• LOGIN
  • No products in the cart.

LSC S2: Mwili wa Binadamu

Utangulizi Mwili wa binadamu umejengwa kwa viungo mbalimbali ambavyo hushiriki katika kufanya kazi pamoja ili mtu aweze kuwa na maisha mazuri. Je! Ni sehemu za mwili zipi unazojua za ndani na za nje? Mada hii itakuwezesha kutambua sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu na umuhimu wake. Pia utaweza kutumia msamiati unaohusiana na mwili wa binadamu katika mawasiliano yako ya kila siku.

Utangulizi
Mwili wa binadamu umejengwa kwa viungo mbalimbali ambavyo hushiriki katika kufanya kazi pamoja ili mtu aweze kuwa na maisha mazuri. Je! Ni sehemu za mwili zipi unazojua za ndani na za nje? Mada hii itakuwezesha kutambua sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu na umuhimu wake. Pia utaweza kutumia msamiati unaohusiana na mwili wa binadamu katika mawasiliano yako ya kila siku.

Sehemu za nje za mwili wa binadamu
Stadi: Kuzungumza, kusikiliza na kuandika
Shughuli 9.1: Kutambua sehemu za nje za mwili wa binadamu.
Katika makundi madogo, shirikiana katika kufanya utafiti, kujadili, kuchora na kuonyesha sehemu mbalimbali za nje za mwili wabinadamu.

Hebu tuzungumze
igua kwa kutaja sehemu za mwili wako.Imba kwa kushika “Chemu za mwi’i wako
Kjchwa mabega magoti vidole x3
Mwi/i mzirna kwa Mungu.
Funzo b:
wa binadamu
Stadi: Kuzungumza na Kusikiliza
Shughuli 9.2: Kueleza umuhimu wa sehemu za nje za mwili wa
binadamu.
Katika makundi, fanyeni utafiti, jadiliana na kueleza umuhimu
wa %ehemu za rue za mwili wa binadamu.

Funzo ch:
Sehemu za ndani za mwili wa
binadamu
Stadi: Kusoma na Kuandika

  1. Sehemu za ndani za mwili wa binadamu
    Shughuli 9.3: Kutambua na kuchora sehemu za ndani za mwili
    wa binadamu.
    Katika makundi,
  2. Fanyeni utafiti na kutaja sehemu za ndani za mwili wa binadamu
    zifuatazo;
  1. Shirikiana katika kueleza umuhimu wa sehemu za ndani za mwili wa binadamu mlizotaja katika (1) hapo juu.
  2. Jaza mapengo kwa kutumia maneno yanayofaa kutoka katikaboksi ifuatayo.

(ii) Usagaji wa chakula
‘A . Stadi: Kusoma na Kuandika
Usagaji wa chakula ni mchakato wa jinsi chakula kinavyoshughulikiwa mwilini tangu kinapoingizwa
kinywani hadi kut01ewa kama kinyesi.

Ili chakula kiweze kutumika mwilini, ni lazima kivunjwevunjwe na kiwe katika hali rahisi ya kuweza
kusharabiwa na mwili. Kazi hiyo hufanywa na mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Sehemu kuu zinazohusika katika umeng’enyaji huo ni kinywa, umio , mfuko wa tumbo, ini, mfuko wa nyongo, utumbo rnwembamba, kongosho, utumbo mpana na puru halafu hutolewa nje ya mwili kupitia mkundu.

Shughuli 9.4: Kueleza mchakato wa usagaji wa chakula mwilini.
Katika makundi,

  1. Shirikiana katika kusoma na kujadiliana kuhusu mchakato wa usagaji wa chakula kama ifuatavyo.
    Kinywa ni sehemu ya kwanza kupokea chakula. Chakulakinapokuwa mdomoni, huvunjwavunjwa na kusagwa kwa menohuku mate yakisaidia kukilainisha. Mate hutoa vimeng’enyo
    ambavyo husaidia katika umeng’enyaji. Wakati chakula kikitafunwa kinywani, ulimi husaidia kugeuzageuza chakula hicho na kukiviringisha ili kuwa tonge. Ulimi pia husaidia kusukuma
    chakula kuelekea kwenye umio.
    Chakula hupitia umio na kuingia katika mfuko wa tumbo. Mfuko huo una uwezo wa kupanuka wakati unapopokea chakula na kusinyaa unapokuwa hauna chakula. Mfuko wa tumbo pia hutoa gastriki ambayo huwa na asidi ya haidrokloriki, uteute na vimeng’enya vinavyosaidia katika usagaji wa chakula. Chakula kikitoka kwenye mfuko wa tumbo, huelekea katika utumbo mwembamba. Hapo chakula hushughulikiwa na vimeng’enya ambavyo hutoka kwenye kongosho na utumbo mwembamba. Vimeng’enya hivyo husaidia kuyeyusha chakula. Kiasi kikubwa cha chakula humeng’enywa na kusharabiwa mwilini katika

utumbo mwembamba. Chakula kilichobaki, huelekea kwenye utumbo mpana.
Katika utumbo mpana, ni kiasi kidogo tu cha chakula ambachohusharabiwa. Sehemu kubwa ya maji iliyotokana na mmeng’enyo wa chakula husharabiwa pia katika utumbo mpana, Mwishowe,
mabaki ya chakula huelekea kwenye puru na kutolewa nje kupitia mkundu kama kinyesi.

2.Tafuteni maneno mapya kutokana na makala, kisha tumieni kamusi kueleza na kuandika maana ya maneno hayo.
3 Shirikiana katika kujibu maswali yafuatayo;
(i) Taja kwa utaratibu angalau sehemu sita ambazo zinashirikikatika umeng’enyaji wa chakula.
(ii) Eleza kinachotendeka kinywani kuhusu mchakato wa umeng’enyaji wa chakula.
(iii) Simulia kimdomo kuhusu mchakato wa usagaji wa chakula.

Kazi ya ziada

  1. Shirikiana katika kujadiliana na kujaza mraba huu.

Kulia

  1. Sehemu ya nyuma ya wayo wa mguu iliyo ngumu.
  2. Sehemu ya mwili ya nje inayotumika kupumua.

3.Hali ya ulimi kutambua kama chakula ni kitamu au chungu ni ku…. ….
4 Sehemu ya mwili inayotumika kutafuna chakula.
5 Sehemu ya mwili iliyofunikwa na nywele na hutumika kubeba vitu.
5 Hutumiwa na mama kunyonyesha mtoto.
6 Sehemu ya mwili inayotumika kusikia sauti mbalimbali.

Chini
8. Sehemu ya mguu inayotumika kukanyaga chini.
9.Sehemu ya mwili inayotumika kuona.
10.Sehemu ya mwili inayosaga na kumengienya chakula.
11.Pua inatambua kunukia na kunuka kwa vitu mbalimbali.
Kwa hivyo, kazi ya pua ni ku…
12. Sehemu ya mwili wa binadamu inayotumika kufanya kazi.
13. Sehemu ya mwili inayounganisha kichwa na kiwiliwili.
amu ananitumia wakati wa kukaa.

Msamiati wa Ulemavu
Funzo d: Ulemavu ni hali ya mtu kuwa na hitilafu ya kudumu mwilini au akilini ambayo humwekea mipaka asiweze kutekeleza shughuli fulani katika maisha yake, tofauti na watu wengine. Kwa hivyo, mlemavu ni mtu aliye na upungufu wa kiungo auviungo fulani vya mwili. Hata hivyo, ulemavu pia unaweza kuwa
wa ngozi. Mtu anaweza kuzaliwa akiwa mlemavu au ulemavu unaweza kusababishwa na ajali au ugonjwa.

Staci: Kusoma na Kuandika
Shughuli 9.5: Kubainisha msamiati wa ulemavu.
Katika makundi,
Imla

  1. Mmsikilize mwalimu wenu kwa makini, atawapa zoezi la imla kuhusu maneno yanayohusiana na ulemavu. Yaandike kwa kuzingatia tahajia sahihi, kisha tumieni kamusi kueleza na kuandika maana ya maneno hayo.
  1. Shirikiana na wenzako kujadiliana na kujaza mraba kwa kutumia msamiati wa ulemavu mliojadili katika (1) hapo juu.

Kulia

  1. Aliye na shida ya kutamka maneno wakati wa kuzungumza.
  2. Mtu aliyelemaa.
    3.Kifaa cha kukalia.
    Chini
    1.Kifaa cha kukalia.
    2 Mtu ambaye masikio yake hayasikii.
    3 Mtu aliyelemaa mguu wake.
    4 Mtu ambaye hawezi kuongea hata kidogo.
    5 Aliyelemaa kabisa na hawezi kutembea wala kutumia
    mikono yake.

Shairi kuhusu Ulemavu
Funzo e:
Stadi: Kusikiliza na Kusema
Shughuli 9.6: Kusoma na kukariri shairi.
Katika makundi madogo,

  1. Shirikiana katika kusoma na kukariri shairi lifuatalo na kisha kujadili ujumbe unaopatikana katika shairi hilo.

Ulemavu si upungufu
Nakiri ni hitilafu, tofauti kwa wengine,
Pengine ninalemewa, kuteke/eza kinyie,
Mungu wako ndiye wangu, uhai twaenda sare,
Ulemavu si kikwazo, cha kutoshiriki kazi
Elimu tuko pamoja, diguri sote twawinda,
Ubaguzi sitaraji, kwako wewe ndugu yangu,
Ushirikiano tele, faraja tupeaneni,
U/emavu si kikwazo, cha kutoshiriki kazi.
Kazi nyingi twashiriki, biashara tuko sote,
Michezo na burudani, hata paralimpikini,
O/impiki za kipeke, na za wasiosikia,
Ulemavu si kikwazo, cha kutoshiriki kazi.
Haki zetu zaju/ika, nchini na duniani,
Mabungeni twaki/ishwa, katiba twaitetea,
Nchi sote twaijenga, ni zaidi ya mmoja,
Ulemavu si kikwazo, cha kutoshiriki kazi.

2.Jadiliana kisha mshirikiane kujibu maswali yafuatayo;
(i) Shairi hili linahusu nini?
(ii)Shairi hili lina beti ngapi?
(iii)Andika mstari unaojirudiarudia katika kila ubeti.
(iv)Ubeti wa tatu unazungumzia nini? Fafanua katika lugha ya
kawaida.
(v)Mshairi anahimiza nini katika ubeti wa pili? Fafanua katika lugha ya kawaida.

Sarufi
Funzo f:
(i) Ngeli ya Li-Ya
Stadi: Kusoma na Kuandika
Shughuli 9.7: Kutambua nomino za ngeli ya li-ya zinazotaja
sehemu za mwili na kuzitumia katika sentensi.

Katika makundi,
I. Someni na kuandika wingi wa nomino za ngeii ya li-ya zifuatazo.

2.(a) Kwa kurejelea matumizi ya vimilikishi vya ngeli ya li-ya,shirikiana katika kutunga sentensi tano katika umoja na wingi kwa kutumia baadhi ya nomino mlizojadili katika (1 )
hapo juu.
(b) Kwa kurejelea matumizi ya vionyeshi vya ngeli ya li-ya, shirikiana katika kutunga sentensi tano katika umoja na wingi kwa kurejelea nomino zizo hizo.

(ii) Ngeli ya Ki-Vi
Kusoma na Kuandika
Shughuli 9.8: Kutambua nomino za ngeli ya ki-vi zinazotaja
sehemu za mwili na kuzitumia katika sentensi.

Katika makundi,
I. Someni na kuandika wingi wa nomino za ngeli ya ki-vi zifuatazo.

  1. (a) Kwa kurejelea matumizi ya vimilikishi vya ngeli ya Ki-Vi,elekezana katika kutunga sentensi tano katika umoja na wingi kwa kutumia baadhi ya nomino mlizojadili katika (1)
    hapo juu.
    (b) Kwa kurejelea matumizi ya vionyeshi vya ngeli ya Ki-Vi, shirikiana katika kutunga sentensi tano katika umoja na wingi kwa kutumia nomino zizo hizo.

(iii) Ngeli ya u-i
Kusoma na Kuandika
Shughuli 9.9: Kutambua nomino za ngeli ya u-i zinazotaja sehemu
za mwili na kuzitumia katika sentensi.

Katika makundi,

  1. Someni na kuandika wingi wa baadhi ya nomino za ngeli ya u-i
    zifuatazo.
  1. (a) Kwa kurejelea matumizi ya vimilikishi vya ngeli ya 0-1, shirikiana katika kutunga sentensi tano katika umoja na wingi kwa kutumia baadhi ya nomino rnlizojadiii katika (1)
    hapo juu.
  2. (b) Kwa kurejelea matumizi ya vionyeshi vya ngeli ya U-l, shirikiana katika kutunga sentensi tano katika umoja na wingi kwa kutumia baadhi ya nomino hizo.

3.
Shirikiana katika kuandika sentensi zifuatazo kwa wingi
(i) Kwa nini mdomo wake huo unatetemeka?
(ii)Kisogo chake kinafanana na cha baba yake.
(iii)Mguu huu umepakwa dawa leo.
(iv)Paja lake lile lilivunjika. Amelifunga kwa bendeji.
(v)Mgongo wake una vijipele.

Funzo g: Viwakilishi vya nafsi
Stadi: Kusoma na Kuandika
Shughuli 9.10: Kutaja viwakilishi vya nafsi katika umoja na wingi
na kuvitumia katika kutunga sentensi.
Katika makundi,

  1. Someni na kujadiliana kuhusu matumizi ya viwakilishi vya nafsi katika sentensi.

(i) Viwakilishi vya nafsi huru

Hivi ni viwakilishi ambavyo hujisimamia bila kuambatanishwa na
neno au mzizi wa neno jingine.

(ii) Viwakilishi vya nafsi viambata
Haya ni maneno au vipande vya maneno vinavyoambatanishw katika mzizi au neno jingine ili kudokeza nafsi inayohusika. Mfano;

3.Shirikiana katika kuandika wingi wa sentensi zifuatazo;
(i) Yeye anafikiri kwamba mimi ni mjinga.
(ii)Mimi nitakunywa soda halafu wewe utakunywa maji.
(iii)Nikija shuleni kesho, utapata pesa.
(iv)Timu yangu ikicheza vibaya, mimi ndiye ninaumia.
(v)Wewe ni mkulima, yeye ni mpishi na mimi ni mwanafunzi.

Fasihi simulizi: hadithi fupi

Stadi: Kusikiliza na Kuzungumza
Shughuli 9.11: Kubuni hadithi fupi.
Katika makundi,

  1. Shirikiana katika kubuni na kusimulia hadithi fupi za kusisimua
    kuhusu sehemu za mwili wa binadamu au hadithi yoyote ambayo
    mtaweza kubuni.
    Kuandika Insha
    Funzo i:
  2. Stadi: Kuandika
    Shughuli 9.12: Kuandika insha kuhusu namna ya kudumisha usafi.
    Katika makundi,
    Shirikiana katika kuandika insha mkieleza kuhusu jinsi mnavyodumisha na kuendeleza usafi wa miili enu.

Mfano wa Shughuli jumlishi: Baadhi ya watu, hawatambui jinsi ya kutunza na kudumisha
usafi wa sehemu za miili yao. Shuleni, wewe umefundishwa kuhusu sehemu za mwili wa binadamu na jinsi ya kudumisha usafi wa mwili wako. Andika insha kuhusu jinsi sehemu za mwili wako za nje na za ndani zinavyosaidiana kufanya kazi mbalimbali ili uwe na maisha mazuri.

Muhtasari wa mafunzo ya mada
Katika mada hii, umejifunza,
Kutambua sehemu za nje za mwili wa binadamu.
Kueleza umuhimu wa sehemu za nje za mwili wa binadamu.
Kutambua na kuchora sehemu za ndani za mwili wa binadamu
na kueleza mchakato wa usagaji wa chakula.
Kubainisha msamiati wa ulemavu.
Kusoma na kukariri shairi kuhusu sehemu za mwili.
Kutunga sentensi za upatanisho wa kisarufi wa ngeli za LI-YA,
KI-VI, na U-l zinazotaja sehemu za mwili.
Kutaja na kutumia viwakilishi vya nafsi katika kutunga sentensi.
Kubuni hadithi
Kuandika insha.

Assignment

Kuandika insha:Mwili wa Binadamu

ASSIGNMENT : Kuandika insha:Mwili wa Binadamu MARKS : 10  DURATION : 1 week, 3 days

 

Courses

Featured Downloads