• LOGIN
  • No products in the cart.

Uongozi wa Kitaifa

Uongozi wa Kitaifa

Utangulizi
Kila taifa huwa linahitaji kuwa na uongozi. Bila uongozi, taifa lingepoteza mwelekeo na kuwa na mitataruku. misuguano na vita visivyoisha. Si taifa pekee. bali kila kundi la watu popote lilipo, huwa linahitaji uongozi wa kuratibu masuala yake. Je. unajua viongozi wa nchi yako? Je, unajua umuhimu wa
kuwa na viongozi? Nembo ya nchi yako unaijua kweli? Umebahatika. Mada hii itakuwezesha kujua viongozi wako na umuhimu wa kuwa na viongozi. Itakuwezesha kujua maana ya nembo za nchi yako na kwa nini ilipangwa hivyo. Aidha. mada itakuwezesha kuthamini viongozi, kujenga uzalendo, kuwajibika
na kushiriki katika shughuli za uongozi katika jamii yako.
Stadi za Lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo a: Kutambua msamiati wa uongozi wa taifa na ala za uongozi
Utangulizi

Kila nchi au taifa huwa na uongozi. Na kila uongozi huwa na ala ambazo hutumika kuwakilisha uongozi wa taifa. Je, umewahi kutambua kuwa kungekuwa na taifa bila uongozi na ala za uogozi halingekuwa taifa? Je, unatambua kuwa kila nchi ina misamiati ya uongozi na ala ambavyo hutofautiana na nchi nyinginezo? Katika mada hii, utatambua msamiati wa uongozi na ala za uongozi.
Msamiati wa uongozi
Shughuli 5.1 Kutambua msamiati wa uongozi wa taifa

  1. Katika vikundi, tazameni picha zifuatazo na kutambua neno linalorejelea picha hiyo.

Kwa kutumia kamusi, tambueni msamiati unaorejelea kazi ambazo viongozi wafuatao hufanya.

Msamiati wa ala za uongozi
Kutambua msamiati wa ala za uongozi

  1. Katika vikundi, shirikiana na kujadiliana kuhusu msamiati wa ala zauongozi na kuwasilisha darasani.

Taz:
2.Tungeni sentensi tano mkitumia misamiati mliyotambua.
3.Tumieni mtandao kutambua ala za uongozi.
Kila nchi huwa na uongozi ambao huwakilishwa na ala za uongozi. Umeweza kutambua kuwa wimbo wa taifa na ofisi mbalimbali za uongozi ni miongoni mwa msamiati unaowakilisha uongozi.
Kujua uongozi wa nchi yako na ala za uongozi wa nchi yako ni ishara ya uzalendo, kujali, kuthamini na kuwajibika. Hii ndiyo sababu watu huimba wimbo wa taifa kwa kusimama wima ili kuheshimu nchi yao na kuwaheshimu viongozi.

Tungeni sentensi tano mkitumia misamiati mliyotambua.
Tumieni mtandao kutambua ala za uongozi.
Kila nchi huwa na uongozi ambao huwakilishwa na ala za uongozi.
Umeweza kutambua kuwa wimbo wa taifa na ofisi mbalimbali za uongozi
ni miongoni mwa msamiati unaowakilisha uongozi.
Kujua uongozi wa nchi yako na ala za uongozi wa nchi yako ni ishara ya
uzalendo, kujali, kuthamini na kuwajibika. Hii ndiyo sababu watu huimba wimbo
wa taifa kwa kusimama wima ili kuheshimu nchi yao na kuwaheshimu viongozi.

Stadi za lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo b: Kufafanua nyadhifa za viongozi mbalimbali
Utangulizi

Nyadhifa za uongozi ni nafasi mbalimbali za majukumu au ofisi za watu. Kila nchi au jamii yoyote huwa na nyadhifa mbalimbali katika uongozi wake. Kila kiongozi ambaye hushika wadhifa fulani hushiriki katika utekelezaji wa majukumu ya kujenga nchi. Je, unatambua nyidhifa za viongozi mbalimbali katika jamii yako au shuleni? Nyumbani kwenu, unaweza kutambua wadhifa wako na majukumu yako? Je, umewahi kugombea wadhifa ya uongozi shuleni? Ni wadhifa gani uliogombea? Je, uliweza kushinda? Katika eneo-bunge lako, umewahi kuona watu wakigombea kuwa wabunge? Hizo nafasi ulizotaja ndizo zinazoitwa
nyadhifa za viongozi. Katika mada hii, utajifunza juu ya nyadhifa za viongozi mbalimbali, huenda na wewe siku zijazo, utachukua wadhifa fulani.

Shughuli 5.3
Kufafanua nyadhifa za viongozi mbalimbali
Katika vikundi, tazameni kwa makini picha zifuatazo na kutambua
wadhifa wa kila kiongozi.

2.Katika vikundi, orodhesheni nyadhifa za uongozi katika viwango vifuatavyo:
i) Kijiji
ii) Wilaya
iii) Wizara
iv) Bunge
v) Nchi
3.Elezeni nyadhifa za uongozi mlizozitambua katia swali la 1.
4.Kwa maoni yenu, kwa nini ni muhimu kutambua nyadhifa za uongozi katika jamii yako?
Taz: Katika sura hii, umetambua nyadhifa mbalimbali na kuelezea nyadhigfa husika. Nyadhifa hizi nyingi ni za kisiasa, nyingine ni za majukumu ya watu katika utekelezaji wa huduma za serikali kwa jamii, nyingine ni majukumu ya kijamii kama vile kushauri jamii, nyadhifa za kidini, nyadhifa za kielimu shuleni na chuoni nakadhalika.

Stadi za lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo c: Kutambua dhima za nembo
ya kitaifa
Utangulizi

Nembo ni muhimu sana. Nembo huitambulisha nchi fulani. Je, unaweza kutambua nembo ya taifa la Uganda na Jumuiya ya Afrika Mashariki? Katika mada ndogo hii, utajifunza juu ya nembo ya taifa la Uganda.

1.Shughuli 5.4 Kueleza umuhimu wa nembo
Katika vikundi, tazameni nembo ya taifa la Uganda kisha mweleze mnachoona.
Jadiliana katika vikundi vyenu na kisha kila kikundi kiwasilishe dhima za nembo ambazo kilijadili.
Tambueni viungo vya nembo ya Uganda na kufafanua maana na umuhimu wa kila kiungo.

Taz: Umetambua kuwa nembo ya Uganda ina dhima nyingi katika maisha ya wananchi wa Uganda. Wananchi huheshimu nembo hii kwa sababu ni ala ya uongozi na utaifa wa Uganda. Ni furaha kuwa nembo yetu inazungumzia mengi kuhusiana na nchi yetu. Utaiheshimu, kujali na kuwajibika kwa ajili ya kujenga utaifa na uzalendo.

Stadi za lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo d: Kudhihirisha shughuli mbalimbali katika kampeni
Utangulizi

Kampeni za uchaguzi zinahusu utafutaji wa kura ili kuweza kuchukua wadhifa katika uongozi. Kampeni hizi mara nyingi huwa za kidemokrasia ambapo, wagombeaji hutoa hoja za kujitetea ili kupewa nafasi ya uongozi. Je, umewahi kushiriki katika kampeni za uchaguzi wowote? Ni shughuli za aina gani ambazo
hujitokeza katika shughuli hii? Katika mada hii, utajifunza jinsi ya kupiga kampeni kwa kudhihirisha shughuli mbalimbali katika kampeni.

1.Chagueni mwanafunzi mmoja miongoni mwenu atakayesimamia mchakato mzima wa kampeni.
2.Undeni makundi matatu ya wanafunzi. Kila kundi lichague mwakilishi mmoja atakayeshiriki katika kugombea uongozi.
3.Wawakilishaji wa makundi wasimame mbele ya wanafunzi wakipiga kampeni, mmoja baada ya mwingine.

Shughuli 5.6Kudhihirisha shughuli zinazojitokeza katika kampeni

1.Katika vikundi, dhihirisheni shughuli mbalimbali zinazofanyika katika kampeni.
2.Ni shughuli gani nyinginezo unazoweza kutambua ambazo hazijadhihirishwa katika maigizo.
3.Katika vikundi igizeni shughuli mbalimbali ambazo mmetambua katika swali la kwanza hapo juu.

Taz: Baada ya kuigiza shughuli za kampeni, umetambua kuwa shughuli hizi huzingatia kanuni ambazo hutolewa na walinda usalama kwa ajili ya kulinda usalama. Katika kampeni kuna kuhakikisha kuwa kampeni zinatendeka kwa kuzingatia muda. Huhakikisha kampeni huepukana na uchochezi bali hujikita kwa uombaji kura kwa njia iliyo ya wazi, inayozingatia umoja na ushirikiano na uzalandeo. Vilevile umetambua kuwa katika kampeni kuna wanaokubali maoni yako, wanaoshangilia na hata wanaopinga maoni yako.

Stadi za lugha: Kusoma
Funzo e: Kusoma makala kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini na kujibu maswali

Utangulizi
Je, umewahi kushiriki katika uchaguzi wowote? Ulishiriki kama mshabiki au mgombea mwenyewe? Je, unaweza kusimulia wasiwasi unaokuwa nao wakati wa kuhesabu kura? Baada ya kutangaza matokeo, unafikiri mshindi na aliyeshindwa wanahisi vipi? Katika makala haya utasoma na kushuhudia matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchi.

Uchaguzi mkuu katika nchi yangu ni muhimu sana. Viongozi huchaguliwa kuwa madarakani kwa miaka mitano. Baada ya miaka mitano, katiba hukubali kuchaguliwa kwa viongozi wengine kugombea tena. Wale ambao walikuwa viongozi hapo awali pia nao wanaruhusiwa kugombea. Nyadhifa za kugombea
ni kama urais, ubunge, udiwani, uchifu na wazee wa mitaa na vijiji pamoja na viongozi wa halmashauri ya jiji ambao tunawaita meya.
Kama ilivyo desturi, uchaguzi wa urais na ubunge hufanyika kwanza ukifuatwa na uchaguzi wa mwenyekiti wa Wilaya kuendelea chini mpaka kwa kijiji. Matokeo ya uchaguzi hutangazwa kutoka katika vituo mbalimbali vya upigaji kura, kisha matokeo husukumwa katika ofisi ya uchaguzi ya Wilaya ambayo husukuma moja kwa moja matokeo hayo kwa kituo kikuu ambacho hutayarishwa katika uwanja wa Nambole.
Matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika jijini Kampala ni mfano mzuri wa kanuni za uchaguzi katika nchi. Wagombeaji wa vyama vya upinzani na chama kinachotawala walishiriki katika uchaguzi huu.

Watu wa rika zote; wazee kwa vijana, kina baba na kina mama, wasichana na wavulana waliamka asubuhi na mapema kwenda kupiga kura katika vituo vyao. Kila mpiga kura alikuwa na kadi ya usajili ya kumruhusu kupiga kura. Yeyote ambaye hakuwa na kadi ya usajili hakuruhusiwa kupiga kura. Vituo ambakyo kura hupigiwa huwa vinafunguliwa saa kumi na mbili na nusu asubuhi na
kufungwa saa kumi na moja jioni.
Upigaji kura wa mwaka huu ulianza saa moja kamili. Kila mpiga kura alistahili kukagua jina lake katika kitabu cha usajili na kisha jina hilo liliwekewa alama. Baada ya kuhakikisha kuwa wewe ni mpigaji kura halisi, ungepewa karatasi yenye picha za wagombea wote ili ujichagulie unayemtaka kuwa kiongozi
wako. Utaratibu huo ulifanyika katika kila kituo.

Kufikia saa kumi na mbili jioni, kura zilianza kuhesabika katika vituo mbalimbali amatokeo kutangazwa papo hapo na tume ya uchaguzi. Baada ya kuhesabu, kura zote zilijumlishwa na kisha mshindi akatangazwa moja kwa moja kwa redio, runinga na kwa umma bila mapendeleo. Utangazaji wa mshindi yeyote katika nchi hutangazwa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ambaye huajiriwa
kwa ajili ya kuongoza uchaguzi kwani amani bila mapendeleo. Matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita yalishuhudia mgombea kiti wa chama kinachoongoza kutangazwa mshindi. Hata ingawa kulikuwepo na vurumai za
upinzani kukataa ushindi huo, mwishowe walikubali kwani walitambua kuwa awakuwa na ushahidi wa kukataa ushindi huo. Kwa kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani, mgombeaji wa mrengo wa
upinzani alimtafuta mshindi na kumpongeza kisha akaomba msamaha na kuomba ushirika ili kuweka maendeleo endelevu katika jiji. Mshindi aliyekuwa amemmega mwenzake kwa kura zaidi ya milioni moja, alimakaribisha na kukubali kuwa kidole kimoja hakiwezi kuvunja chawa. Alimwomba kuwa karibu naye na kumshauri palipo na dosari ili kujenga nchi yenye amani na maendeleo ya kiwango cha juu.

Ama kweli uchaguzi huu ulikuwa ngoma na mfano mzuri wa siasa katika nchi yangu. Kubali kushindwa na shirikiana na wapinzani wako kujenga nchi badala ya ubaguzi, ukabila, uchoyo na ubinafsi wa matumbo yetu. Aidha tUwachague wazalendo wanaopenda maendeleo ya nchi yao badala ya
mahasidi wa kuwatenganisha jami.

Kujibu maswali kuhusiana na habari
Jibu maswali yafuatayo kutokana na makala uliyosoma

  1. Kwa mjibu wa makala haya, uchaguzi mkuu ulifanyika wakati gani?
  2. Ni kina nani waliokuwa wagombeaji katika upigaji kura hii?

3.Eleza utaratibu ambao mwananchi hutarajia kupitia kabla ya kupiga kura
4.Baada ya kupiga kura katika kituo chako, ni nini jingine hufanyika katika kituo hicho?
5.Baada ya kura kuhesabika, ni nani anayeruhusiwa kutangaza mshindi na mshindwa?
6.Ni nani anayesimamia uchaguzi mkuu katika nchi yetu?
7.Eleza baadhi ya methali zilizotumika katika makala haya.
8.Toa maoni kuhusiana na matokeo ya uchaguzi katika jamii yako

Stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo f: Sarufi – Kutambua viwakilishi Viashiria,vihisishi,
nomino za ngeli za i-zi zinazohusiana na uongozi na
kuzitumia katika sentensi
Utangulizi

Viwakilishi viashiria ni maneno yanayotumiwa kuonyesha mahali ilipo nomino kuzingatia ukaribu, umbali kidogo na umbali sana na msemaji kwa umoja na wingi. Je, unaweza kutambua viashiri hivyo? Ikiwa mtu yupo karibu nawe, mwingine yupo mbali kidogo na mwingine hayupo au yupo mbali sana unaelezaje umbali huo? Katika mada ndogo hii, utajifunza namna ya kutumia viashiria katika sentensi.

Kutunga sentensi kwa kutumia viwakilishi viashiria
Shughuli 5.9
T azama picha zifuatazo kisha utumie viashiria vilivyomo kudhihirisha maana ya kila kiashiria..

Baada ya kudhihirisha viashiria vya hapo juu katika vikundi, igizeni viashiria hivyo.

  1. Tunga sentensi tano ukitumia viwakilishi viashiria kwa umoja na wingi.
  2. Chunguza kwamakini viashiriavilivyomo katikajedwali lifuatalo na uvitumie kuashiria nomino nyingine za ngeli ya i-zi- zinazohusiana na uongozi.

Taz•. Ni muhimu kuelewa kuwa viashiria hutofautiana kutegemea ngeli za majina. Viashiria hivi ambavyo tumeangalia katika mada ndogo hii ni vya ngeli ya i-zi-. Ngeli nyingine Zina viashiria ambavyo ni tofauti na vya ngeli hii. Kwa mfano, ngeli ya a-wa, ina viashiria huyu, huyo na yule kwa umoja, na hawa, hao na wale kwa wingi.

Stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Vihisishi
Utangulizi

Unatembea njiani na kwa ghafia unamwona jirani yako anatereza kuanguka. Aidha upo na wenzako na kwa ghafla kitendo cha ajabu kinatendeka. Ni maneno yapimtakayotumia kuonyesha hisia za kushangaa, kushtuka, kuhuzunika, kufurahia na kadhalika? Maneno ambayo mmetaja ndio yanayoitwa vihisishi. Katika mada hii, utajifunza vihisihsi vya aina mbalimbali kuonyesha jinsi tunavyohisi katika maisha yetu.
Hebu jaribu kufanya kitu cha kushangaza kisha utasikia sauti kutoka darasani.

Kuorodhesha na kutumia vihisishi kutunga sentensi
Shughuli 5.10

Katika vikundi, jadiliana na kutambua vihisihi angalau vitatu ambavyo mara nyingi hutumia kuonyesha hisia zifuatazo:
a) Huzuni
b) Furaha
c) Kuudhika
d) Kukata tamaa
e) Kushangaa
f) Kuapa
g) Kusifu
h) Kiburi

  1. Wasilisheni matokeo ya mjadala wenu kwa kuigiza mbele ya darasa lenu.
  2. Tungeni sentensi kwa kutumia angalau kihisishi kimoja.
  3. Ni nini ambacho mmejifunza kuhusiana na matumizi ya vihisishi?
  4. Mnafikiri vihisishi vina umuhimu gani katika mazungumzo?
    Taz: Umetambua kuwa vihisishi ni maneno yanayotumika kuonyesha hisia za mzungumzaji au mtazamaji. Maneno haya hutumika hasa katika mshutuko, kushangilia, kusifia, furaha, huzuni, mshangao, kukubali

jambo, au hisia nyingineyo. Alama ya mshangao (!) au kihisishi hutumika kuonyesha hisia husika kulingana na muktadha. Hii ni maana kuwa kila jamii ina maneno yanaoyoonyesha hisia.
Stadi za lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo g: Kueleza vinyume vya vitenzi na kuvitumia
katika sentensi
Utangulizi

Kinyume ni hali inayokinzana au kupingana na nyingine. Je, umewahi kubishana na mwenzako katika shughuli zenu? Kwa mfano unataka kupanda mti na mwenzako aliye juu tayari anakwambia kusubiri ili ashuke au unataka kumeza chakula ambacho umekula na mwenzako anakwambia kukitema? Hali kama
hii ndio itakayoshughulikiwa katika mada ndogo hii. Katika mada hii utajifunza kanuni na utaratibu wa kutambua vinyume vya maneno na vitendo.

.Kuandika kinyume
1.Katika vikundi andika vinyume vya kawaida ambavyo mmekuwa mkitumia katika shughuli zenu za kila siku.
2.Katika vikundi
a) Andikeni kinyume cha vitendo vifuatavyo
i) Ficha
ii) Umba
iii) Fumba
iv) Tega
v) Lia
vi) Penda
vii) Panda
viii) Kaa
b) Andikeni kinyume cha vivumishi vifuatavyo
i) Zuri
ii) Refu
iii) Karimu
iv) Eusi
v) Chafu
vi) Pana

Taz: Katika mada hii, umejifunza kuwa maneno yanayotumika katika kinyumemni yenye maana inayopingana. Ni muhimu kutambua kuwa kuna tofautimmkubwa kati ya kinyume na kukanusha. Kukanusha ni kukataa ujumbewa sentensi bila kubadilisha maneno. Kwa hivyo ni muhimu kutambua
kukataa jambo au wazo Kukanusha) na maana kinzani (Kinyume).

Nomino za ngeli ya i-zi
Utangulizi
Katika Kiswahili, nomino huwa zinaainisha kulingana na upatanisho wake. Mwainisho huu husababisha kuwepo kwa ngeli za majina. Kwa hiyo kuna ngeli mbalimbali za nomino. Je, unajua ngeli zozote za majina? Unaweza kutaja ngapi? Katika mada hii utajifunza kuhusu nomino za ngeli ya i-zi zinazohusiana na uongozi.
Kutambua nomino za ngeli ya i-zi zinazohusiana
Shughuli 5.12
na uongozi

  1. Mkiwa katika vikundi, fanyeni utafiti katika kamusi, vitabu na mtandaommnomino za ngeli ya i-zi zinazohusiana na uongozi.
  2. Kila kikundi kiwasilishe matokeo yake mbele ya wanafunzi darasani.
  3. Baada ya kuwasilisha nomino, rudini katika vikundi vyenu na kutungam entensi sahihi mkitumia nomino zile zile.

Fasili simulizi
Stadi za lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo h: Kujadili jinsi uongozi unavyoendelezwa
kulingana na hadithi
Utangulizi

Kuna aina mbalimbali za uendelezaji wa uongozi katika jamii. Unaposikiliza habari au taarifa au kusoma hadithi mbalimbali, utatambua mengi kuhusiana na uongozi wa kifamilia, kijamii, kitaifa na kimataifa. Je, umewahi kusoma au kusikiliza hadithi na kutambua jinsi uongozi unavyoendelezwa katika jamii? Katika sehemu hii, utajifunza jinsi ya kusimulia hadithi juu ya jinsi uongozi unavyoendelezwa.

Hapo zamani katika kijiji cha Sijui, waliishi Bwana Gimono na Bi Natushaba. Familia hii ilikuwa imejaliwa na watoto watano. Wasichana watatu na wavulana wawili. Familia hii ilikuwa ikishiriki katika ukulima wa vyakula mbalimbali na ilikuwa nadra sana kuwapata popote ila mashambani kwao. Asubuhi moja, Bwana Gimono na familia yake walienda shambani kuvuna baadhi ya mazao yao ya ndizi. Kufika shambani walipata kuwa ndizi zote zilikuwa zimevunwa bila wao kujua.
Gimono aliishiwa na nguvu. Alisimama kilimani na kuanza kupiga nduru ili kupata msaada. Hata hivyo, ni majirani wake pekee waliokuja kumpa pole kwa msiba wa kuibiwa. Alipokuwa hapo, mkewe alimwonyesha magurudumu ya gari. Alitambua kuwa wezi waliowaibia walikuwa na gari lililobeba ndizi zao.

Bila kusita, Bwana Gimono alianza kufuata magurudumu haya akijua kuwa kufuata nyuki ni kula asali. Nitawapata. Hakuna mchezo. Nikiwapata kila mmoja atapata jeraha. Jasho langu ni langu. Uzembe na
wizi! Hapana! Hapana! Bwana Gimono alimaka. Alifuata magurudumu haya kwa kiapo huku akitokwa na machozi kwikwikwi. Alipofika barabara kuu, hakuweza kuona tena magurudumu.
Mkutano wa dharura uliandaliwa na malalamishi kutolewa mbele ya viongozi wote. Afisa wa polisi aliwapa utaratibu wa kusuluhisha matatizo yao. Aliwaomba kuwa kisa kama hicho kikitokea tena ni muhimu
kumwelezajirani wako, kwenda kwa wazee wa vijiji au mitaani na madiwani ili wawasaidie kusuluhisha matatizo katika ngazi zao katika uongozi. “Hapana. Itabidi mfahamu uongozi na kuzingatia siyo kujichukulia sheria mikononi.” Afisa aliwaonya.

“Kijana mwenyewe ameshikwa na sasa tunamtafuta mzee wa kijiji na mzee wa mtaa pamoja na diwani ili watusaidie kumtafuta mzazi wa mvulana huyo.Anasema kuwa pesa zake zote aliwaachia wazazi wake”.
Afisa aliripoti. Nani Huyo? Wananchi walitaka kujua hata hivyo afisa alijua kuwa hasira hasara na akisema huenda akasababisha vita vingine. kuamuru vijana. “Hapana Mwananchi. Sikiliza. Sisi tunafanya kazi na
polisi na leo hii tumelishika gari lililokuwa na ndizi usiku…. ‘tiko wapi?”
akiwakata kauli, “Subiri. Wote tumewakamata. Waliiba ndizi vijijini na hata wakaja hapa na kuiba ndizi sokoni.” Salaale! Kweli! Wallahi bilahi tallahi ningewapata! Mfanyibiashara mwingine alishangaa huku mwingine akila kiapo la kuwaangamiza.
“Subira yavuta heri, Nikimaliza mtaniuliza maswali. Sasa tunataka kujua mzee Gimono ni nani? Mzee Gimono kwa hasiri iliyokuwa inatulia aliitika, “Naam! Nipo. Wako wapi?” Subiri. “Kuna kijana ambaye
aliyauza mazao yako.” Afisa wa polisi aliendelea. Nani tumwangamize! Wananchi walihukumu.
Hapana! Haiwezekani. Hebu nipande mtini nitawaona. Bwana Gimono åliwaeleza waliokuwa wanamsindikiza. Aliutafuta mti mrefu na kuukwea. Hata hivyo hakuona chochote. Aliangulia patupu.
Alishindwa la kufanya. Alihuzunishwa sana na kitendo cha wezi. Kwa sababu Bwana Gimono ni mwingi wa hasira na asiyechoka kutafuta anachotafuta, alianza kukimbia kwa kasi na kujikuta sokoni huku
akifuatwa na majirani, mkewe na watoto wake waliokuwa wamebeba fimbo, mishale na mikuki ya kuwaangamiza maadui wao.

Wananchi waliandamana na Afisa hata hivyo walioibiwa peke yao ndio walioruhusiwa kwenda waliobaki walishauriwa kurudi makwao na kuwashirikisha viongozi wao katika kutatua matatizo yao. Walielimishwa
kufahamu viongozi wao na nyadhifa zao. Kuanzia siku hiyo Bwana Gimono na wananchi wote walijifunza kuripoti wezi na kukabiliana na wezi bila matumizi ya nguvu zake. Wananchi walimshukuru afisa kwa ushauri na kuwaokoa katika kupunguza hasira za Gimono aliyejulikana kuwa hatari na asiye kuwa na subira. Sasa kijiji kizima kinaishi kwa amani na utulivu, maendeleo na ushirika mkuu na viongozi. Wanafanya maombi kizalendo na kuwajibika, kujali na kuthaminiana. Wananchi ni wazingativu wa sheria
na washiriki wakuu katika uongozi na utatuzi wa matatizo ya nchi yao.

1.Katika vikundi tafuteni maneno magumu katika kamusi au mtandaoni na kueleza maana ya kila neno.

3.Katika vikundi vyenu, simuliana hadithi kuhusu uongozi na baadaye mchague mtu mmoja mwenye hadithi nzuri aisimulie wanafunzi wote kwa zamu.

Stadi za lugha: Kusoma na Kuandika
Funzo j: Kufupisha makala kwa maneno yaliyoigizwa
Kuandika Ufupisho
Utangulizi

Ufupisho ni muhtasari wa habari au taarifa. Mara nyingi huwa unawaona wasomaji habari wanapoanza habari zao wanaanza kwa kusema, ifuatayo ni taarifa ya habari na kwanza ni muhtasari wake, kisha anatoa vidokezi vya habari

nzima ambayo ataisoma kwa muda wa dakika ishirini na tano au thelathini. Je, umewahi kuwasikia wasomaji habari wakitoa muhtasari wa habari? Katika mada ndogo hii, utajifunza jinsi ya kufupisha taarifa unazopewa.

2.Kufupisha habariShughuli 5.15
Katika vikundi, someni kwa makini kifungu cha habari kifuatacho na
kukielewa vizuri.
Uganda ni Nchi yangu. Nchi hii inapatikana katika Afrika ya Mashariki barani Afrika. Nchi hii inapakana na Kenya, Rwanda, Sudani, Kongo, Burudi na Tanzania. Ninaipenda nchi hii kwa sababu ya mambo mengi. Kuna jua la kutosha, udongo wenye rutuba, misitu ya kijani inayopendeza na kuvutia mvua ya kutosha,
wanyama pori wengi, wananchi wakarimu na wenye bidii. Kufika Uganda, utatambua kuwa Uganda imejaa makabila ya watu wengi; si Wakiga, si Wanyankole, si Watooro. Wakonzo, Wabwisi, Wasamia,
Wagisu, Wasabiny, Wapokoti, Wakaramoja, Wateso, Acholi, Langi, Alur, Lugbara, Kagwa, Wanyoro, Waganda, Wasoga, Japadhola, Wagwere, Wanyarwanda, Warundi, na makabila mengineyo mengi
ambayo ni zaidi ya makabilia 40. kula sana chakula kutegemea mazingira tunamotoka. Kwa mfano utatambua kuwa chakula kinacholiwa Mashariki ni tofauti na chakula kinacholiwa Kati ya Uganda
na kaskazini Kasikazi pamoja na Magharibi au Kusini ya Magharibi. Mbali na makabila haya, tuna Wahindi wa Uganda. Kwa hiyo ni furaha kuwa tuna wazungu wahindi na wahindi ambao ni wananchi wa Uganda.
Wananchi wa Uganda ni wananchi ambao wengi wanapenda kukaa mjini. Hata hivyo asilimia kubwa ya watu kutoka Magharibi, Mashariki na Kaskazini wanapenda kuishi katika miji ya maeneo yao na hata
kufanya kazi ya ukulima. Tuna nafasi kubwa sana ya kibiashara na mgeni yeyote anayeingia hukaribishwa na kuingizwa katika msururu wa familia ya Wana Uganda.
Maswli
1.Elezeni kwa sentensi moja kichwa kuhusu habari hiyo.
2.Je, ni hatua gani iliyowaongoza kutambua anwani moja inayotoa muhtasari wa hadithi nzima?
3.Kwa kutumia hatua mlizotumia fupisha kifungu hicho kwa maneno 80.

Taz: Baada ya kufupisha umetambua kuwa, ufupisho ni kuandika muhtasari wa habari iliyosomwa kwa kutumia maneno machache kwa kudondoa tu habari au ujumbe muhimu bila kujirudia. Wakati wa ufupishaji, unafaa

kusoma na kuhakikisha kuwa hakuna ujumbe muhimu ulioachwa nje na kuhesabu idadi ya maneno na kuyaweka kulia kwa mkono wako na mwiShO kutoa muhtasari wa kichwa kimoja kinachofupisha habari nzima.

Muhtasari wa mada
Katika mada hii, umejifunza juu ya:

Msamiati wa uongozi na ala za uongozi
Nyadhfa za viongozi mbalimbali
Dhima na nembo za kitaifa
Shughuli mbalimbali katika kampeni.
Kusoma makala kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu na kujibu maswali
Viwakilishi viashiria, vihisishi, nomino za ngeli ya i-zi zinazohusiana
na uongozi na azitumie katika sentensi
Vinyume vya vitenzi na kuvitumia katika sentensi
Jinsi uongozi unavyoendelezwa kulingana na hadithi fupi
Hatua mwafaka za ufupishaji wa makala
Kufupisha makala kwa maneno uliyoagizwa

Assignment

Mfano wa Shughuli Jumlishi juu Uongozi wa Kitaifa

ASSIGNMENT : Mfano wa Shughuli Jumlishi juu Uongozi wa Kitaifa MARKS : 10  DURATION : 1 week, 3 days

 

Courses

Featured Downloads