To provide the best experiences, we use technologies like cookies to store and/or access device information. Consenting to these technologies will allow us to process data such as browsing behavior or unique IDs on this site. Not consenting or withdrawing consent, may adversely affect certain features and functions.
The technical storage or access is strictly necessary for the legitimate purpose of enabling the use of a specific service explicitly requested by the subscriber or user, or for the sole purpose of carrying out the transmission of a communication over an electronic communications network.
The technical storage or access is necessary for the legitimate purpose of storing preferences that are not requested by the subscriber or user.
The technical storage or access that is used exclusively for statistical purposes.
The technical storage or access that is used exclusively for anonymous statistical purposes. Without a subpoena, voluntary compliance on the part of your Internet Service Provider, or additional records from a third party, information stored or retrieved for this purpose alone cannot usually be used to identify you.
The technical storage or access is required to create user profiles to send advertising, or to track the user on a website or across several websites for similar marketing purposes.
Utangulizi
Je! Unafikiri kwa nini ni muhimu watu kujuliana hali? Je! Ni matendo gani yanayotendwa na watu wenye adabu katika jamii? Mada hii itakuwezesha kutambua salamu mbalimbali na wakati mwafaka napotumika. Pia utaweza kuthamini umuhimu wa kujuliana hali katika jamii. Katika mada hii pia utajifunza mambo na vitendo vya adabu ambavyo vinafaa kutumika au kufanyika kila siku vinavyotimiza matakwa ya jamii
Msamiati wa ziada wa salamu
Stadi: Kusikiliza na Kuzungumza
Shughuli 4.1: Kutambua msamiati wa ziada wa salamu.
Katika makundi,
Tazameni, someni na kuigiza salamu katika michoro ifuatayo;
Kuigiza Salamu
Funzo b:
Stadi: Kusikiliza na Kuzungumza
Shughuli 4.2: Kuigiza, kuanzisha na kuitikia salamu kwa namna
inayostahili.
Katika makundi,
Maneno ya adabu
Funzo ch:
Stadi: Kusoma na Kuandika
Shughuli 4.3: Kutambua na kuigiza maneno ya adabu.
Katika makundi,
Imla
I. Mwalimu atawapa zoezi la imla. Atawasomea maneno mbalimbali yanayohusu adabu. Mmsikilize kwa makini na myaandike kwa kuzingatia tahajia sahihi. Tumieni kamusi kueleza na kuandika maana ya maneno hayo.
ZingatiaAdabu ni hali ya mtu kuwa mwema, muungwana na
2. kutenda mambo yanayokubalika katika jamii. Kwa hivyo,maneno ya adabu ni yale matamko yanayodhihirisha wema na uungwana wa mtu pamoja na heshima miongoni mwa wanajamii.
Shirikiana katika kujadiliana kuhusu mnachoona na kinachotendeka katika mchoro huu.
(a) Mazungumzo haya yanahusu watu wangapi?
(b)Ni nani alimpa Atubo barua ya Mzee Cherotwo?
(c)Barua ilihusu nini?
(d)Mkutano ungekuwa wa saa ngapi tena ungetokea wapi?
(e)Jazeni majibu ya maneno ya adabu yafuatayo;
(i) pole——————–
(ii) asante—————-
(iii) alamsiki_——————-
(3) hapo juu.
Funzo d:Ufahamu: Salamu na Adabu
Stadi: Kusoma na Kuandika
Shughuli 4.4: Kutambua na kuigiza maneno ya adabu.
Katika makundi,
ifuatayo;
Salamu ni wajibu
Atweeta alikuwa mtoto mjeuri shuleni tena mwenye kiburi. Kuna baadhi ya siku ambazo hakupenda kusalimia au kusalimiwa. Wenzake wengemsalimia na angeendelea kuwatazama kama sanamu huku mikono ikiwa mifukoni. Kwa sababu hiyo, hakuwa na rafiki yeyote shuleni. Walimu na wazazi walimwonya Atweeta kuhusu tabia hii mbaya, lakini ni kama masikioni mwake mlikuwa na pamba. Siku moja, Atweeta alitumwa na mama yake kupeleka pesa kwa nyanyake. Kwa bahati mbaya, gari lilimpitisha kwenye stendi
ambako angeshukia. Machozi yalianza kumlengalenga alipotoka garini. Hakuwa na la kufanya ila tu kuanza kulialia. Aliamua kuuliza kuhusu namna ya kurudi katika kijiji kinachoitwa Kamdini alikoishi nyanyake.
Atweeta alitambua kuwa kila aliyeuliza, alikuwa hamsaidii. Wasiwasi na uoga ulianza kumwingia. Jioni ilikuwa imeingia. Machozi yakaanza kumtoka njia mbili mbili. Mara, kukajitokeza mwanamke mmoja aliyekuwa amebeba mtoto mgongoni huku akisukuma baiskeli. Atweeta akaamua kujifanya mtoto mzuri.
Kwa mara ya kwanza, Atweeta aligundua kuwa salamu ni wajibu. Tangu siku hiyo, Atweeta alibadilika na kuwa mtoto mzuri, tena mwenye adabu! Ni muungwana na mwenye kujali wenzake.
(i) Eleza kwa nini Atweeta hakuwa na rafiki yeyote shuleni?
(ii) Unafikiri ni kwa nini Bi. Awino alikataa kumsaidia Atweeta?
(iii) Elezea jinsi Atweeta alivyosaidiwa na kufika kwa nyanya
vake.
(b) Chagua neno moja kutoka mabanoni kujibu maswali yafuatayo;
(tabia, kiburi, sanamu, hakusikia)
(iii) Atweeta hakuwa na marafiki shuleni kwasababu alikuwa na————–
mbaya.
(iv) Inasemekana kuwa Atweeta aliposalimiwa na watu,
angebaki akiwatazama tu kama———————–
Shirikiana katika kuigiza hadithi ya Atweeta.
Sarufi Ngeli ya a-wa
Funzo e:Stadi: Kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika
Ngeli ya a-wa, huzingatia nomino zinazotumia kiambishi cha umoja ‘a’ katika umoja na ‘wa’ katika wingi.
Nomino zote za ngeli hii hutumia upatanisho wa kisarufi unaofanana. Hii ni ngeli ya nomino za watu, wanyama, ndege, wadudu, samaki n.k.
Shughuli 4.5: Kutambua nomino katika ngeli ya a-wa na kuzitumia
kutunga sentensi.
I. Fanyeni utafiti na kuandika nomino zisizopungua kumi za ngeli
ya a-wa katika umoja na wingi.
a) Upatanisho wa kisarufi kwa matumizi ya vimilikishi naviwakilishi
b) Upatanisho wa kisarufi kwa matumizi ya vionyeshi na vivumishi
4 Shirikiana na wenzako katika kutunga sentensi tano zeny
maana katika umoja na wingi kutokana na jedwali mlilojadili
hapo juu.
5 Andikeni sentensi zifuatazo katika wingi.
(i)Msichana huyu alisalimia mvulana yule.
(ii)Mtoto wangu huyu anatabasamu kila mara.
(iiii)Simba anatembea msituni.
(iv)Kiongozi wako atafika hapa saa ngapi?
(v) Mpishi yule anajua kupika nyama vizuri.
Funzo e: Ngeli ya i-zi
Stadi: Kusoma na Kuandika
Shughuli 4.6: Kutambua matumizi ya nomino za ngeli ya i-zi katika
sentensi.
Katika makundi,
I (a) Shirikiana katika kutazama na kujadlilana kuhusu mnachoona
katika michoro.
(b) Tunga sentensi yoyote kuhusu kila mchoro katika sehemu
ya umoja na ya wtngi.
2.
3.
Hebu tuzungumze
Ulijifunza matumizl ya nomino za Ngell ya i-zi katika kidato cha kwanza, katlka mada ya sita. Unaweza kukumbuka na kutaja angalau nomtno zatdl ya tano za ngeli ya i-zi?
2 Shirikiana katika kufanya utafiti na kuandlka angalau nomino zaidi ya kumi za ngeli ya i-zi katika umoja na wingi.
3 Kwa kurejelea upatanisho wa kisarufi wa ngeii ya i-zi, shirikiana katika kutunga angaiau sentensi kumi katika umoja na Wingi mkitumia nomino mlizoandika katika (2) hapo juu.
Viwakilishi vya nafsi
Funzo f:
Stadi: Kusoma na Kuandika
Shughuli 4.7: Kutaja viwakilishi vya nafsi vya umoja na wingl kuvitumia katjka sentensi.
Katika makundi,
I. Shirikiana katika kusoma na kuigiza kinachotendeka katika kila mchoro.
Viwakilishi hivi hutumika kwa niaba ya nafsi katika umoja
Zingatia
na wingi.
(i) Yeye anafikiri kwamba mimi sijui kuzungumza Kiswahili.
(ii) Mimi nitakula nyama halafu wewe utakula maharagwe.
(iii) Nyinyi ni waislamu na Sisi ni wakristo.
(iv) Wao wamekataa kusoma, nyinyi someni vitabu vyenu,
msiwe kama wao!
(i)Mimi nitakaa darasani.
(ii)Wewe ni mwanafunzi mchoyo.
(iii)Yeye hawezi kutoroka leo.
(iv)Mimi nilifikiri kuwa yeye hataki chakula.
(v)Wewe utarudi nyumbani saa ngapi?
Funzo g:Fasihi simulizi (Nyimbo)
Stadi: Kusikiliza na Kuzungumza
Shughuli 4.8: Kukariri na kuimba wimbo wa salamu na adabu.
Katika makundi,
nyimbo zifuatazo;
Tunakukaribisha Mwa/imu.
Habari ya asubuhi mwalimu x2
Habari ya asubuhi x2
Habari ya asubuhi mwa/imu.
Shikamoo mwalimu shikamoo! X2
Shikamoo mwa/imu x2
Shikamoo mwalimu shikamoo!
Wimbo. 2
Kumekucha nalutahi. wanvi nn•vasa/itnu,
Shikatnoo tnanta yangu, S/’lkatnoo baha yangu
Ndugu zangu hatnjatnbo ? tnwatnbajo hali ya matnbo ?
Sisi hall sjyo tnbaya, tu wazima hatujatnbo!
Watu wote sal/tnia. hali zao unjue,
Kuweni watu wazuri, adabu ni uungwana,
O/isini darasani, siingio ovyo ovyo!
Bisha hodi hodi humu, ili ruhusa upewe.
Kushukuru si kigumu, ni kusema tu asante,
Huruma na kuliwaza, pole ndiyo dawa yako,
Kutnlaki ni karibu, Kwa heri ndiyo kumwaga,
Kuweni watu wazuri, Adabu ni uungwana.
Wimbo 3
Asante x2
Asante mwa/imu Kutu/undisha x2
Kwaheri x2
Kwaheri mwa/imu Tutaonana x2
Na Resho x2
Na Resho mwalimu — Tutaonana x2
unaoupenda na kisha uuimbe darasani.
Kuandika Insha
Funzo h:
Stadi: Kusikiliza, kuzungumza, kusoma na Kuandika
Shughuli 4.9: Kuandika insha
Katika makundi, Jadiliana kuhusu vitendo vya adabu katika
michoro na kisha mshirikiane kuandika insha kwa kuongozwa na
vitendo hivyo. Insha yako inatangulizwa na sentensi, “Mwanafunzi
mwenye adabu anastahili———————————-
Rafiki yako aliyekutembelea wikiendi iliyopita, wazazi wako walisema kuwa ni mtoto mwenye adabu.
Andika insha juu ya rafiki yako, ukimsifu kwa kurejelea salamu.vitendo na maneno ya adabu anayotumia kila Siku. Muhtasari wa malunzo ya mada Katika mada hii, umejifunza,
Kutambua msamiati wa ziada wa salamu.
Kuanzisha na kuitikia salamu kwa namna inayostahili.
Kutambua na kuigiza maneno ya adabu ya ziada.
Kuigiza na kusoma mazungumzo,
Kutambua matumizi ya upatanisho wa kisarufi wa nomino za
a-wa na i-zi.
Kutaja viwakilishi vya nafsi katika umoja na wingi na kuvitumia
katika sentensi.
Kukariri na kuimba wimbo wa salamu na adabu.
Kueleza hatua mwafaka za uandishi wa insha.
Kuandika insha kuhusu vitendo vya adabu.
Assignment
ASSIGNMENT : Kuandika insha :Salamu na Adabu MARKS : 10 DURATION : 1 week, 3 days