To provide the best experiences, we use technologies like cookies to store and/or access device information. Consenting to these technologies will allow us to process data such as browsing behavior or unique IDs on this site. Not consenting or withdrawing consent, may adversely affect certain features and functions.
The technical storage or access is strictly necessary for the legitimate purpose of enabling the use of a specific service explicitly requested by the subscriber or user, or for the sole purpose of carrying out the transmission of a communication over an electronic communications network.
The technical storage or access is necessary for the legitimate purpose of storing preferences that are not requested by the subscriber or user.
The technical storage or access that is used exclusively for statistical purposes.
The technical storage or access that is used exclusively for anonymous statistical purposes. Without a subpoena, voluntary compliance on the part of your Internet Service Provider, or additional records from a third party, information stored or retrieved for this purpose alone cannot usually be used to identify you.
The technical storage or access is required to create user profiles to send advertising, or to track the user on a website or across several websites for similar marketing purposes.
LSC: MADA KUU 1.4 WANYAMA NA NDEGE
Utangulizi
Nchi ya Uganda ina utajiri mwingi kutokana na wanyama na ndege wa aina mbalimbali. Baadhi ya Wanyama hawa ni wa nyumbani na wengine ni wa porini. Vilevile, baadhi ya ndege hawa ni wa nyumbani na wengine ni wa porini. Je, kuna wanyama wowote unaojua? Ni wanyama gani wa nyumbani unaojua? Je, kuna wanyama wa porini unaojua? Je, Wanyama hao wana umuhimu gani kwa jamii? Unajua umuhimu wa ndege kwa jamii?
Funzo a: Kutambua majina ya wanyama na ndege wa nyumbani
Shughuli 1.4: Kusikiliza na kuzungumza
1. Katika vikundi;
(a) Jadiliana kuhusu wanyama wa nyumbani na kisha kila kikundi kitaje majina ya wanyama waliojadiliana.
(b) Jadiliana kuhusu ndege wa nyumbani na kisha kila kikundi kitaje ndege waliojadiliana.
(c) Tazameni michoro ya wanyama iliyopo hapa chini na kila mmoja ataje majina ya wanyama hao. Chagua jina sahihi kutoka yale uliyopewa katika boksi hapo chini.
WANYAMA WA NYUMBANI
Ng’ombe Mbuzi Punda
Farasi Kondoo Sungura
2. Katika jozi,
(a) Kubalianeni kati yenu juu ya milio ya wanyama au ndege na kila mmoja wenu atoe milio ya wanyama wawili.
WANYAMA/NDEGE NA MILIO YAO
A B
Mbuzi Klaak-klaak
Kondoo Kwaak-kwaak
Kuku Mee-mee
Paka Moo-moo
Mbwa Bwoo-bwow
Bata Baa-baa
Ng’ombe miaw-miaw
b) Shirikiana kueleza umuhimu ndege wafuatayo.
FAIDA ZA WANYAMA WA NYUMBANI.
MNYAMA FAIDA
a) Mbuzi Nyama, maziwa ,ngozi, mbolea.
b) Ng’ombe Maziwa, nyama, mbolea,ngozi.
c) Punda Kubeba mizigo,usafiri ,mbolea.
d) Farasi Kubeba mizigo,usafiri,mbolea,michezo mbalimbali.
d) Kondoo Nyama,maziwa,sufu,ngozi,mbolea.
e) Paka Kushika panya.
f) Mbwa Ulinzi na usalama.
g) Sungura Nyama,mbolea.
h) Nguruwe Nyama ,mbolea
i)Ngamia Kubeba mizigo,usafiri,nyama,mbolea,ngozi.
Funzo b: WANYAMA NA NDEGE WA PORINI.
Simba ndovu Pundamilia
Fisi Sokwe Tumbili
wanyama na ndege wengine ni ;
ngiri ,chuimilia ,chui, twiga ,nyati,korongo ,bundi, tai ,mwewe ,kuku ,jogoo kifaranga ,batamzinga nk.
Funzo d: Kutambua vikembe mbalimbali.
VIKEMBE;
Hawa ni watoto wa wanyama. Vikembe ni pamoja na:
Shughuli 4.4: Kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika
(a) Katika jozi, tumieni kamusi, maktaba au mtandao kutafiti kuhusu vikembe mbalimbali. Baada ya utafiti, kila jozi liwasilishe majina ya vikembe darasani mbele ya wanafunzi wengine darasani.
(b) Katika vikundi, jadiliana na kuandika majina yaa vikembe na kila kikembe andikeni jina la mzazi wake.
Funzo e: Kusoma Makala kuhusu sifa za wanyama na ndege.
wanyama wengi wanatembea katika vikundi.
wanyama wanakula.
wanyama wanafa.
wanyama wanazaa.
wanyama wanapenda.
Ndege wanaweka mayayi.
Faida za wanyama wa nyumbani
Wanyama wa nyumbani ni wale ambao wanakubali kufugika na kuridhiana na mwanadamu katika mazingira ya kinyumbani, bila ya madhara mabaya.
Wanyama hawa wafugwao wana faida chungu nzima kwa mwanadamu; kuna ngamia, ng’ombe, mbuzi, mbwa paka, sungura na wengineo. Miongoni mwao wamo waliwao na wale wasioliwa, ingawaje wasioliwa pia wana umuhimu wao mwingi kwa mwanadamu; kama vile mbwa ni mlinzi madhubuti, farasi naye ni hodari kwa ubebaji wa mizigo na
usafiri. Paka ni msasi wa panya pamoja na faida nyingine nyingi.
Ama wale waliwao tukianza na ng’ombe ana manufaa makubwa katika harakati za ulimaji. Pakosekanapo trakta basi yeye huingia kazi, huchangia sehemu kubwa ya uchumi na maendeleo katika kilimo na ufugaji. Na kama ilivyo kawaida kuwa nyama zao ni kitowe, huliwa na kuuzwa pamoja na kutupa maziwa. Ngozi kama za ngamia, ng’ombe na mbuzi huleta pesa nyingi, kwani ni mali ghafi ya vifaa vingi kama vile viatu, mabegi, mikanda, majaketi, kofia, foronya za viti na kadhalika.
Ufugaji wa wanyama wote wa nyumbani waliwao na wasioliwa ni kitega uchumi kikubwa ambacho huleta maendeleo ya kiuchumi kwa mfugaji binafsi na taifa kwa ujumla.
Shirikiana na wenzako kujibu maswali
(a) Unaelewa nini kuhusu wanyama wa nyumbani kulingana na taarifa hii?
(b) Taja wanyama watano wa nyumbani waliwao.
(c) Taja wanyama watatu wa nyumbani wasioliwa.
(d) Eleza faida tatu za ng’ombe.
(e) Ni vitu gani ambavyo hutengenezwa kwa ngozi za wanyama?
Sarufi:
Funzo f: Kutumia vivumishi vimilikishi katika sentensi
Shughuli 6.4: Kusoma na kuandika
Katika makundi;
i. Jadiliana na kutambua maana ya vivumishi vimilikishi huku mkitoa mifano.
ii. Tumieni vivumishi vimilikishi mlivyotambua katika i. hapo juu kutunga sentensi mkitumia nomino za a-wa zinazotaja wanyama na ndege.
Funzo g: Kutumia vipatanishi vya nomino za ngeli ya a-wa katika sentensi
Mbuzi
Simba
Wetu
Wao
wake
Mbuzi
Simba
Wetu
Wao
wake
Shughuli 7.4: Kusoma na Kuandika
Mkiwa katika vikundi,
i. Jadiliana kuhusu nomino za ngeli ya a-wa zinazotaja majina ya wanyama na ndege na kisha mziandike nomino hizo katika madaftari yenu.
ii. Tungeni sentensi sahihi kwa kutumia vipatanishi vya kisarufi vya ngeli ya a-wa. Sentensi hizi ziandikwe kwa chati kwa umoja na wingi na kutundikwa ukutani ili vikundi vingine vilinganishe na zao.
Funzo h: Kuandika insha kutokana na ufasiri wa michoro.
Shughuli 8.4: Kuandika.
a.Mada ikibadilika na kuwa “ndege wa porini wana umuhimu mkubwa kwa jamii” Eleza hoja ambazo utatoa kuunga mkono mada hiyo.
b Tunga sentensi tano katika wakati uliopo kwa kutumia majina ya wanyama na kisha uzigeuze sentensi hizo kwa wingi.
Muhtasari wa mada
Katika mada hii, umejifunza kuhusu,
a. majina ya wanyama na ndege wa nyumbani na porini.
b. faida za wanyama na ndege.
c. vikembe mbalimbali.
d. kusoma na kujadili makala yanayohusu sifa za wanyama na ndege.
e. matumizi ya vivumishi vimilikishi katika sentensi.
f. upatanishi wa kisarufi wa ngeli ya A–WA katika sentensi.
g. kuandika insha ya mwongozo kwa kufasiri michoro kuhusu wanyama na faida zao.