To provide the best experiences, we use technologies like cookies to store and/or access device information. Consenting to these technologies will allow us to process data such as browsing behavior or unique IDs on this site. Not consenting or withdrawing consent, may adversely affect certain features and functions.
The technical storage or access is strictly necessary for the legitimate purpose of enabling the use of a specific service explicitly requested by the subscriber or user, or for the sole purpose of carrying out the transmission of a communication over an electronic communications network.
The technical storage or access is necessary for the legitimate purpose of storing preferences that are not requested by the subscriber or user.
The technical storage or access that is used exclusively for statistical purposes.
The technical storage or access that is used exclusively for anonymous statistical purposes. Without a subpoena, voluntary compliance on the part of your Internet Service Provider, or additional records from a third party, information stored or retrieved for this purpose alone cannot usually be used to identify you.
The technical storage or access is required to create user profiles to send advertising, or to track the user on a website or across several websites for similar marketing purposes.
Jumuiya ya Afrika Mashariki
Utangulizi
Nadhani umewahi kusikia methali kwamba umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Hii ina maana kwamba kuwa na nguvu, watu wanahitaji kuungana na kufanya kazi kwa pamoja. Ikiwa si hivyo, basi, hawatafika mbali na hawatafanya kazi kubwa. Hii ndiyo sababu watu hushirikiana na kuunda mashirika kwa sababu ushirikiano huo huwapa nguvu. Je, unajua sababu kwa nini watu huungana? Je, kuna chama chochote au kikundi chochote ambacho wewe ni mwanachama au mwanakikundi? Ikiwa wewe ni mwanachama, unaweza kueleza sababu za kuunda chama hicho? Ikiwa wewe si mwanachama chochote
lakini unajua chama cha wengine, unaweza kutabiri sababu za kuunda chama chao? Katika mada hii, utajifunza juu ya muungano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ili uweze kuibuka ukiwa mzalendo anayethamini utaifa na umataifa. Utaweza kutumia msamiati unaohusiana na muungano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mawasiliano yako ya kila siku. Aidha, utakuza na kuendeleza umoja na ushirikiano, kuthamini, kufanya kazi kwa bidii, kulinda Amani, uhuru na utamaduni wa nchi yako kwa ajili ya kujenga jumuiya bora.
Stadi za lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo a: KuimbawimbowaJumuiayaya Afrika Mashariki
Utangulizi
Miongoni mwa vifaa vinavyotambulisha na kutofautisha shirika, shule au nchi ni wimbo rasmi wa taifa hilo au shirika hilo. Jumuiya ya Afrika Mashariki ina wimbo unaohimiza na kushauri jamii kuisha kwa pamoja katika maisha. Je, unajua wimbo wa Afrika Mashariki? Je, unajua beti zote za wimbo huo? Katika
mada hii, utajifunza kuimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kukariri na kuimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Masharik
Shughuli 7.1
Kariri wimbo wa jumuiya Afrika mashariki kisha kuimba.
2.
WIMBO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Ee Mungu twaomba uilinde
Jumuiya Afrika Mashariki
Tuwezeshe Kuishi kwa amani
Tutimize na malengo yetu.
KIBWAGIZO
Jumuiya Yetu sote tui/inde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu. Uzalendo pia mshikamano
Viwe msingi wa Umoja wetu
Na tuilinde uhuru na Amani
Mila zetu na desturi zetu.
Viwandani na hata mashambani
Tufanye kazi sote kwa makini
Tujitoe kwa hali na mali
Tuijenge Jumuiya bora.
2.Katika vikundi, imbeni wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Baadaye, vikundi vyote viungane pamoja viimbe wimbo huo kwa pamoja.
Stadi za lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo b: Kueleza Ujumbe Unaojitokeza Katika Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Utangulizi
Ujumbe ni wazo ambalo hujitokeza katika mazungumzo au maelezo; yawe yameandikwa au yamesemwa kimdomo. Kwa hiyo, kila wimbo unaoimbwa huwa na ujumbe unalenga kutoa. Je, umewahi kusikiliza wimbo wowote? Wimbo huo ulikuwa na ujumbe gani? Ikiwa kuna wimbo wowote usio na ujumbe, wimbo huo haufai. Mada hii itakuwezesha kueleza ujumbe uliomo katika wimbo wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kueleza ujumbe unaopatikana katika wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Taz: Umetambua kuwa wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki in jumla ya stanza atu na kiitikio kimoja ambacho huimba baada ya kila stanza. Umelewa kuwa wimbo huu unahimiza, kumotisha na kushauri jamii kuishi kwa amani daima kwa mendeleo endelevu ya jamii nzima na mengineyo mengi.
Stadi za lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika Funzo c: kutaja nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki
Taz: Umetambua kuwa wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki in jumla ya stanza tatu na kiitikio kimoja ambacho huimba baada ya kila stanza. Umelewa kuwa wimbo huu unahimiza, kumotisha na kushauri jamii kuishi kwa amani daima kwa mendeleo endelevu ya jamii nzima na mengineyo mengi.
Stadi za lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo c: kutaja nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki
Muungano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umekuwapo kwa sababu ya kuungana kwa nchi fulani. Je, unajua idadi ya nchi zinazounda muungano wa Afrika Mashariki? Unaweza kutaja majina ya nchi hizo? Mada ndogo hii itakuwezesha kutaja majina na idadi ya nchi zilizomo katika muungano wa
Afrika Mashariki.
Kutaja nchi zilizomo katika Muungano wa Jumuiya ya Shughuli 7.3
Afrika Mashariki
Mkiwa katika vikundi,
Taz: Katika funzo hili, umejifunza kuwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni nchi ambazo hupatikana katika ukanda wa Afrika Mashariki. Wengine huziita nchi hizi nchi za maziwani. Afrika Mashariki ilianzishwa wakati wa ukoloni,na kuendelezwa baada ya uhuru wa mataifa matatu ya
jumuiya ya Afrika mashariki. Jumuiya hii ilipata majina mbalimbali kuanzia utawala wa kikoloni, baada ya uhuru na kuanzia miaka ya 1992. Fanya utafiti juu ya haya ujinufaishe zaidi.
Watu hawawezi kukubali kushirikiana bila kunufaika au kunufaisha jamii. Ushirikano ambao unajenga jamii na watu wake ni ushirikiano chanya. Je unaweza keleza sababu kwa nini watu hushirikiana? Unaweza kueleza umuhimu wa muungano wa jumuiya ya Afrika Mashariki? Mada ndogo hii
itakuwezesha kujadili umuhimu wa muungano wa Afrika Mashariki.
Kueleza umuhimu wa muungano wa Jumuiya ya
Shughuli 7.4
Afrika Mashariki.
Katika vikundi, jadiliana juu ya umuhimu wa muungano wa Afrika Mashariki.
Wasilisheni hoja mlizojadili mbele ya wanafunzi, darasani.
Funzo e: Kusoma makala na kujibu maswali
Kusoma makala kuhusu sababu za kuzinduliwa kwa
Shughuli 7.5
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
soma makala yafuatayo na kisha ujibu maswali yanayofuata. Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyoanzishwa na wakoloni karne ya ishirini ilikuja kupokezwa nchi husika baada ya uhuru mwaka 1961. Hata hvyo, baada ya
mwaka 1977, jumuiya ya Afrika Mashariki ilikuwa imefifia kwa sababu ya kisiasa na kiuchumi pamoja na kijamii. Baada ya miaka 23 ya kuanguka kwa jumuiya ya Afrika Mashariki, mfumko wake ulizinduliwa mwaka 1993. Kufikia mwaka 1999, mkataba wa kuzinduliwa kwa jumuiya ya Afrika Mashariki ulitiwa
saini tarehe 30 Novemba, 1999 na kuanza kutumika rasmi tarehe 7 Julai, 2000 baada ya nchi hizo kuridhia mkataba huo.
Nchi zilizozindua jumuiya zilikuwa tatu, Kenya Tanzania na Uganda. Sababu kuu ya kuanzishwa kwa ushirika huu ilikuwa kuziunganisha nchi hizi kisiasa, kiuchumi na kijamii. Sababu ya nchi hizi kuingia katika ushirikiano ilikuwa ni kuimarisha biashara, uwekezaji na maendeleo ya viwanda kati ya nchi hizo.
Pia zilikuwa na nia ya kuwa na Sarafu moja na Sera za Fedha. Aidha walikuwa na sababu ya kuweka Miundombinu na huduma ya pamoja ili itekelezwe kama ilivyotekelezwa kati ya Kenya, Tanzania na Uganda huduma ya pamoja katika mipaka yao. Kwenda Tanzania ukaguzi wa forodha na stakabadhi za usafiri hufanyiwa Tanzania na ukitoka Tanzania ukaguzi hufanyika Uganda.
Muungano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulilenga kudumisha utendakazi, Sayansi na Teknolajia; usafiri usio na vikwazo na masharti. Mfanyakazi mwenye marifa fulani ana uwezo wa kwenda na kufanya kazi katika nchi mwanachama bila vikwazo, kutumia simu na mtandao akiwa katika nchi mwanachama, na
hata kuendeleza uzalishaji mali. Tumeona haya yamefanikishwa ambapo unapata baadhi ya mabasi kama Friends, Modern Coast, Masha Poa, Trinity, Jaguar, Gateway, na kadhalika yakisafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine. Jambojingine ambalo lililengwa kukuzwa ni kilimo ambacho kilipewa kipaumbele
hasa uzalishaji, usafirishaji na uuzaji wa chakula katika nchi zote zilizomo katika muungano. Ushuru wa bidhaa hivi uliwekwa chini na ushuru kuondolewa kwa baadhi ya vyakula. Mahindi, maharagwe, mboga, njugu, unga, n.k husafirishwa bila ushuru kwa sababu hivi ni vyakula vya wananchi wa Afrika Mashariki. Hali hii ilikuwa na sababu ya kuimarisha kilimo na kuhakikisha kuwa baa la njaa
linaondolewa Afrika Mashariki.
Mazingira na usimamizi wa mali asili, utalii na usimamizi wa wanyamapori ni miongoni mwa sekta ambazo muungano ulikubaliana kukuza. Lengo kuu lilikuwa ni kulinda mazingira ambayo yataendeleza uzalishaji wa maliasili, kuwavutia watalii wa ndani na nje na kujenga Afrika Mashariki yenye manufaa
kwa watu wake na wageni. Kwa mfano, Tanzania na Kenya wana mbuga moja ya wanyamapori ambapo wanyama kama nyumba na Vifaru hutoka Tanzania na kuja malishoni Kenya na baadaye hurudi Tanzania. Kwa hiyo ulinzi ulikuwa na manufaa mengi sana.
Kwa jumla, kumekuwa na uendelezaji wa mikataba ya shughuli za kiafya, kijamii na kitamaduni. Pia kumekuwa na ushirikishwaji wa sekta za kibinafsi na jumuiya ya kiraia pamoja na ushirikiano katika masuala ya sheria na utoaji haki. Masuala ya kisiasa kama vile ulinzi, usalama wa ndani na mambo ya nje
yote yanasisitizwa. Haya yote ndiyo yalisababisha kuanzisha na kuendeleza muungano wa jumuiya. Muungano huu una nyaraka zenye taarifa zaidi. Ukizisoma au kuzitafuta kwenye mitandao ya intaneti utanufaika zaidi.
Maswali
1.Katika vikundi, elezeni sababu za kuzinduliwa kwa muungano wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
2.Tumieni mtandao au maktaba kutafuta sababu nyingine za kuzinduliwa
kwa muungano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mbali na zile zilizotajwa katika taarifa.
a) Katika vikundi, tathmini sababu za muungano mlizotoa hapo juu na kueleza ikiwa zimetimizwa au zimeshindwa.
b) Tambueni maneno magumu katika taarifa na mtumie kamusi kutafuta maana ya kila neno mlilotambua.
stadi za lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo f: Sarufi – Kutunga sentensi kutumia viwakilishi
Virejeshi
Utangulizi
viwakilishi virejeshi ni maneno yanayotumika kuelezea zaidi kuhusu nominotajwa kwa njia ya kuifafanua zaidi. Unaweza kutambua maneno hayo na kutunga sentensi? Mada ndogo hii itakuwezesha kutunga sentensi kwa kutumia vireshi amba- na O- rejeshi.
Kutunga sentensi kwa kutumia viwakilishi virejeshi Katika vikundi, tambueni viwakilishi virejeshi katika sentensi zifuatazo:
Tambueni nomino zinazohusiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuzitumia kutunga sentensi mkitumia amba- na o-rejeshi kwa umoja na wingi.
Taz: Katika funzo hili, umetambua kuwa vivumishi virejeshi vinaweza kuwa vya O-rejeshi au amba- ambavyo hutumika kurejelea nomino. Vivumishi hivi hutumika kulingana na ngeli.
Stadi za lugha: kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo g: Udogo na ukubwa wa nomino
Utangulizi
Maneno yote katika lugha huwa katika hali ya wasatni au kawaida. Maneno haya yanawezwa kugeuzwa na kuwekwa katika hali ya ukubwa au udogo yanapozidi kiasi cha wastani au hali inayotarajiwa. Je, unatambua baadhi ya nomino za udogo na ukubwa ambazo hujitokeza katika lugha ya Kiswahili au
mnazotumia katika jamii yenu? Mada ndogo hii itakuwezesha kujifunza juu ya udogo na ukubwa wa nomino ili uzitumie katika mawasiliano yako ya kila siku.
Shughuli 7.7
1.Kutumia ukubwa na udogo wa nomino kutunga senteni
1.Katika vikundi, tambueni angalau nomino ishirini katika hali ya ukubwa.
2.Tambueni angalau nomino ishirini katika hali ya udogo.
3.Kwa kila nomino mliyotambua, tungeni sentensi sahihi mkitumia nomino hizo.
4.Jazeni jedwali kuonyesha ukubwa na udogo wa nomino
5.
Fuateni maagizo ili kubadilisha sentensi hizi katika hali mliyoagizwa kufuata.
a) Mtu aliingia chumbani na kutuibia (ukubwa)
b)Mbwa mkubwa alimkimbiza mwizi. ( andika katika ukubwa)
c)Kijoka kilichokutisha kimeuliwa. ( andika katika wingi)
d)Watoto wadogo wameenda nyumbani kulala. ( andika katika ukubwa)
e)Milima iliyoboromoka imeangamiza watu wengi ( andika katika udogo)
f)Msichana yule mdogo anafanya kazi vizuri sana. (andika katika udogo kwa wingi)
Taz: Umejifunza kuwa maneno ya kawaida huweza kugeuzwa kudhihirisha dhana kadhaa kama vile kusifia, kudunisha au kudharau. Ili kufanikisha dhamira hizi, umetambUa kuwa kuna kanuni zinazozingatiwa kuyageuza maneno au nomino husika katika hali ya ukubwa na Udogo. Kwa mfano, majina yote katika ukubwa hutumia ngeli ya Ii-ya kuonyesha ukubwa wa nomino, kuongeza kiambishi ji- au kuondoa kiwakilishi cha ngeli kutegemea viambishi vya ngeli. Nomino ambazo huanza na kikatika hali ya kawaida, huweza kugeuzwa katika ukubwa kwa kudondosha kiambishi awali ki- na badala yake kutumia kiambishi ji-. Ji- hutumika vile vile kwenye maneno ya silabi mbili ambayo si lazima yawe yameanza na kiambishi ki- Kama vile (Mtu – Jitu).Nomino zinazoanza na kiambishi ch- mwanzoni, hudondoshwa na badala yake kiambishi ji hutumika kuwakilisha ukubwa. Kundi la nomino za ngeli ya Ii-ya pamoja na ngeli nyingine
zisizokuwa na kiambishi maalumu katika umoja hutumia kiambishi Ji. Kama nomino imeanza na kiambishi ji, Kiambishi kingine cha ji huongezwa tena ili kuunda ukubwa, kwa mfano, Jina – Jijina.
Udogo wa Nomino
Shughuli 7.8
Kutambua na kutumia udogo wa nomino katika sentensi Maneno vilevile huweza kuwekwa kwa udogo ili kusifia udogo wake au kudunisha nomino husika au kuonyesha madharau. Je, umewahi kutumia au
kusikia watu wakitumia udogo wa nomino? Somo hili Iitakuwezesha kutumia nomino katika udogo wake.
b) Mto
a) Kiti
d) Chungu e) Mji
c) Mlango
hapo juu .
Taz: Katika funzo hili, unatambua kuwa kuweka nomino katika hali ya udogo, ngeli ya ki-vi hutumika ambapo kwa kutumia kiambishi ki- au kiji- au kuacha kiambishi cha ngeli katika neno husika.
Stadi za lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo h: Kutambua vinyume Vya Vitenzi na kuvitumia katika sentensi
Utangulizi
Kinyume ni hali inayopinga au kukinzana na nyingine. Kwa hiyo kinyume cha vitenzi ni kitenzi kinachokinzana au kupingana. Unakumbuka ulichojifunza katika sura ya tano, mada ndogo G? Je, unakumbuka kanuni ya kuandika kinyume? Katika mada ndogo hii, utajifunza zaidi kuhusu matumizi ya vinyume vya vitenzi.
Stadi za lugha: Kusikiliza na Kuzungumza Kufumbua
Funzo i: Fasili Simulizi mbalimbali mafumbo
Katika kidato cha pili, ulijifunza kuhusu mafumbo na ukaeleza maana yake. Je, unakumbuka maana ya neno fumbo? Unajua umuhimu wa mafumbo katika maisha ya mtu? Mada ndogo hii itakuwezesha kufumba na kufumbua mafumbo na pia kuthamini umuhimu wa mafumbo kwa watu.
MafumbO
Kufumba na kufumbua mafumbo
Katika vikundi, jadilianeni juu ya maana ya fumbo. Baada ya kuelezea maana ya fumbo, tambueni mafumbo yanayohusiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa mafano, mafumbo yanayozungukia ushirikiano, uzalendo, umoja, n.k
a) Fumbo: Mimi, ndugu yangu, na babangu tulishirikiana na kuchanga pesa za kununua mfugo wa kuzalisha mali. Tulipofika sokoni, baba alituamrisha kununua fahali watatu. Tuliwanunua na
kwenda nyumbani. Matumaini yetu ni kwamba baada ya mwaka, kila mmoja akizaa, tutapata ng,ombe wengi. Kwa hiyo, baada ya mwaka, tutakuwa na fahali wangapi kwa ujumla?
b) Fumbo: Juma ana vitu vitatu; mbwa, mbuzi na nyasi anavyotaka kuvusha mto wa Kagera na kuvipeleka Tanzania. Sheria za daraja analotaka kuvuka na vitu vyake ni kwamba, hawezi kuvusha vitu
viwili kwa pamoja. Ni lazima avushe kimoja kimoja. Akivusha mbwa kwanza, mbuzi atakula nyasi zake, Akiacha mbwa na mbuzi, mbwa atakula mbuzi. Je, alifanyaje kuvusha vitu vyake?
c) Nina watoto wawili; mmoja ana tumbo na kichwa kikubwa na mwingine hana. Nitafanyaje ili wawe sawa? d) Nilipokuwa na Mutoni pamoja na watoto wangu, mmoja alituhadhariSha kutopita vichochoroni kuelekea nyumbani. Hata hivyo ni hatari sana kupita katika kichochoro kimoja ukiwa pekee, Kwa hiyo, Bi. Mutoni alitufahamisha kuwa ikiwa mahali ni hatari ni vyema usipite peke yako na kama unataka kuwapa ujasiri wavamizi kuwavamia basi mnaweza kupita kwa ushirika wa watu
zaidi ya mmoja.Unafikiri Bi Mutoni alikuwa akimaanisha nini?
Taz:Umejifunza kuwa mafumbo ni semi zinazotumia lugha ya kumfikirisha au kumpa msikilizaji kazi ngumu ya kutambua au kifichua maana ya usemi husika. Ni usemi wa kuchemsha ubongo wa msikilizaji. Mafumbo hufumbuliwa kulingana na muktadha, mazingira na hali. Unaweza kufumba mafumbo kwa njia ya kufurahisha kwa kufuata mfumo huu;
1.Nina kuku wangu sita. Ndege alipita juu ya nyumba yetu, kuku wote waliangalia juu kuona ndege huyo. Ni macho mangapi ya kuku yaliyoona ndege kwa pamoja?
2.Treni ya umeme inakimbia kuelekea Mashariki. Moshi inaotoa utaelekea upande upi?
Stadi za lugha: Kusoma na Kuandika
Funzo j: Kutambua hatua mwafaka za uandishiwa insha
ya maelezo
Utangulizi
Insha ni utungo juu ya jambo fulani ambao huandikwa kwa lugha ya nathari ya kuvutia, kupangwa kwa njia iliyo nzuri, yenye mtriririko wa mawazo na muktadha uliounganika vizuri kuelezea juu ya kisa au wazo. Je, unaweza kutambua insha ya maelezo ni insha ya aina gani? Unatambua hatua ambazo huzingatiwa
wakati wa kuandika insha ya aina hii? Katika funzo hili, utajifunza kuhusu hatua mwafaka za kuandika insha ya maelezo.
‘ ‘3 Shughuli 7.11
Kutambua hatua za uandishi wa insha ya maelezo
Stadi za lugha: Kuandika Funzo k: Insha ya maelezo- Kuandika insha kuhusu
Jumuiya ya Afrika Mashariki
Kuandika insha kuhusu faida za muungano wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki
Baada ya kutambua hatua za uandishi wa insha ya maelezo;
Assignment
ASSIGNMENT : Shughuli Jumlishi Pendekezwa juu Jumuiya ya Afrika Mashariki MARKS : 10 DURATION : 1 week, 3 days