To provide the best experiences, we use technologies like cookies to store and/or access device information. Consenting to these technologies will allow us to process data such as browsing behavior or unique IDs on this site. Not consenting or withdrawing consent, may adversely affect certain features and functions.
The technical storage or access is strictly necessary for the legitimate purpose of enabling the use of a specific service explicitly requested by the subscriber or user, or for the sole purpose of carrying out the transmission of a communication over an electronic communications network.
The technical storage or access is necessary for the legitimate purpose of storing preferences that are not requested by the subscriber or user.
The technical storage or access that is used exclusively for statistical purposes.
The technical storage or access that is used exclusively for anonymous statistical purposes. Without a subpoena, voluntary compliance on the part of your Internet Service Provider, or additional records from a third party, information stored or retrieved for this purpose alone cannot usually be used to identify you.
The technical storage or access is required to create user profiles to send advertising, or to track the user on a website or across several websites for similar marketing purposes.
Afya na Usafi
Utangulizi
Usafi ni suala muhimu katika kutunza afya njema kwa binadamu. Je! Unafikiri kwa nini ni muhimu kutunza usafi? Mada hii itakuwezesha kutambua jinsi ya kuendeleza usafi wa rnwili na wa mazingira yako, na jinsi ya kuepukana na magonjwa yanayotokana na uchafu.
Funzo a :Msamiati wa usafi
Stadi: Kusikiliza na Kuzungumza
Shughuli 2.1: Kutambua msamiati wa usafi
Katika makundi,
Je! Ni uungwana? Ikiwa si uungwana, kwa nini unafikiri hivyo?
(i)Kusukutua maji mdomoni na kuyatema nje kupitia dirishani!
(ii) Kula chakula huku ukiongea!
(iii) Vijana sita kupiga mswaki kwa kutumia mswaki mmoja!
(iv) Kuvaa mavazi yaliyopigwa pasi!
(vi)Kuenda msalani bila karatasi laini ya choo au maji!
(vi) Kula chakula kabla ya kunawa mikono!
(vii) Kuumauma kucha za vidole!
(viii) Kukuza na kutochana nywele!
(ix) Kufarishi kitanda chako kila asubuhi!
(x) Kukohoa bila kufunika mdomo na kutema sakafuni darasani!
(xi) Kutumia choo na baadaye kutoka bila kufoka maji!
(xii) Kuingiza mkono na kujikunakuna katika sehemu zako za
siri mbele ya watu!
(xiii) Kujamba kati ya wenzako darasani!
(xiv) Kuchokora pua yako kwa kidole kila mara!
(w) Kupiga chafya bila kufunika mdomo kwa kitambaa au bila
kuvaa barakoa.
Vifaa vya usafi
Stadi: Kusikiliza na Kuzungumza
Shughuli 2.2: Kutambua na kueleza vifaa vya usafi.
Katika makundi,
1 (a) Tazameni na kutaja mnachoona au mnachojua kuhusu michoro ifuatayo;
(b) Kwa kurejelea michoro mliyojadili katika (Ia) hapo juu,someni, jadiliana na kuhusisha baadhi ya sentensi zifuatazona michoro hiyo;
1.Hii ni sabuni, sifongo na beseni ya kubebea maji. Ninatumia sabuni, sifongo na maji kuoga mwili.
2 Ninatumia wembe kama huu kukata kucha.
3 Hii ni taulo. Ninatumia taulo kujipangusa maji mwilini baada ya kuoga.
4 Huu ni mswaki na dawa ya meno. Ninatumia mswaki na dawa ya meno kupiga mswaki.
5 Kifaa cha kusafishia masikio. Ninasafisha masikio kwa kutoa nta. Nta huonekana kama grisi ayotengenezwa sikioni.
6 Hiki ni kitana. Pia huitwa kichana. Ninatumia kitana kuchana nywele.
7 Kinyozi anatumia mashine kama hii kunyoa nywele au
ndevu za wateja wake.
8 Hii ni sodo. Inatumika sana na wasichana au wanawake
9.Hii ni hanchifu. Ninatumia hanchifu kujipangusa jasho au
kusafisha pua.
10 Sabuni ya unga au ya maji inayotumika kusafishia vitu
au sehemu mbalimbali.
11Karatasi laini ya chooni. Ninatumia karatasi ya Choo
kujisafisha baada ya kwenda haja.
12 Hili ni kwanja. Tunatumia kwanja kufyeka nyasi.
13 Huu ni ufagio. Ninatumia ufagio kufagia.
Funzo ch: Msamiati wa afya
Shughuli 2.3: Kutambua msamiati wa afya. Katika makundi,
2.
Someni na kuhusisha baadhi ya sentensi zifuatazo na michoro mliyojadili hapo juu.
(i) Hii ni machela. Machela ni kitanda cha kubebea wagonjwa wasioweza kutembea.
(ii) Huyu ni daktari. Kazi yake daktari ni kupima na kutibu wagonjwa.
(iii)Hizi ni tembe. Tembe ni dawa tunazopewa na daktari tukiwa wagonjwa ili tuzimeze.
(iv) Huyu ni mgonjwa. Amelazwa hospitalini. Ugonjwa ni hali ya mtu kukosa kuwa na afya.
(v)Hii ni zahanati. Zahanati pia huitwa dispensari. Ni mahali
ambapo magonjwa yasiyokuwa makubwa hutibika.
(vi)Mvulana huyu ananyunyiza dawa. Anapiga dawa chumbani
kuua wadudu.
zifuatazo kwa kutumia msamiati sahihi.
(i) ……………………………………………………..husaidia akina mama wajawazito kujifungua.
Anayesaidia daktari kutibu wagonjwa huitwa………………………………………….
Kifaa kinachotumiwa kutilia dawa ili kudunga mtu huitwa
Sehemu ya mwili yenye jeraha huitwa………………………………………………………………………..
Wadudu hatari wanaosababisha magonjwa
Stadi: Kusoma na Kuandika
Shughuli 2.4: Kutambua wadudu hatari wanaosababisha
magonjwa mbalimbali na namna ya kujikinga na magonjwa hayo.
Katika makundi,
katika michoro.
Shirikiana katika kusoma na kujadiliana kuhusu maelezo yafuatayo. Husisheni wadudu katika michoro mliyojadili hapo juu na maelezo yafuatayo.
Mbu
Mbu ni mdudu hatari sana. Mbu husababisha ugonjwa wa malaria. Mbu hutaga mayai katika maji tuama, sehemu zenye giza, madimbwi ya maji, mifereji na mitaro ya maji tuama, vichakani, chupa zilizotupwa ovyo, vigae vya nyungu n.k Jadiliana kuhusu njia za kuepukana na ugonjwa wa malaria.
Nzi
Nzi ni mdudu hatari. Nzi ni wadudu wachafu ambao wanapendakukaa katika mazingira kuchafu sana. Nzi wanapenda kutuakwenye chakula cha binadamu kukifyonza. Wakitua juu yachakula hicho, huwa wamebeba uchafu. Nzi wanasababisha ugonjwa wa kuendesha kwa binadamu. Ugonjwa wa kuendesha
pia hujulikana kama kuhara. Uchafu unaobebwa na nzi kwenye vyakula vyetu husababisha ugonjwa wa kipindupindu. Ugonjwa wa kipindupindu una ishara ya kutapika na kuhara sana. jadiliana kuhusu njia za kuepukana na ugonjwa wa kipindupindu.
Mende
Mende pia hujulikana kama kombamwiko. Mende hupenda kula karatasi, nguo na uchafu. Mende hupenda kuishi katika mashimoya paipu, sinki, majokofu, makabati, katika nyufa za kuta, maboksini
au majalalani. Mende pia wanabeba vijidudu vinavyosababishahoma ya matumbo. Ugonjwa huu ni wa kuharisha damu. Homa ya matumbo hutokana na kula vyakula au kunywa maji yenye
uambukizo wa bakteria hatari wanaoshambulia matumbo. Jadiliana kuhusu njia za kuepukana na ugonjwa wowote unaoweza kuletwa na mende.
Kiroboto
Viroboto hupenda kujificha katika nyufa za kuta, chini ya mikeka,matambara au mazulia. Pia hupenda kukaa katika manyoa ya wanyama. Viroboto huweza kusababisha ugonjwa wa tauni. Ugonjwa wa tauni humfanya mtu kuwa na homa kali baada ya kuumwa na viroboto wa panya wenye ugonjwa. Jadiliana kuhusu njia za kuepukana na ugonjwa wa tauni.
Kunguni
Kunguni ni mdudu hatari anayependa kufyonza damu ya watu. Hupenda kujificha katika mianya ya vitanda na magodoro au mablanketi. Kunguni husababisha uvimbe wa mwili. Jadiliana kuhusu njia za kuepukana na kunguni nyumbani kwetu.
Mbung’o
Mbung’o ni mdudu wa jamii ya nzi anayeuma na kufyonza damu ya wanyama na binadamu na kusababisha ugonjwa wa malale. Malale ni ugonjwa wa kusinzia. Jadiliana kuhusu njia za kuepukana na ugonjwa wa malate.
Funzo e Ufahamu: Afya na usafi
Shughuli 2.5: Kusoma makala na kujibu maswali.
Katika makundi,
huu.
2.
Shirikiana katika kusoma na kujadiliana kuhusu taarifa iliyomo
katika makala ifuatayo.
Nyumbani kwa Kadingo ni kuchafu sana! Hawafagii nyumba yao waia ua wao.
Chumbani mwake Kadingo mmejaa viroboto na kunguni. Wanamwuma na kufyonza damu yake kila siku. Hata katika mararuraru yake, unaweza kupata milioni ya chawa na viroboto. idole vya miguu yake vimevimba, anatembea kwa taabu! Ana funza katika miguu yake.
Kadingo anapenda kula kiporo kila siku nyumbani kwao. Siku moja asubuhi alipoamka, alipakua mlima wa chakula kwenye sahani yake. Alikuwa hata hajapiga mswaki wala kunawa usoni. Alikiweka chakula arazani ya nyumba. Kabla hajaanza kula, alijihisi angejisaidia msalani kwanza ili ajihisi tumbo tupu ndipoafyeke vizuri huo mlima wa chakula.
Alipotoka kwenda msalani, hakufunika kiporo chake. Alikiacha wazi tu pale barazani. Kwa hivyo, nzi walianza kuangushana mieleka na kubingirishana pale kwenye chakula hicho. Jambo la kushangaza Pia, hakuenda na karatasi laini ya choo wala maji yoyote! Alipomaliza kujisaidia baada ya muda wa dakika tatu hivi, alirudi akichokora pua yake kwa kidole cha shahada cha mkono wa kulia. Baadaye, alijipangusa vidole kwenye kaptura yake bila kunawa mikono wala kuomba na kuanza kula chakula.
Kadingo alikuwa amesahau kufunika shimo la choo kwa kifuniko kilichokuwa mle ndani. Kwa hivyo, nzi walianza kutoka chooni mle, mmoja baada ya mwingine mpaka wakawa bumba wakiruka juu ya chakula chake. Aliendelea kupiga mlo wake huku mkono wa kushoto ukifukuzana na nzi wale watundu.
Kadingo alipomaliza kula chakula chake, alibaki amekaa pale barazani kwa uchovu. Aliendelea kuramba vidole vyake mpaka vilipoonekana safi kabisa. Hakuona haja ya kutafuta maji na sabuni kunawa mikono tena. Baada ya muda wa saa mbili hivi, Kadingo alisikika akilia “ayiii…ayiii…!” huku akiwa ameshikilia
tumbo lake.
Alihisi anataka kutapika na kwenda chooni kila wakati. Angeenda chooni kama sasa, akiwa anarudi kutoka chooni baada ya kujisaidia, ungemwona anakimbia anarudi chooni tena! Baadaye,
alileta kigoda na kuamua kukaa karibu na choo kwa sababu alikuwa amechoka kutimua mbio za kwenda na kurudi kujisaidia mara kwa mara! Mama yake alimpeleka hospitalini. Daktari alipopima, aligundua
kuwa Kadingo alikuwa na ugonjwa wa kipindupindu.
Hebu tuzungumze
Kwa kurejelea mchoro mliotazama katika (1) hapo juu, ni ugonjwa gani mbali na kipindupindu, ambao Kadingo na familia yake wanaweza kuugua. Eleza sababu zaidi ya mbili.
(i) Kadingo alifaa kufanya nini kabla ya kula chakula?
(ii) Nzi walifanya nini kwenye chakula cha Kadingo?
(iii) Taja wadudu wanaopatikana katika nguo za Kadingo.
(iv) Baada ya kujisaidia, Kadingo alifanya nini ambacho si cha Uungwana?
(v) Ni mdudu gani anayesababisha ugonjwa wa kipindupindu?
(vi) Ni nani alipeleka Kadingo hospitalini?
(vii) Eleza kwa nini Kadingo aliamua kukaa karibu na choo.
(viii) Taja mambo muhimu matatu ambayo Kadingo angefaa kufanya ili aepukane na ugonjwa wa kipindupindu.
Sarufi N gel i y a Ya
zingatia Hii ni ngeli ya vitu visivyoweza kuhesabika. Ngeli hii ina nomino za wingi tu. Nomino za ngeli hii, mara nyingi huanza kwa Ma- Majina ya ngeli hii yanatumia kiambishi yal – cha upatanisho wa kisarufi katika sentensi
Stadi: Kusoma na Kuandika
Shughuli 2.6: Kutunga sentensi kwa kutumia nomino za ngeli ya
Katika makundi,
I. Tazameni na kujadiliana kuhusu kinachotendeka katika mchoro
ufuatao.
.
(ii) Upatanisho wa kisarufi kwa matumizi ya vionyeshi na vivumishi
na
katika umoja na wingi kutokana na majedwali mliyojadili katika
(2) hapo juu.
(i) Mazingira yako hayo yanatisha.
(ii) Marashi yake ya kila siku yamezidi.
(iii) Maji yangu haya si baridi sana.
(iv) Maziwa hayo ni meupe pepepe!
Mnyambuliko wa vitenzi
Stadi: Kusikiliza na Kuzungumza
Shughuli 2.7: Kutambua mnyambuliko wa vitenzi katika kauli ya
kutendwa, kutendeana na kutendana.
Katika makundi,
zifuatazo.
(a)Kabogoza anasoma kitabu cha hadithi fupi.
(b)Kitabu cha hadithi fupi kinasomwa na Kabogoza.
(c)Kabogoza na Ojega wanasomeana kitabu Cha hadithi fupi.
(d)Ojega anasomewa kitabu cha hadithi fupi na Kabagoza.
(e)Kabogoza na Ojega wanaongozana katika kusoma kitabu cha hadithi fupi.
3.
Shirikiana katika kutunga sentensi tano zenye vitenzi vilivyonyambuliwa katika kauli zifuatazo.
(i) tendewa
(ii) tendeana
(iii) tendana
(i)Aboga na Balekye wanapika chakula. (tendeana)
(ii)Nsaze alifanya kazi jana. (tendwa)
(iii)Masereka anaosha vyombo vya Mariam (tendeana)
(iv)Kanyina ataosha miguu ya Otoa. (tendana)
(v)Akampa ataletea wanafunzi keki darasani. (tendewa)
(vi)Mwendawazimu anarusha mawe kwa mwendawazimu mwenzake. (tendeana)
(vii)Mtoto anafundisha mtoto mwenzake namna ya kutumia
choo vizuri. (tendana)
viii) Ng’ombe huyu anaramba ng’ombe mwenzake. (tendana .
Funzo h: Vielezi mbalimbali
Stadi: Kusoma na Kuandika
Shughuli 2.8: Kubainisha vielezi vya namna na vya idadi na
kuvitumia katika sentensi.
Katika makundi,
1.
Shirikiana katika kusoma na kujadiliana kuhusu maana ya
sentensi zifuatazo kwa kusisitiza maneno yaliyokolezwa.
(i) Ugonjwa wa virusi vya korona unaambukiza haraka sana.
(ii)Baiskeli yake iliharibika vibaya.
(iii)Mambo yao siku hizi ni ya kisirisiri.
Ajuna anatembea kwa maringo.
0 Pia, kuna baadhi ya vielezi vya namna ambavyo huelezea
kitendo kwa kusisitizia namna kinavyotendeka. Hapa vielezi
husika hurudiwa mara mbili mfululizo. Kwa mfano;
(i)Wanafunzi hawa wanaelewa haraka haraka.
(ii)Kobe yule anatembea pole pole.
(iii)Katooma hakulipwa kwa kufanya kazi ovyo ovyo!
(iv)Maskauti walikimbia mbio mbio mpaka mjini.
Kuna baadhi ya vielezi vya namna Pia, ambavyo huelezea
hali au namna kitendo kinavyotendeka. Hivi hutoa dhana ya
ulinganishaji wa hali, tabia au kiwango fulani kwa kutumia
Kil ya mfanano. Kwa mfano;
(i)Emulgat anavaa kiofisa kila siku.
(ii)Mbona huyu Kapere anapenda kucheka kijinga?
Opolot anazungumza kiungwana.
(iv)Katima analala kifalme kitandani mwake kila usiku
(a) Sisi tunasoma lugha ya Kiswahili mara mbili kwa Wiki.
(b) Mgonjwa huyu aliambiwa ameze dawa yake mara tatu kwa siku.
(ch) Ng’ombe wangu anakamuliwa maziwa mara moja tu kwa siku.
(d) Tunaenda uwanjani kucheza mpira mara mbili kila Wiki.
Funzo i: Tanakali za sauti
Tanakali za sauti ni vielezi pia ambavyo huelezea kitendo kwa kusisitiza namna kinavyotendeka au
kilivyotendeka. Hivi huigiza sauti au miio wa kitu, hali au jinsi kinavyotendeka.
Stadi: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika Shughuli 2.9: Kuigiza tanakali za sauti.
Katika makundi,
1.
Someni na kuigiza tanakali za sauti zifuatazo.
1. Mti umeanguka chini pu!
2 Kengele iligonga ngo’ngo’ngo’!
3 Embe lilitumbukia majini chubwi!
4 Akrabu za saa zilienda tik tok tik tok!
5 Mwizi alitulia tulii baada ya chifu kumzaba kofi shavuni pya!
6 Wanafunzi wote wamenyamaza jii!
7 Mali yote imezama zii!
8 Bandimba hulewa chakari kila siku.
9 Mama aliteleza prrr na kuanguka chini pu!
10 Nje kuna giza totoro!
11 Mtoto amelala fofofo!
12 Kaliisa amecheka kwe kwe kwe walipomtikinya!
13 Mwalimu amekataa katakata kusamehe wanaopiga kelele
darasani!
14 Maskauti wanafanya kazi chapuchapu!
Alipojikwaa kido e, a I I kwi kwi kwi!
zinazofaa.
(i) Jiwe lilianguka mtoni
(ii)Alipofika nyumbani, alikuwa amelewa
(iii)Akicheka, meno yake hunipendeza, ni meupe
(iv)Asina amepoteza pesa zake. Amelia
asubuhi
(v)Nakaliika alitupa funguo zikaanguka mchangani
(vi)Maji yalichururika mtungini
tangu
Kuandika Insha
‘ Stadi: Kuandika
Shughuli 2.10: Kuandika insha
Katika makundi, andikeni insha isiyopungua maneno 150 na isiyozidi maneno 250 kuhusu namna unavyoweza kujikinga dhidi ya ugonjwa wowote unaosababishwa na mdudu yeyote. Zingatia yafuatayo; Mdudu hatari, Mdudu anapenda kukaa wapi? Anasababisha ugonjwa gani? Mdudu huyo anaenezaje ugonjwa huo? Ni ishara gani za ugonjwa huo? Ni njia gani zinazoweza kupitiwa kujiepusha ugonjwa huo? Mtu anafaa kufanya nini baada ya kupata ugonjwa huo? n.k.
Mfano wa Shughuli jumlishi: Usafi ni suala la msingi katika tahadhari ya magonjwa mbalimbali
katika maisha ya binadamu. Kwa hivyo, usafi ni suala muhimu katika uendelezaji wa afya njema katika jamii. Andika hotuba utakayowasomea wanafunzi wenzako shuleni ili wapate kudumisha usafi. Unafaa kuzungumzia vitendo ambavyo vinaendeleza usafi pamoja na vifaa mbalimbali vya usafi.
Muhtasari wa mafunzo ya mada
Katika mada hii, umejifunza,
Kutambua msamiati wa usafi.
Kutambua vifaa vya usafi na matumizi yake.
Kutaja msamiati wa afya.
Kutambua wadudu hatari wanaosababisha magonjwa na namna
ya kujikinga na magonjwa hayo.
Kusoma insha na kujibu maswali kuhusu afya na usafi.
Kutunga sentensi kwa kutumia upatanisho wa kisarufi wa ngeli
ya ya-ya.
Kutambua mnyambuliko wa vitenzi katika kauli ya kutendewa,
kutendeana na kutendana.
Kubaini vielezi vya namna na idadi halafu na namna ya
kuvitumia katika sentensi.
Kutambua na kuigiza tanakali za sauti.
Kuandika insha kuhusu namna ya kujikinga na magonjwa
mbalimbali yanayosababishwa na baadhi ya wadudu.
Assignment
ASSIGNMENT : Kuandika Insha:Afya na Usafi MARKS : 10 DURATION : 1 week, 3 days