• LOGIN
  • No products in the cart.

DAYOLOJIA/MAZUNGUMZO (Dialogue/conversation)

Dayolojia ni mazungumzo kati ya watu wawili ama zaidi kuhusu jambo Fulani. Dayolojia huwa na mada/kichwa. (A dialogue is a conversation between two or more people about something. It should be with a heading)

Kwa mfano:

MAZUNGUMZO KATI YA BABU NA MJUKUU WAKE

(The dialogue between a G.father and his G.child)

 

Mjukuu:      Shikamoo babu?

Babu:          Marahaba mjukuu wangu. U hali gani?

Mjukuu:      Ni mzima babu.

Babu:          Habari za utokeako?

Mjukuu:      Ni njema babu. Unaonekana una haraka sana. Unaelekea wapi?

Babu:            Ninaenda kwa mheshimiwa Polibo Baraka. Nimejulishwa  kwamba aliaga      dunia jana usiku.

 

Mjukuu: Maskini! Hayati Polibo Baraka ameipa dunia kisoga! Alikuwa                     Mgonjwa?

Babu: Ndiyo. Alikuwa kaugua ugonjwa wa saratani kwa muda Mrefu.Tumepoteza kiongozi shupavu.

Mjukuu:     Kweli babu nakuunga mkono. Mheshimiwa Polibo Baraka alileta maendeleo katika eneo letu hili. Sijui kama tutampata mwingine kiongozi kama huyu. Makiwa.

 

Babu:    Yamepita. Mungu atatujalia. Ni vizuri kufanya mema ukiwa hai. Utakumbukwa hata ukiaga dunia. Hebu nijiunge na wenzangu katika matanga. Kwa heri mjukuu wangu.

 

Mjukuu:  Kwa heri ya kuonana babu.

 

Msamiati katika mazungumzo haya. (Vocabulary in this dialogue)

Aga dunia: kufa (To die)

Hayati: marehemu (The late)

Ameipa dunia kisogo: kutoka katika dunia. (Say bye to the world)

Kaugua: kuwa na ugonjwa. (Got sickness)

Ugonjwa: Sickness/illness

Saratani: Cancer

Tumepoteza kiongozi shupavu: We have lost a strong leader

Nakuunga mkono: kubaliana na mtu (agree with someboday)

Mungu atatujalia: God will take care of us.

Hai: Alive

Hebu nijiunge na wenzangu: Let me join my friends.

Katika matanga: In the funeral

Maswali

  1. Babu alikuwa anaenda wapi?
  2. Ni nini maana ya kuipa dunia kisogo
  3. Kwa nini mheshimiwa Polibo Baraka aliitwa marehemu?
  4. Mheshimiwa polipo alikuwa na akifanya kazi gani?
  5. Neno matanga lina maana gani?
  6. Taja neno jiingine la hayati
  7. Taja maneno matatu ya heshima yaliyotumiwa katika mazungumzo haya.
  8. Kwa nini mheshimiwa Polibo Baraka aliitwa shupavu?

 

MAZUNGUMZO SHULENI

Mwanafunzi:             Hodi! Hodi!

Mwalimu mkuu:        Karibu Nobert Asingya

Mwanafunzi:                         Asante mwalimu mkuuu. Shikamoo mwalimu mkuu?

Mwalismu mkuu:      Marahaba. Nyumbani hawajambo?

Mwanafunzi:             Hawajambo mwalimu. Ila baba yangu ni mgonjwa. Nimekuja                                              kukuomba ruhusa ya kuniridhia kusoma kwa sababu sina usaidizi                                        wowote.

Mwalimu mkuu:        Pole sana. Mungu amjalie, apate nafuu. Nitakuruhusu usome hadi                                        atakapo pata nafuu.

Mwanafunzi:             Asante sana mwalimu mkuu.

Mwalimu mkuu:        Unasoma kidato kipi?

Mwanafunzi:             Mimi ninasoma kidato cha tano.

Mwalimu mkuu:        Unafanya masomo yapi?

Mwanafunzi:             Ninafanya Kemia, Hisabati na Biolojia.

Mwalimu mkuu:        Umekuwa ukitendaje darasani?

Mwanafunzi:             Nimekuwa nikitenda vizuri. Nina ndoto ya kuwa Daktari.

Mwalimu mkuu:        Weka bidii katika masomo. Mfuata nyuki hula asali. Utafanikiwa                                        ukisoma kwa bidii. Kumbuka kuomba mungu kila siku.

Mwanafunzi:             Asante sana mwalimu mkuu. Mungu akubariki. Kwa kheri.

Mwalimu mkuu:        Kwa kheri ya kuonana.

Maswali

  1. Mazungumzo haya yalitokea wapi?
  2. Mazungumzo haya yalitokea kati ya akina nani?
  3. Kwa nini mwanafunzi alienda kwa mwalimu mkuu?
  4. Mwanafunzi anasoma kidato kipi?
  5. Mwanafunzi anafanya masomo yapi?
  6. Mwanafunzi anafanya masomo mangapi?
  7. Eleza ndoto ya mwanafunzi
  8. Mwalimu mkuu alimwambia mwanafunzi kufanya nini ili afanikiwe ndoto yake?
  9. Eleza maneno ya hekima katika dayolojia hii.
  10. Eleza sifa za mwalimu mkuu.

 

                                                                                                   

DAYOLOJIA MAHAKAMANI

(Dialogue in court)

Hakimu:         Bwana Misitika Kakembo, kwa nini umeletwa mahakamani?

Mshitakiwa:   Mheshimiwa hakimu, ninatuhumiwa kuwa niliiba gari.

Hakimu:         Bwana Misitika Kakembo, unashitakiwa kuwa tarehe 12/06/2016,                           ulipatwa ukiiba gari la waziri wa afya. Ni haki ama ni uongo?

 

Mshitakiwa:   Mheshimiwa hakimu, huo ni uongo. Mimi sijawahi iba hata kalamu             Shuleni maishani mwangu.

 

Hakimu:         Ushuhuda nilionao hapa unaonyesha kwamba wewe na rafiki yako                          mlienda Katika wizara ya afya mkaiba gari la waziri. Mlikuwa na                              bunduki aina ya AK47.Rafiki yako alikimbia na bunduki bada ya                            kufukuzwa na walinzi wa afya.Sema ukwali ili usamehewe.

 

Mshitakiwa:   Kwa kusema ukweli, tarehe 12/06/16 nilidanganywa na rafiki yangu                       Aitwaye Chamba M.W.Z. kwamba tuende tukaibe gari la waziri                              ili tupate pesa. Kwa hivyo ninaomba msamaha.

 

Hakimu:         Nitakusamehe lakini nitakupa adhabu. Nitakufunga kwa miaka miwili                     na fimbo ishirini kila siku.

 

Mshitakiwa:   Eh! Mungu wangu! Mheshimiwa hakimu naomba upunguze adhabu                        yangu. Sitarudi tena hakimu.

 

Hakimu:        Sawa napunguza adhabu yako. Utakuwa ukipalilia maua katika bustani        ya Mahakama hii kwa miaka miwili. Pia utapewa fimbo tano kila siku. Usipotekeleza haya utafungwa milele.

Maswali

  1. Dayolojia hii ilitokea wapi?
  2. Eleza wahusika katika dayolojia hii.
  3. Mshitakiwa anaoitwa nani?
  4. Kwa nini mstakiwa aliletwa mahakamani?
  5. Fafanunua ushuhuda kuhusu mshitakiwa
  6. Andika tarehe 12/04/2016 katika maneno.
  7. Kwa nini mshitakiwa alikubalili kuwa alihusika katika kitendo cha wizi?
  8. Mshitakiwa na rafiki yake walitumia nini walipoiba gari la waziri?
  9. Eleza adhabu ambayo ilipiwa mshitakiwa.
  10. Eleza kwa nini wezi walioiba gari la waziri.
  11. Ungekuwa wewe, ungemhukumu vipi huyu mwizi?
  12. Eleza sifa za hakimu.

Misamiati                                            msamaha (forgiveness)     uongo (false)

Hakimu (A judge)                                samehe (forgive)               haki (truth)

Mshitakiwa (The accused)                   adhabu (punishment)        Uamuzi (judgement)

Mahakamani (in court)                         adhibu (punish)                 punguza (reduce)

Mahakama (court)                                nitakufunga (I will jail you)

Wizara ya afya (Ministry of health)     bustani (compound)            wizi (Theft)

Waziri (minister)                                  palilia (weed)                    tuhumiwa (suspected)

Wizara (ministry)                                 maua (flowers)                 iba (steal)

Wahusika (characters)                          ushuhuda (witness)          sifa (characters)

 

 

MAZUNGUMZO DUKANI

Mteja:             Hodi hodi?

Muuza duka: Karibu. Habari ya asubuhi?

Mteja:             Ni nzuri. Ninataka Sidiria moja, chupi moja na kilo tatu za sukari.Unauza                            shiligi ngapi?

Muuza duka: Sidiria ni shilingi elfu nne, chupi ni elfu tano, kilo ya sukari ni elfu mbili.

Mteja:             Oh! Bei yako ni nzuri sana. Wengine wanauza bei ya juu. Nitakuwa nikinunua                   bidhaa zangu hapa.

Muuza duka: Karibu. Unaishi wapi?

Mteja: Mimi ninaishi Madongoporomoka.

Muuza duka: Unafanya kazi wapi?

Mteja: Mimi ni mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Naalya.

Muuza duka: Haaaaa! Hapa karibu, watoto wangu wanasomea kwa shule yako.

Mteja:             Wanaitwa nani?

Muuza duka: Watoto wangu wanaitwa Mapaja, Makalio na Kaswera. Wanasoma kidato                     cha nne.

Mteja:  Nawajua watoto wako. Shika pesa zako. Kwa kheri.

Muuza duka:             Asante sana, Rudi tena.

Maswali.

  • Dayolojia hii ilitokea wapi?
  • Dayolojia hii ilitokea kati ya nani na nani?
  • Kwa nini mteja alienda kwa muuza duka?
  • Mteja anaishi wapi?
  • Mteja alinunua nini?
  • Mteja alilipa shilingi ngapi kwa muuza duka?
  • Kwa nini mteja alisema kuwa atakuwa akinunua bidhaa zake katika duda hili?
  • Mteja anafanya kazi gani?
  • Mteja anafania wapi kazi?
  • Watoto wa muuza duka wanaitwa nani?
  • Watoto wa muuza duka wanasoma darasa gani?
  • Taja misamiati mitatu ambayo hupatikana sokoni.                       

 Misamiati

Muuza duka. (Shop attendant)      Mteja (customer) Sidiria (bra) Chupi (pants)   Bidhaa (commodities)     Bei (price)   Uza (sell)

HESABU (Counting)

  1. Sufuri Thelathini na moja
  2. Moja Thelathini na mbili
  3. Mbili Thelathini na tatu
  4. Tatu Thelathini na nne
  5. Nne Thelathini na tano
  6. Tano                                   Thelathini na sita
  7. Sita Thelathini na saba
  8. Saba Thelathini na nane
  9. Nane                Thelathini na tisa
  10. Tisa Arobaini
  11. Kumi Hamsini
  12. Kumi na moja Sitini
  13. Kumi na mbili                                 Sabini
  14. Kumi na tatu Themanini
  15. Kumi na nne Tisini
  16. Kumi na tano Mia moja
  17. Kumi na sita                                   Mia moja na moja
  18. Kumi na saba Mia moja na mbili
  19. Kumi na nane Mia moja na tatu
  20. Kumi na tisa   Mia moja na nne
  21. Ishirini Mia moja na tano
  22. Ishirini na moja Mia moja na sita
  23. Ishirini na mbili Mia moja na saba
  24. Ishirini na tatu Mia moja na nane
  25. Ishirini na nne Mia moja na tisa
  26. Ishirini na tano Mia moja na kumi
  27. Ishirini na sita                               Mia moja kumi na moja
  28. Ishirini na saba Mia moja kumi na mbili
  29. Ishirini na nane Mia moja kumi na tatu
  30. Ishirini na tisa                        Mia moja kumi na nne
  31. Thelathini Mia moja kumi na tano
  32. Mia moja kumi na sita 200. Mia mbili
  33. Mia moja kumi na saba 300. Mia tatu
  34. Mia moja kumi na nane 400. Mia nne
  35. Mia moja kumi na tisa 500. Mia tano
  36. Mia moja ishirini 600. Mia sita
  37. Mia moja thelathini 700. Mia saba
  38. Mia moja aronaini 800. Mia nane
  39. Mia moja hamsini 900. Mia tisa
  40. Mia moja sitini 1000. Elfu moja
  41. Mia moja sabini 1001. Elfu moja na moja
  42. Mia moja themanini 1002. Elfu moja na mbili
  43. Mia moja tisini

 

  1. Elfu moja kumi 1020. Elfu moja ishirini
  2. Elfu moja kumi na moja 1030. Elfu moja thelathini
  3. Elfu moja kumi na mbili 1040. Elfu moja arubaini
  4. Elfu moja kumi na tatu
  5. Elfu moja na tisa 2000. Elfu mbili
  6. Elfu moja kumi 3000. Elfu tatu
  7. Elfu moja kumi na moja 4000. Elfu nne
  8. Elfu moja kumi na mbili 5000. Elfu tano
  9. Elfu moja kumi na tatu 6000. Elfu sita
  10. Elfu moja kumi na nne 7000. Elfu saba
  11. Elfu moja kumi na tano 8000. Elfu nane
  12. Elfu moja kumi na sita 9000. Elfu tisa
  13. Elfu moja kumi na saba 10,000. Elfu kumi
  14. Elfu moja kumi na nane 10,001. Elfu kumi na moja
  15. Elfu moja kumi na tisa 10,002. Elfu kumi na mbili

10,010. Elfu kumi kumi                                              100,000. Elfu mia moja/laki moja

10,011. Elfu kumi kumi na moja                                      200,000. Elfu mia mbili/laki mbili

10,020. Elfu kumi ishieini                                                300,000. Elfu mia tatu/laki tatu

10,100. Elfu kumi mia moja                                             400,000. Laki nne

10,999. Elfu kumi mia tisa tisini na tisa                           500,000. Laki tano

11,000. Elfu kumi na moja                                               600,000. Laki sita

12,000. Elfu na mbili                                                        700,000. Laki saba

13,000. Elfu kumi na tatu                                                 800,000. Laki nane

14,000. Elfu kumi na nne                                                 900,000. Laki tisa

15,000. Elfu kumi na tano                                                1,000, 0000. Milioni moja

  1. Elfu kumi na sita 2,000,000. Million mbili

17,000. Elfu kumi na saba                                                3,000,000. Milioni tatu

18,000. Elfu kumi na nane                                               100,000,000. Milioni mia moja

19,000. Elfu kumi na tisa                                                 1,000,000,000. Bilioni moja

20,000. Elfu ishirini  30,000. Elfu thelathini 

40,000. Elfu arubaini                            

50,000. Elfu hamsini                             

60,000. Elfu sitini                          

70,000. Elfu sabini

80,000. Elfu themanini

90,000. Elfu tisini

Noti: Kumbuka kwamba tofauti iliopo kati ya 11,000 na 10,001 ni ya kimatamshi tu. Lakini zote huandikwa sawasawa. (The difference between the above figures in Kiswahili is just in pronounciation but all are written the some way)

 

Zoezi.

Andika herufi zifuatazo katika maneno.

10333                                      17890                         10238                            4, 444,444

19996                                     15555                           2008                             77, 007

111111                                 15, 000, 000                       1019

02                                           720000                        9999999

Alama za Hesabu.
(Mathematical signs)

 

+ Ongeza (add/addition)

X zidisha/ mara (Multiply/multiplication)

÷ Gawia/ gawa (divide by/divide)

–  Toa/ondoa (subtract/subtraction)

= sawa na (equal to)

* Nyota (star)

# Alama ya reli (hash)

% Asilimia (percent)

> Ndogo kuliko (less than)

˂ Kubwa kuliko (greater than)

 

Kwa mfano

  1. 20+30 = 50 (Ishirini ongeza thelathini ni sawa na hamsini)
  2. 12+3 = 15 (kumi na mbili ongeza tatu ni sawa na kumi na tano)
  3. 10×10 = 100 (kumi zidisha kumi ni sawa na mia moja/kumi mara kumi ni sawa na mia moja)
  4. 60 2 = 30 (sitini gawia mbili ni sawa na thelathini)
  5. 8-4 = 4 (Nane toa nne ni sawa na nne)
  6. *12999028400# (nyota 12999028400 alama ya reli)
  7. 5>2 (Tano ni kubwa kuliko mbili)
  8. 2˂5 (Mbili ni ndogo kuliko tano)

Zoezi

  1. Andika kauli zifuatazo kwa kutumia alama za hesabu. (write the following statements using mathematical signs)
  2. Nilienda hatua kumi na tano mbele nikaondoa hatua tatu
  3. Baba yangu alienda sokoni akanunua vitabu kumi, akaongeza kalamu tano, akaogeza vibiriti saba.
  4. Wanafunzi wawili walichuma mapera mia tano. Waligawana sawawsawa. Kila mmoja alipata mangapi?
  5. Mwalimu alipata mshahara wa laki tisa aliondoa laki moja kununua nguo. Alibakisha shilingi ngapi?
  6. Kumi na sita ni kubwa kuliko kumi namoja
  7. Sufuri ni ndogo kuliko tano.
  8. Tulienda sokoni kunua bidhaa. Tulinunua samaki watatu, tukanunua jozi tatu za viatu, tukanunua vyandalua vitatu na kilo tano za sukari. Kila samaki ni shilingi elfu sita, jozi moja ni shilingi elfu ishirini, chandalua kimoja ni shilingi elfu kumi na kilo moja ya sukari ni shilingi elfu nne.

NAMBARI ZA KIRUMI.
(Roman numerals)

  1. Moja XXL. Arubaini                       CC. Mia mbili
  2. mbili XL. Hamsini                          CCC. Mia tatu
  • Tatu LX. Sitini                               CD. Mia nne
  1. Nne LXX. Sabini                            D. Mia tano
  2. Tano
  3. Sita LXXX. Themanini                   DC. Mia sita
  • Saba XC. Tisini
  • Nane
  1. Tisa C. Mia moja                             DCC. Mia saba
  2. Kumi                              DCCC. Mia nane
  3. Kumi na moja CM. Mia tisa
  • Ishirini M. Elfu moja

XXX.   Thelathini

 

 

 

AKISAMI (Fractions)

½. Nusu                                   11/12. Kumi na moja kwa kumi na mbili

1/3.Theluthi                             20/25.Ishirini kwa ishirini na tano

¼. (Robo)                                17/20.  Kumi na saba kwa ishirini

1/5(Humusi)                                  1⅓ . Moja na theluthi

1/6.(Sudusi)                                  3⅓. Tatu na theluthi

1/7.(Subui                                     4⅛. Nee na thumni

1/8. (Thumni)                               3/8.Thumni tatu

1/9. (Tusui)                                  ¾. Robo tatu

1/10. (Ushuri)                               4/9. Tusui nne

ASILIMIA (Percentage)

10%. Asilimia kumi

60%. Asilimia sitini

80%. Asilimia themanini

90.5%. Asilimia tisini nukta tano

17.04%. Asilimia kumi na saba nukta nne

0.005%. Asilimia sufuri nukta sufuri sufuri tano.

SIKU ZA WIKI/JUMA (Days of the week)

Kuna siku saba za wiki. Neno wiki ni sawa na juma. Siku hizi ni zifuatazo. (There are seven days of the week. The word wiki is the same as juma. These days are)

Jumapili (Sunday), Jumatatu (Monday,) Jumanne (Tuesday), Jumatano (Wednesday), Alhamisi (Thursday), Ijumaa (Friday), Jumamosi (Saturday)

Kuna mgogoro kati ya jumapili na jumatatu kuwa siku ya kwanza ya wiki. Lakini kulingana na wakristo, Jumapili ndiyo siku ya kwanza katika wiki. Kulingana na Warabu, Jumamosi ndiyo siku ya kwanza. Hata hivyo, neno mosi humaanisha kwanza. Kwa hivyo Jumamosi humaanisha siku ya kwanza ya wiki/juma. (There is a contradiction about which day is the first in the week, of Sunday and Monday. But according to the Christians, Sunday is the first day of the week where as according to the Arabic calenda Saturday is the first day of the week.the Arabic calenda gives the true meaning of mosi which means first. This means that Jumamosi is the fist day of the week)

Jumapili ni siku ya kwanza ya wiki (Sunday is the fist day of the week)

Jumatatu ni siku ya pili ya wiki (Monday is the second day of the week)

Jumanne ni siku ya tatu ya wiki. (Tuesday is the third day of the week)

Jumatano ni siku ya nne ya wiki. (Wednesday is the fourth day of the week)

Alhamisi ni siku ya tano ya wiki. (Thoursday is the fifth day of the week

Ijumaa ni siku ya sita ya wiki. (Friday is the sixth day of the week)

Jumamosi ni siku ya saba ya wiki. (Saturday is the seventh day of the week)

Sentensi

  1. Nitaenda mjini jumatano (I shall go to town on Wednesday)
  2. Baba yangu huenda sokoni Jumamosi. (My father goe to the market on Saturday)
  3. Wiki hii nitaenda mjini (This week I shall go to town)
  4. Wiki ijayo tutaenda shambani kulima. (Next week we shall go to the garden to dig)
  5. Wiki iliyopita tulisoma vitabu vyetu. (Last week we read ou books)

NOTE

  1. Note the following changes of singular and plural forms of these adverbs

Umoja (singular)                                  wingi (plural)

Wiki hii (this week)                                wiki hizi (these weeks)

Wiki ijayo (next week)                           wiki zijazo (coming weeks)

Wiki iliyopita (last week)                       wiki zilizopita (past weeks)

  1. It is important to know the tense that is grammatically correct in accordance to the above adverbs. Eg

It is wrong to say wiki ilyopita nitaenda kwa soko (Last week I shall go to the market) it is supposed to be, Wiki iliyopita nilienda kwa soko (Last week I went to the market)

Wiki hii/wiki hizi use Present/Future/Past tenses

Wiki ijayo/wiki zijazo use future tense

Wiki iliyopita/wiki zilizopita use past tense

MIEZI YA MWAKA (Months of the year)

Kuna miezi kumi na miwili katika mwaka kama ilivyo hapa chini.

Januari: January (Ni mwezi wa kwanza wa mwaka)

Febriari: February (Ni mwezi wa pili wa mwaka)

Machi: March (Ni mwezi wa tatu wa mwaka)

Aprili: April (Ni mwezi wa nne wa mwaka)

Mei: May (Ni mwezi wa tano wa mwaka)

Juni: June (Ni mwezi wa sita wa mwaka)

Julai: July (Ni mwezi wa saba wa mwaka)

Agosti: August (Ni mwezi wa nane wa mwaka)

Septemba: September (Ni mwezi wa tisa wa mwaka)

Oktoba: October (Ni mwezi wa tisa wa mwaka)

Novemba: November (Ni mwezi wa kumi na moja wa mwaka)

Desemba: December (Ni mwezi wa kumi na mbili wa mwaka)

 

Umoja                                                                                 wingi

Mwezi huu (this month)                                             Miezi hii (these months)

Mwezi uliopita last/previous month)                           Miezi iliyopita (passed months)

Mwezi ujao/mwezi kesho (next month)                      Miezi ijayo (coming months)

Sentensi

  1. Mwezi huu tungependa kuenda ughaibuni. (This year we would like to go abroad)
  2. Mwalimu alienda Nairobi mwezi uliopita. (The teacher went to Nairobi last month)
  3. Shule yetu itatunua gari mwezi ujao. (Our school shall buy the vehicle next month)
  4. Mama yangu alizaa kitinda mimba wetu mwezi uliopita. (My mother gave birth to our last-born last month.
  5. Sisi tutanunua vitabu mwezi ujao. (We shall buy the books next month)

KUSOMA TAREHE (Reading date)

Kwa mfano.

  1. 1st/01/2000. Tarehe moja/mosi, mwezi wa januari, mwaka wa elfu mbili
  2. 2nd/03/1999. Tarehe mbili, mwezi wa machi mwaka wa elfu moja mia tisa, tisini na tisa.
  3. 9th/05/1990. Tarehe tisa, mwezi wa mei, mwaka wa elfu moja mia tisa tisini.
  4. 15th/12/1988. Tarehe kumi na tano, mwezi wa desemba, mwaka wa elfu moja mia tisa themanini na nane.
  5. 31st/11/1940. Tarehe thelathini na moja , mwezi wa novemba, mwaka wa elfu moja mia tisa arubaini.

Zoezi.

Andika tarehe zifuatazo katika Kiswahili.

  1. 02/09/1414
  2. 22/06/1910
  3. 11/07/1934
  4. 08/09/1739
  5. Nchi ya Uganda ilipata uhuru tatehe ngapi? (When did Uganda get her ndipendence?)
  6. Ulizaliwa tarehe ngapi? (When were you born?)
  7. Utamaliza kusoma tarehe ngapi? (when will you finish studies/reading)
  8. Utaenda mjini tarehe ngapi? When will you go to town?)
  9. Yesu kristo alizaliwa tarehe ngapi? When was Jesus Christ born?
  10. Leo ni tarehe ngapi? (When is today/which date ia today?)
  11. Kesho ni tarehe ngapi? (Which date is tomorrow?)
  12. Jana ilikuwa tarehe ngapi? (Which date was yesterday?)
  13. Juzi ilikuwa tarehe ngapi? (Which date was the previous day)

KUSOMA SAA (Reading Time)

Tunaposoma saa, misamiati ifuatayo ni muhimu kuijua. (When reading time, the following vocaburies are important to know)

Saa   (Time/ a watch/ hour)

Sekunde (Seconds)

Dakika (Minutes)

Robo   (Aquarter passed/15 minutes passed)

Kamili (exactly)

Nusu    (Half an hour/30min)

Kasorobo (Aquarter to/15 min to the next hour)

Kasoro (Minutes remaining to the next hour)

Asubuhi (Morning/time between 12:00am-11:59am)

Mchana/adhuhuri (Afternoon/ time between 12:00pm-4:59pm)

Jioni (Evening time between 5:00pm-6:59pm)

Usiku (Night/ time between 7:00-11:59pm)

Alfajiri (The period of the morning before the sunrises, usually between 5:00am-6:30am)

Alasiri (A period from 2:00pm-4:59pm/late afternoon)

Usiku wa manane (In the dead of the night/time between 2:00am-3:00am)

Machweo/magharibi (Sunset)

Macheo/mapambazuko (Sunrise)

Mafungulia ng’ombe (Time when animals are let out for grazing in the morning)

Mafungianyama (The time when animals are brought back from the grazing in the evening)

Kwa mfano

Asubuhi (12:00am-11:59am)

7:00am   Saa moja kamili asubuhi

7:15am   Saa moja dakika kumi na tano asubuhi/saa moja na robo asubuhi.

7:30am   saa moja dakika thelathini asuhuhi/ saa moja na nusu asubuhi

7:45am   Saa mbili kasorobo asuhuhi/saa moja dakika arubaini na tano asubuhi (Aquater to 8:00pm)

7:50am   Saa moja dakika hamsini asubuhi/saa mbili kasoro dakika kumi asubuhi. (Ten minutes to eight oclock)

Mchana/adhuhuri (12:00pm-4:59pm)

12:00pm    Saa sita kamili za mchana

1:15pm       Saa saba dakika kumi na tano mchana/saa saba na robo mchana

1:30pm      Saa saba dakika thelathini mchana/saa saba na nusu mchana

2:45pm     Saa nane dakika arobaini na tano mchana/saa tisa kasorobo mchana/alasiri

Jioni (5:00pm-6:59pm)

5:00pm     Saa kumi na moja kamili jioni

6:12pm     Saa kumi na mbili dakika kumi na mbili jioni

5:30pm      Saa kumi na moja dakika thelathini joni

6:45pm     Saa kumi na mbili dakika arubaini na tano jioni/ saa moja kasorobo usiku (aquater to seven)

5:53pm      Saa kumi na mbili kasoro dakika saba. (Seven minutes to seven)

Usiku (7:00pm-11:59pm)

8:00pm   Saa mbili kamili usiku

9:14pm   Saa tatu dakika kumi na nne usiku

10:35pm Saa nne dakika thelathini na tano usiku

11:59pm Saa tano dakika hamsini na tisa usiku

NOTE

  1. When reading time, you must state/indicate the period of that particular time you refer to eg mchana, jioni, asubuhi, usiku. etc
  2. In 24 hours, time is divided into pm and am. These are undersood better by identifying when different periods begin since in Kiswahili, these distinctions are not specific/clear, as it is in English.
  3. Alasiri is part of the afternoon. Either therefore, you can use alasiri or mchana for the time indicated by it and so is for alfajiri, which is part of morning. In the period of alasiri, you can as well use mchana and so is alfajiri /usiku wa manane, asubuhi can be used to avoid confusion.
  4. The following can be abbreviated in kiswahili as,

Asubuhi      As e.g 8:00As (8:00am)

Mchana      Mch e.g 12.00Mch (12:00Pm)

Jioni            Jn e.g 05:00Jn (05:00pm)

Usiku          Usk e.g 07:00Usk (07:00pm)

ZOEZI

Andika saa zifuatazo katika lugha ya Kiswahili

  1. 9:00pm 10:50pm
  2. 8:15am 2:30am
  3. 11:10pm 6:00am
  4. 3:23pm 7:00pm
 

Courses

Featured Downloads