugeuzwa na kufanywa nomino au kinyume. Je, umewahi kutambua baadhi ya maneno ambayo huundwa kutokana na vitenzi? Je, unaweza kueleza hali hii ya uundaji wa maneno? Mada ndogo hii itakuwezesha kuunda nomino kutoka kwa vitenzi, na kuzitumia katika mawasiliano yako ya kila siku.
Kueleza dhana ya unominishaji wa vitenzi
Katika vikundi, tambueni angalau vitenzi vitano mnavyotumia sana katika shughuli zenu za kila siku.
2.Tazameni picha hizi na kutambua kitendo na nomino yake
3.Tofautisha maneno yafuatayo na kueleza kama ni vitenzi au nomino
a) Piga
b) Pendo
c) Pamba
d) Fundisho
e) Jengo
Taz: Katika funzo hili, umejifunza kuwa Unominishaji wa vitenzi ni hali ya
1.kugeuza kitenzi na kukifanya kuwa nomino. Ni ile hali ya kuunda nominokutoka katika kategoria ya vitenzi. Katika unominishaji, umetambua kuwa
vitenzi vinaweza kunominishwa kwa njia kadhaa:
2.kiambishi (-0) hutumika badala ya kiambishi I-a) cha kibantu hasa kuundonomino zinazotokana na vitenzi vya kibantu.
sauti /i-/ au /-li-/ huongezwa kwa baadhi ya vitenzi vya kibantu kuunda
nomino. Hii hali ya kuongeza sauti hizi inaitwa uundaji wa nomino kutoka
kwa vitenzi nyambulishi.
3.kuambatanisha sauti /e-/ na /-o
4.kwa kuongeza viambishi nyuma ama mbele na kuongeza kiambishi /-m-/ nyuma na /-ji-/ mwishoni mwa mzizi.
5.Mkiwa katika vikundi, someni maelezo yafuatayo na kutoa mifano mitano kwa kila kategoria za hapo juu.
Stadi za lugha: kusoma na kuandika
Funzo h: Kubainisha maana mbaimbali kutoka kila vitawe
Utangulizi
Je, umewahi kutumia neno moja katika mazingira tofauti? Ni nini ambacho uliwahi kutambua. Katika lugha ya Kiswahili, kuna maneno ambayo huwa na maana zaidi ya moja, unaweza kutambua baadhi ya aina ya maneno kama hayo? Unaenda kutambua baadhi ya maneno kama haya katika funzo hili na
hata kuyatumia katika mawasiliano yako kwa urahisi.
Shughuli 4.11
1.kutambua vitawe na kueleza maana yake kwa kutumia sentensi
1.Katika vikundi tambueni maneno kumi ambayo yana maana zaidi ya moja.
2.Kwa kutumia kamusi maktabani, mtandaoni, simu au tarakilishi ya mkono tambueni maana ya maneno yafuatayo.
c) fua
b) paa
a) kaa
3.Tambueni neno moja ambalo lina maana zifuatazo:
a) kaa au chukua muda mrefu mahal fulani au ongoza katika shindano.
b) Mnyama katika familia ya paa anayefugwa nyumbani au Chombo cha kukunia nazi.
c) nyama mkubwa porini/ndovu au Kileweshi au pombe.
Tungeni sentensi mbili kuonyesha maana tofauti za maneno yafuatayo:
b) Mlango c) Mbuni, d) kiboko
a) Vua
Taz: Umegundua kuwa vitawe ni maneno yenye maana zaidi ya moja. Katika funzo hili umetambua kuwa kuna maneno mengi ambayo huwa na maana zaidi ya moja katika lugha ya Kiswahili. Aidha, inafaa utambue kuwa watu wanapotumia maneno kama haya, ni lazima utambue muktadha wa matumizi
yake ili kutambua maana kamili.
Stadi za lugha: Kusoma na kuandika
Funzo i: Kutumia nomino a ngeli ya u-u katika sentensi
Utangulizi
Ngeli ni makundi ya majina. Katika lugha ya Kiswahili, ulijifunza katika kidato cha kwanza na pili kuhusu ngeli. Je, ni nini ambacho unatambua kuhusiana na uainishaji wa nomino? Je, unaweza kutambua nomino katika ngeli ya u-u? Majina katika ngeli ya u-u ni majina ya aina gani? Je, unaweza kutunga sentensi
kuonyesha matumzi ya nomino katika ngeli hii? Mada ndogo hii itakuwezesha kutambua na kutumia nomino za ngeli ya u-u kwa usahihi.
Kutumia nomino za ngeli ya u-u katika sentensi
c) Ugoro
a) Ugali
b) Ujima
Taz: Ni mambo gani ambayo ulijifunza kutokana na ngeli ya u-u? Unastahili kutambua kuwa ngeli ya u-u huhusisha majina ya nomino za wingi yanayoanzakwa kiambishi u. Kuna aina mbili kuu ya majina katika ngeli hii. Nomino za maneno yanayoonyesha hali ya jambo au kitu (dhahania). Maneno haya
huanza kwa kiambishi u au w. Aina ya pili ni ya nomino za vitu visivyohesabika
Fasihi simulizi
Stadi za lugha: Kusoma, Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo j: Kujadili jinsi haki za binadamu zinavyokiukwa
katika hadithi fupi
Utangulizi
Hadithi tunazosimuliwa, kusikia au kusoma katika vitabu, magazeti na hata katika majarida ni hadithi ambazo hutupa ujumbe wa hali ya maisha katika jamii. Umewahi kuhadithiwa ama kusoma hadithi ambazo zinahusiana na haki za binadamu? Je, ulijihisi Vipi kuhusiana na hadithi uliyosoma? Mada ndogo hii itakuwezesha kusoma hadithi kuhusu jinsi haki za binadamu zinavyokiukwa.
Kusoma hadithi kuhusu haki za binadamu Soma hadithi ifuatayo kwa makini na kisha ujibu maswali yanayofuata. Ssemakokilo alikuwa mtoto wa Bwana Ssekulya na Bi Mutoni. Mtoto huyu alikuwa mtoto wa pekee wa familia hii. Kwa kotobahatika, mamake Semakokilo aliaga dunia kwa ajali ya barabarani. Ilikuwa huzuni kwa baba na mtoto kumpoteza mlezi wao. Bwana Ssekulya aliishi na mtoto wake kwa
upweke huku wakitokwa na machozi ya kwikwikwi. Waliokuwa wakila mapema wakaanza kula wamechelewa. Waliokuwa wakila chakula kitamu wakaanza kula chakula ambacho kilikuwa aidha kibichi au chumvi kuzidishwa. Hali hii ilikuwa ngumu sana. Baba na mtoto wakakubaliana kumpata msaidizi. Hata
hivyo yaliyojiri baadaye yalikuwa ya kuhuzunisha zaidi.
Mama Kambilingisa alikuwa chaguo zuri kwa wote. Mama huyu alikuwarafiki wa dhati wa Bi Mutoni. Alikuwa akiwatembelea wakati fulani fulani kwa gumzo na mamake Semakokilo. Hata hivyo, Mama Kambilingisa alikuwa hajabahatika kupata jiko. Alikuwa akimsubiri mpenzi wake aliyekwenda
ughaibuni. Hata baada ya miaka na mikaka ya subira yavuta heri, mpenzi wake hakurudi. Alimhini haki ya mapenzi yake. Alikuwa amekata tamaa na kuingia mawindoni kumtafuta wa kumwoa kabla macho yake kuingia giza Bwana Sekulya, kwa msaada wa .rafiki yake wa kufa kuzikana Bwana Masumbuko, walienda kwa wazazi na kwa furaha, mama Kambilingisa akapata faraja. Karamu ya kufukuza ukapera ikafanyika na mama Kambilingisa akajikuta kwa boma la rafikiye bila kujua. Aligombana ila mahari yalikuwa
yamelipwa. Alikasirishwa sana na Bwana Masumbuko aliyemdanganya kuhusu mtu aliyekuwa anamjua. Mwisho alikubali nafasi yake ya kumlinda Semakokilo na Bwana Sekulya
Kwa mara ya kwanza, Mama Kambilingisa alionyesha mapenzi ya dhati kwa familia yake mpya. Alifanya kazi kwa bidii na kwa kuwa alikuwa mpishi hodari. Mambo hayakwenda mrama wakati wa chamcha na chajio. Kila mara furaha ilikuwa imejaa furifuri katika nyuso ya familia hii. Baada ya miaka miwili, Mama Kambilingisa alibahatika kumpata mtoto wa kike na akaitwa jina la Bahati na la ukoo akaitwa Sekulya.
Mara mama akaingiwa ushetani wa ajabu. Akaanza kumchukia Semakokilo. Akawa anampiga, anamtuma kila wakati na tena kwa hasira; kumbebesha mizigo na kumtupia matusi ya kuhuzunisha. Hali hii iliendelea sana hadi Bahati akamwuliza mamake shida yake. Alimwomba kumheshimu, kumtunza na kumkimu Semakokilo kama afanyavyo kwake. Hata hivyo, masikio yamama yalikuwa yemewekewa nta, hakusikia la mwadhini wala la mteka maji. Alizidisha kumnyima chakula, kumpiga, kumchoma moto na hata wakati
mwingine kunyimwa kwenda shuleni.
Siku moja, babake Bahati na Semakokilo walienda malishoni. Kufika malishoni, semakokilo alitumwa kurudi nyumbani kuleta mkeka. Semakokilo alipofika, mama Semakokilo hakusubiri kumuuliza kilichomrudisha nyumbani. Alimzaba kofi, mvulana akayumbayumba, akaanguka na kisha kuzirai. Mama
mtu hakujali wala kukubali, alizidi kumchuna masikio na kumwona kama alikuwa anajidanganya. Baada ya muda, akamshika mtoto na kutambua kuwa kweli alikuwa katika hali mahututi. Mama mtu hakuwa na la kusema. Hakuwa na mbele wala nyuma. Kuona kuwa hali ni mbaya, mama mtu alitoroka. Alijificha katika shamba la jirani, migombani.
Migombani alikutana na joka kubwa lililomuuliza alikokuwa akienda. Joka lilimuuliza kitendo alichokifanya nyumbani. Kwa kupigwa na butwaa, hakuwa na la kunena. Mara Joka likazidi kumkaribia. Chini lilikuwa na miguu ya binadamu, juu kichwa cha Joka. Likazidi kumkaribia sura ikizidi kubadilika. Mama Kambilingisa alikimbia na kurudi nyumbani. Aliwakuta watu wakiwa wamekusanyika bomani na kusikitika kwa kitendo kibaya cha kumhini Semakokilo haki za binadamu. Alipofika, kijiji kizima kilikuwa tayari kumwangamiza. Alizabwa makofi, mateke, ngumi na watu waliokuwa na hasira kwa kitendo chake cha ukatili. Hata hivyo, walitambua kuwa haikuwa haki yao kumwua wala kumwadhibu kwani kujichukulia sheria mikononi ni
hatia ya uvunjaji wa haki za binadamu. Polisi waliitwa. Mama akashikwa na kuweka mbaroni kwa kuvunja haki za yatima. Bahati alimweleza mamake kushika adabu na kuheshimu haki za watoto. Alimhurumia ila tu alimkejeli, mama, siku za mwizi ni arubaini. Nilikueleza kuheshimu haki ya kakangu. Sasa uone. Hujielewi. Pole na haki itendwe kwako.
Mama Kambilingisa alilia kwa ghadhabu. Alikubali hatia ya kumnyanyasa mtoto wa marehemu rafiki yake. Alipiga magoti mbele ya umati na kuomba msamaha, Semakokilo alipelekwa hospitalini na ikatambulika kuwa atakuwa salama. Baada ya siku mbili alirudi nyumbani. Mama alifungwajela kwa miaka kumi na mitatu. Shirika la utetezi wa haki za binadamu lilikubali kumsaidia Semakokilo. Baada ya mika kumi na mitatu, mamake Bahati alirudi nyumbani akiwa ameshika adabu. Bwana Sekulya, Bahati na Semakokilo walimkaribisha na kumwomba asirudie tena matendo ya kuvunja haki za binadamu. Kuanzia siku hiyo mama mtu alikula yamini kulinda haki za watu wote na hata mifugo. Sasa wanaishi maisha ya raha
mstarehe bila uvunjaji wa sheria. Mama Kambilingisa sasa ni mshauri wahaki za watoto katika kijiji chao cha Mtemakuni.
Jibu maswali
a)Wahusika katika hadithi hii ni kina nani? Elezea
b)Ni mambo gani mnayotambua katika hadithi?
c)Tambua wahusika ambao walionekana kuvunja haki za binadamu katika hadithi.
d)Ingawa Mamake Bahati alivunja haki, naye alivunjiwa haki za binadamu, elezea Katika vikudi jadilianajinsi haki zinavyokiukwa katika hadithi hii
Taz: Umejifunza kuwa ukiukaji wa haki za binadamu ni hali ya kuwanyima watu haki zao. Umeelewa kuwa haki za watoto katika jamii zetu hukiukwa na watu wasio na huruma. Miongoni mwa watoto wengi wanaonyanyaswa ni
mayatima. Aidha, umetambua kuwa kuna haki nyingi zinazovunjw kuanzia kwa haki ya maisha, kiuchumi, kielimu, kidemokrasia na hata kijamii. Vile vile, ulitambua kuwa hata wanavunja sheria nao hupatwa na majanga ya kuvunjiwa haki zao. Katika muktadha huu, naamiini umejifunza kulinda haki za binadamu. Usipolinda haki za binadamu huenda ukapatwa na adabu kwani ni ukiukaji wa sheria za nchi na jamii.
Stadi za Lugha: Kuandika
Funzo k: Kuandika insha ya methali
Utangulizi
Insha ya methali ni insha ambayo husimulia kisa kinachohusiana na maanaya ndani ya methali. Methali hufumba maana ya ndani yenye funzo kwa jamii. Umewahi kusoma hadithi au kusimuliwa hadithi ambayo ni kichwa cha methali? Je unatambua muundo wa uandishi wa insha ya methali? Unaenda kuelekezwa kuandika insha ya methali na baada ya mwongozo, utaweza kuandika insha ya methali.
Shughuli 4.15 Kuandika insha ya methali
1.Katika vikundi, elezeni maana ya juu na ndani ya methali, ‘Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.’
2.Elezeni funzo au ushauri unaojitokeza katika methali hiyo.
3.Jadiliana kuhusu hatua za kufuatwa wakati wa kuandika insha ya methali.
4.Baada ya kutambua maana na funzo, andika insha ya methali ya,’Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.’
5.Iwasilishe insha hiyo mbele ya wanafunzi wa darasa lako.
Taz: Katika uandishi wa insha ya methali, mwandishi lazima azingatie pande mbili. Ni lazima sehemu zote zipewa uzito sawa. Hii inatokana na kuwa sehemu ya kwanza hutoa wazo na sehemu ya pili kutoa jawabu au kukamilisha wazo, suluhisho au matokeo ya kisa kutokana na methali. Aidha, unastahili kujua
kuwa kuelewa maana ya methali ni muhimu sana kabla ya kuandika insha.
Mfano wa Shughuli Jumlishi
Bwana Katwanga amekuwa akifanya biashara ya utumwa kwa miaka mingi.Kutokana na tajiriba yake katika biashara hii, ametambua mengi kuhusiana na ukiukaji wa haki za binadamu. Amekuwa akijaribu kuepukana na hali hii lakini ameshindwa aanzie wapi. Asichojua ni kwamba kazi anayofanya ni
haramu, inavunja sheria
Muhtasari wa mada
Katika mada hii, umejifunza juu ya:
Maneno yenye uhusiano na haki za binadamu
Njia mbalimbali za ukiukaji wa haki za binadamu
Jinsi haki za binadamu zinavyokiukwa kupitia maigizo
Mashirika ya utetezi wa haki za binadamu
Jinsi mashirika yanavyotekeleza haki za binadamu
Kusoma makala kuhusu haki za binadamu na kujibu maswali
Unominishaji wa vitenzi na kutumia nomino hizo katika sentensi
Maana mbalimbali za vitawe
Nomino za ngeli ya u-u katika sentensi
Jinsi haki zinavyokiukwa katika hadithi fupi
Insha ya methali
Assignment
ASSIGNMENT : Mfano wa Shughuli jumlishi juuHaki za Kibinadamu MARKS : 10 DURATION : 1 week, 3 days