• LOGIN
  • No products in the cart.

Rangi Mbalimbali

Rangi Mbalimbali

Utangulizi
Rangi hupendeza katika macho ya kila mtu. Rangi zinapatikana kokote, wakati wowote na kila mtu anayo rangi inayompendeza. Je, wewe unapendezwa na rangi gani? Nguo ambazo unapenda kuvaa ni za rangi gani? Ukitazama katika mazingira yaliyokuzunguka sasa hivi, unaweza kutaja rangi ngapi ambazo
unaona katika mazingira hayo? Katika mada hii, utatambua majina ya rangi na msamiati mwingine unaohusiana na rangi na kuutumia kutunga sentensi na kuimarisha mawasiliano yako.
Stadi za Lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo a: Kutambua msamiati wa rangi mbalimbali na kueleza maana yake

Utangulizi
Kuna misamiati kadhaa inayotumiwa kurejelea rangi au kueleza juu ya rangi. Mada ndogo hii itakusaidia kukuza msamiati unaohusiana na rangi.

Kutaja na kufafanua maana za rangi mbalimbali
i) Kutaja rangi mbalimbali

  1. Tazama rangi hizi na kutambua majina yake

2.Katika vikundi, nendeni katika mazingira yenu ya Shule na kutafuta
rangi za vitu ambavyo mtakutana navyo. Mkirudi darasani, onyesheni
vitu mlivyokutana navyo na kutaja rangi ya kila kitu.
3.Kila mwanafunzi atunge sentensi kwa kutumia rangi yoyote anayopenda
4.Kwa kutumia mtandao, tambua rangi mbalimbali na majina yake (unaweza pia kucheza mchezo wa rangi uliomo katika mtandao ukitumia tarakilishi au simu ya mkononi.

Taz: Umejifunza kuwa kuna rangi mbalimbali na kila rangi huwa na maana iliyojisetiri ndani mwake. Kwa mfano rangi ya Waridi ni ya mapenzi. Pia umetambua kuwa kila mtu anapenda rangi yake.

Kufafanua Maana ya rangi tofauti tofauti
Katika jamii mbalimbali, baadhi ya rangi Zina maana ambazo zinatambulika na kuthaminiwa. Kwa mfano, nchini Uganda, rangi ya manjano husimamia jua. Je, kuna rangi nyingine zenye maana unazojua? Sehemu hii ya mada, itakuwezesha kueleza maana za rangi mbalimbali.

  1. Katika vikundi, tambueni rangi zenye maana mnazojua na kisha elezeni maana ya kila rangi mliyotambua.
  2. Mkitumia mtandao, tambueni nembo angalau mbili za nchi zilizomo katika muungano wa Jumuiya Mashariki na kueleza maana za rangi zilikoko kwenye nembo hizo.

Taz: Umejifunza kuwa ulimwengu una rangi nyingi sana. Pia umetambua kuwa

ukiingia katika mtandao unaweza kujifunza na hata kucheza mchezo wa rangi na kuweza kutambua zaidi kuhusu rangi mbalimbali ni jinsi zinavyotumika katika mavazi, nembo, bendera na hata vitu vinginevyo.
Stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika

Funzo b: Kubaini rangi tofauti za upinde wa mvua
Utangulizi
Je, umewahi kuona upinde wa mvua au hata kuimba wimbo juu ya upinde wa mvua? Unaweza kutambua idadi ya rangi na kupangilia rangi hizo? Katika mada hii, utajifunza juu ya upinde wa mvua na kutambua rangi zake kwa mpangilio.
Shughuli 9.2
Kutambua rangi za upinde wa mvua
i) Kutaja rangi mbalimbali

  1. Katika vikundi, tazameni picha ya upinde wa mvua na kutambua majina ya rangi ulio nazo.
  1. Choreni upinde wa mvua kwenye Chati na kuuwasilisha mbele ya darasa
  2. Tambueni rangi zinazopatikana katika upinde wa mvua.
  3. Kwa kutumia mazingira yako, tambua majani ya miti na matunda ambayo yana rangi za upinde wa mvua katika makundi ya watu saba. Taz: Umejifunza kuwa upinde wa mvua una rangi saba zinazopendeza na zenye mpangilio maalumu. Upinde hutokea hasa kunapokuwepo manyunyu ya mvua pamoja na jua. Kila jamii ina miiko na mila zinazoelezea juu ya rangi za upinde wa mvua na utokeaji wake. Kuna wanaouona na kusema kuwa kuna hatari ya njaa, wengine hudai kuwa unaashiria kifo, na hata wengine wanauabudu kuwa baraka na wengi wanadia kuwa upinde hunyonya damu za watu na kadhalika. Stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika

Funzo c: Kutambua rangi zilizo katika taa za barabaran na kueleza maana ya rangi hizo
Utangulizi

Nafikiri umekuwa ukitembea ama kwa miguu au kwa magari. Kuna mahali hasa mijini penye njia panda ambapo unakuta taa za kuchunga utaratibu wa kupita kwenye njia panda hiyo. Je, umewahi kuhesabu idadi ya taa hizo? Unajua rangi zote zilizoko kwenye taa hizo? Unajua maana ya kila rangi ya taa? Mada ndogo hii itakuwezesha kueleza maana ya rangi za taa za barabarani.

I.intaneti
Kutaja rangi za taa za barabarani na kueleza maana
Shughuli 9.3

ya kila rangi
Tazama picha ya taa za barabarani iliyopo hapo juu na kutambua rangi zilizoko.
Katika makundi, jadiliana juu ya ishara au maana ya rangi hizo zinapojitokeza.
Elezeni maana ya rangi hizo za taa za barabarani.
4.Fikiria kuwa unaendesha gari lako. Kufika kwenye njia panda unakuta kuna taa ya rangi ya kijani, utafanya nini?
5.Elezeni ni lini dereva anatakikana kupita au kusimama au kujitayarisha kupita.
Taz: Umetambua kuwa rangi za barabarani ni muhimu sana. Inafaa unapotembea, kuendesha gari na hata kuvuka katika vifuko vya barabara, kuwa makini kutambua rangi na maana yake. Aidha, usipishane na magari bali kuwa mvumilivu, subiri taa na kufuata maagizo ili kulinda usalama wa barabarani.

Stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na uandika
Funzo d: Kutambua rangi zilizo katika bendera ya taifa na kueleza maana ya rangi hizo
Utangulizi

Bendera ya taifa la Uganda inapendeza sana. Ina rangi ambazo tunajivunia. Je, unafahamu rangi za
bendera ya taifa la Uganda? Unaweza kutambua rangi hizo na maana ya kila rangi?
Mtandao wa intaneti

Katika mada ndogo hii, utajifunza rangi za bendera ya Uganda na maana ya kila rangi kwenye bendera
hiyo.

kutambua rangi za bendera na maana zake
Shughuli 9.4

1.Kila mwanafunzi achore bendera ya Uganda katika kitabu chake.
2.Tazama picha ya bendera na kutambua rangi zinazopatikana.
3.Katika vikundi, elezeni maana ya kila rangi ya bendera ya Uganda.
4.Ni rangi gani unayopenda katika bendera na kwa sababu gani?
Taz: Umejifunza kuwa rangi za bendera ya Uganda ni muhimu sana. Rangi hizi huelezea historia ya nchi yetu, mazingira yetu, rangi yetu na uzalendo wetu. Ni kitambulisho cha nchi yako ambayo unajivunia. Ni muhimu
kuithamini, kuijali, kuwajibika na kuheshimu bendera yako kuonyesha umoja na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu kulinda nchi yako.

Stadi za Lugha: Kusoma
Funzo e: Kusoma makala na kujibu maswali

Shughuli 9.5
Kusoma makala kuhusu usalama barabarani

1.Someni Makala haya kwa makini na kutambua ujumbe uliomo. Asilimia kubwa ya ajali mbaya barabarani inatokana na matumizi mabaya ya barabara. Tabia za waendeshaji magari barabarani, magari mabov,

kutozingatia kanuni na sheria, ulevi, kutowajali watumiaji wengine barabarani, uzembe, kutozingatia alama za barabarani na kukosa uzalendo. Idara ya masuala ya usalama na uchukuzi nchini inaeleza kuwa
watumiaji wa barabara wanastahili kuzingatia kanuni na sheria za matumzi ya barabarani ili kuhakikisha kuwa wanasafiri salama. Katika uchunguzi wao, walitambua kuwa aghalabu kila ajali zinazotokea
barabarani zinaweza kuepukika. Wanaeleza kuwa ajali mara nyingi hutokea kwa sababu ya kutojali kwa madereva.
Kama wahenga walivyonena kuwa, “tahadhari kabla ya hatari,” Polisi wanaohusika na usalama barabarani wameweka mikakati mingi kuhakikisha kuwa kuna usalama barabarani. Miongoni mwa mikakati hii ni kuhakikisha kuwa abiria wanaosafiri wanajifunga mishipi wanaposafiri. Wanaamini kuwa
hata gari likipatwa na shida, wana uwezo wa kuweza kuokoa maisha yao. Aidha magari yote yamelazimishwa na idara ya uchukuzi kuhakikisha kuwa wameweka vidhibiti mwendo kuhakikisha kuwa gari haliendeshwi kwa kasi kupindukia na kusababisha ajali.

Aidha, idara hii imehakikisha kuwa wanakandarasi wanaojenga barabara wanaweka alama za barabarani kutoa taarifia ya hali ya barabara kwa watumiaji. Alama hizi ni michoro ya alama za barabarani iliyopo kwenye mabango ambayo huwekwa pembezoni mwa barabara au kwenye maeneo
yanayozunguka barabara kutoa habari ya matumizi sahihi ya barabara. Alama hizi ni za aina nyingi. Kuna alama za kudhibiti magari kama vile simama, hakuna kuingia, pita kulia, mbele panda kulia au kushoto, kuna ng’ombe mbele na kadhalika. Vilevile kuna alama za tahadhari, alama za taarifa, alama za kuongoza na kadhalika. Ni muhimu watumiaji kujali na kuzingatia alama hizi ili kuzuia ajali barabarani.
Kwa ajili ya kuwaadhibu wavunjaji sheria, mamlaka ya usalama wa barabarani na uchukuzi pamoja na polisi wa usalama barabarani wameweka mikakati ya kuhakikisha kuwa kuna kufika salama. Miongoni mwa mikakati hiyo ni kuweka vizuizi barabarani vya fika salama, mabasi kuhakikisha
wanadhibiti muda wao wa kusafirisha abiria bila pupa na pia kutii taa za barabarani. Mikakati mingine ni kuyashika magari mabovu barabarani, kuwaelimisha madereva na wenye magari ya uchukuzi na usafirishaji wa abiria na kuwatoza viwango vya faini wanapopatikana na hatia ya kubeba abiria kupita kiasi. Pia, kuna kufunga walio na hatia ya kuunja sheria na kufutilia mbali liseni magari yanayofanya ajali kila mara. Kumbuka methali ya wahenga kuwa mwenda pole hajikwai.

Aidha watumiaji wa bodaboda, baiskeli na wanaotumia miguu wanaelimishwa kila ukicha kuhakikisha kuwa wanatambua alama za barabarani. Wanashauriwa kupita mahala pa mataa ya usalama
na kuzingatia sheria na kanuni za kutumia barabara. Kwa wale wasiozingatia sheria nao huadhibiwa kwa kutozwa faini pamoja na kuwaongoza kutambua matumizi bora ya barabara. Bodaboda
zimedhibitiwa na kusimamishwa kupita katika baadhi ya barabara na kuhakikisha kuwa waendeshaji wanavaa mavazi ya uslama kama kofia, buti na mavazi ya kuwasaidia kutambulika usiku na mchana.
Katiba ya nchi imehakikisha kuwa sheria zinaundwa na kutumika kwa ajili ya kudhibiti barabara ambazo ni hatari kwa ajali hasa barabara kuu kama vile Masaka -Mbararara, Tororo-Mbale, Lira Kitgumu,
Kampala Gulu, Kampala – Entebbe, Kampala-Busia, Kampala Malaba na barabarara nyinginezo.
Waendesha magari na wenye magari wamekuwa wakielimishwa kuhakikisha kuwa magari yanachunguzwa kabla ya kwenda barabarani, magari mabovu kuondolewa barabarani na hatua nyinginezo za
kuboresha barabara. Wizara ya barabara na uchukuzi pia wamekuwa wakiombwa kutengeneza barabara na kuzikarabati zingine kwa ajili ya kuzidi kudhibiti viwango vya barabara na kulinda usalama wa barabara. Aidha, ikiwa usalama utadumishwa, walevi na wanaoendesha magari wakiwa wanafanya shughuli kama vile kusoma gazeti, kula na kunywa, kuongea kwa simu wanashauriwa kutojaribu kupatikana barabarani. Madereva wanaombwa kutoendesha magari wakiwa walevi, au kula na kuongea kwa simu wakiwa wanapumzika au kuegesha magari yao. Wavunjaji wa kanuni wakipatikana, sheria ichukue kipaumbele. Wanaotaka kuzunguka mbuyu, madereva, wamiliki magari na abiria wenye kiburi wafungwe maisha na kweli usalama wa barabarani utadumu milele. Wakila kalenda, huenda usalama barabarani utadumu.

Maswali
2Katika vikundi,
a) Elezeni mambo yanayohatarisha usalama wa barabarani.
b) Tambueni idara zinazojihuisha na usalama wa barabarani.
c) Elezeni majukumu ya watumiaji barabara, abiria, dereva na wenye magari katika suala la usalama wa barabarani
d) Tambueni sababu za ajali barabarani katika jamii nyingi. Ni ushauri gani unaotoa kwa watumiaji barabara katika jamii yako?
Tambueni maneno magumu katika Makala na kutumia kamusi kutafuta
maana ya maneno hayo.

stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Funzo f: Kueleza jinsi ya kuepuka ajali Barabarani
Utangulizi

Ajali ni hali ya dharura ambayo hutokea katika maisha yetu bila kutarajia. Hata hivyo tunaweza kuepukana na hali kama hii tukiwa makini katika utekelezaji wetu. Je, umewahi kupatwa na ajali au kushuhudia ajali? Unaweza kutambua baadhi ya ajali ambazo hupatikana katika jamii zetu? Katika sehemu hii,
utajifunza juu ya jinsi ya kuepuka ajali.
Shughuli 9.6
Kueleza namna ya kuepuka ajali barabarani

  1. Katika vikundi;
    a) Elezeni sehemu mbalimbali katikajamii zetu ambapo ajali hutokea.
    b) Tambueni baadhi ya vyanzo vya ajali katika maisha yetu.
    c) Elezeni jinsi ya kuepukana na ajali barabarani kulingana na makala
  2. Pendekezeni njia mwafaka za kuepukana na ajali, mbali na zile zilizotajwa katika makala.
    Stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
    Funzo g: Sarufi -Kutunga sentensi kutumia viwakilishi
    vya ‘-a’ unganifu, viwakilishi vya pekee na vielezi vya
    mahali na wakati
    Utangulizi

‘-a’ unganifu ni kivumishi-kimilikishi kinachotumika kuonyesha uhusiano
wa nomino na maneno mengine. Je, unafahamu kuwa katika mazungumzo
yako huwa unatumia sana ‘-a’ unganifu? Je, unafahamu jinsi ‘-a’ unganifu
inavyotumika? Katika funzo hili, utajifunza matumizi ya ‘-a’ unganifu na jinsi ya
kuitumia katika sentensi.
i”) Shughuli 9.7
Kutumia ‘-a’ unganifu katika sentensi

  1. Katika vikundi, Tambueni ‘-a’ unganifu katika sentensi zifuatazo:
    a)Bendera ya Uganda inapepea ikionyesha rangi zake.
    b)Chungwa la mtoto lina rangi ya manjano.
    c)Taa za barabarani huchunga madereva na kulinda usalama.
    d)Maembe ya Palisa yana rangi ya kijani.
    e)Rangi ya bendera inapendeza

Tambueni ‘-a’ unganifu katika kila ngeli na kuandika wingi wa sentensi katika jedwali.

Katika makundi, elezeni yale mnayotambua katika matumizi ya ‘-a’ unganifu.

Taz: Umejifunza kuwa ‘-a’ unganifu hutumika kuonyesha umilikaji. Hutuelezea zaidi kuhusu nomino kwa kuonyesha kitu kinachomiliki nomino hiyo. Huundwa kwa kuambatanisha kiambishi cha nafsi/ngeli pamoja na kiambishi -a cha a-unganifu, kisha nomino.
Kutunga sentensi kutumia viwakilishi vya pekee
Utangulizi
Katika vipindi vya awali, mlijifunza juu ya vivumishi vya pekee. Je, unaweza kutambua aina mbalimbali za vivumishi vya pekee? Je, unaweza kutambua viwakilishi ambavyo hutumika kuwakilisha vivumishi vya pekee? Sehemu hii itakuwezesha kutambua vimilikishi vya pekee na kuvitumia kutunga sentensi.
1.Kutambua viwakilishi vya pekee na kuvitumia.8kutunga sentensi
Katika vikundi, tambueni viwakilishi vya pekee.
2.Tungeni sentensi kwa kutumia viwakilishi vya pekee.
3.Kila kikundi kitoe maoni yake kuhusiana na matumizi ya viwakilishi vya pekee.

umejifunza kuwa viwakilishi vya pekee ni mizizi au maneno am ayo hutumika kuwakilishia vivumishi vya pekee. Ni muhimu kwa hiyo kutambua kwa, maneno haya ni -ote na o-ote, enye, na -enyewe, -ingine na ingineo. Maneno haya huwa na maana au matumizi maalumu. Kwa mfano; Dote hutumika kuonyesha ujumla wa kitu au vitu. -o-ote kuonyesha bila kubagua au kuchagua. ‘enye hutumika kuleta maana ya umilikaji wa nomino. ‘enyewe hutumika kuisisitiza nomino fulani katika utendaji. ‘Ingine huonyesha
tofauti au zaidi ya kitu fulani. Mwisho, ‘ingineo hutumika kuonyesha ziadi. Viwakilishi hivi huchukua upatanisho wake wa kisarufi kulingana na ngeli ya nomino ambayo kinaivumisha. Kwa mazoezi zaidi pitia funzo la awali la 3.6.5. Kazi Mradi: Katika makundi, tafiti zaidi kuhusu viwakilishi vya pekee, kutunga
sentensi na kuwasilisha darasani katika kipindi kitakachofuata

Vielezi
Kutunga sentensi kutumia vielezi vya mahali
Utangulizi

Vielezi vya mahali ni vielezi ambavyo hutoa habari kuhusu mahali ambapo kitendo kilitendeka, kinatendeka au kitatendeka. Je, unaweza kutambua vielezi vya mahali?

Shughuli 9.9
Kutambua vielezi vya mahali na kuvitumia katika sentensi

  1. Katika vikundi,
    a) Tambueni kielezi cha mahali katika sentensi zifuatazo:
    i) Rangi ya manjano ilipakwa chumbani mwangu.
    ii) Mwalimu mkuu ameleta rangi ya hudhurungi shuleni.
    iii) Mpishi ameenda kununua matunda ya kibichi sokoni.
    iv) Bendera ya taifa inapepea shuleni kwetu.
    v) Waumini wa kikatoloki wameingia kanisani mapema sana.
    vi) Agume ameenda Kampala kununua rangi ya kupaka nyumba yake.
  2. Tungeni sentensi tano kuonyesha matumizi ya vielezi vya mahali.
    Taz: Umejifunza kuwa vielezi vya mahali hutumika kutaja jina la mahali au kuongeza kiambishi -ni-mwishoni mwa neno linaloashiria mahali.

Stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
Kutunga sentensi kutumia vielezi vya wakati
Utangulizi
Vielezi vya wakati huelezea zaidi kuhusu wakati ambapo kitendo kilitendeka, kinatendeka, kimetendeka au kitatendeka. Je, unajua kuwa vielezi hivi hutumiwa sana katika shughuli zako za kila siku? Unaweza kutambua vielezi hivyo?

Kwa Mfano: juzi, jana, leo, sasa, sasa hivi, kesho, keshokutwa, mtondo, mtondogoo, jioni, asubuhi, saa sita mchana, usiku, na kadhalika.
Kazi ya ziada
Ukizingatia msamiati wa rangi mbalimbali, tunga sentensi ukitumia vielezi vya wakati.

Fasihi Simulizi
stadi za Lugha: Kusikiliza na Kuzungumza
Funzo h: Kubuni shairi Kuhusu Rangi tofauti
Utangulizi
Mashairi mengi ambayo umekuwa ukisoma ni mashairi ambayo yanatokana na fikra za wandishi. Je, umewahi kutambua kuwa nyimbo zinazoimbwa hutokana na fikra za mwimbaji kutokana na mazingira yake? Je, umewahi kutunga wimbo wowote? Ni hatau gani ulizozingatia katika kuandika? Katika funzo hili
Ia kubuni shairi, utatumia tu uwezo ulio nao kutunga shairi husika.

Kutambua viwakilishi vya pekee na kuvitumia kutunga sentensi
Shughuli 9.11

I. Katika vikundi, buni shairi linalohusu rangi mbalimbali
a) Zingatieni yafuatayo:
b) Ni shairi la aina gani unalotaka kuandika (lenye vina au lisilo navyo)
c) Shairi Iitakuwa na beti ngapi?
d) Kila ubeti utakuwa na mishororo mingapi?

  1. Ujumbe unahusu rangi?
    Taz: Katika funzo hili, umejifunza kuwa katika kubuni shairi, unahitaji kuwa na ari inayokusuma pamoja na kanuni za kutambua mishororo, beti, vina, mizani, kiitikio na ujumbe.
    Stadi za Lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika
    Funzo i: Kutambua kanuni za ufupishaji
    Utangulizi

    Katika sura ya tano, ulijifunza juu ya ufupisho. Je, unaweza kutambua kanuni ambazo ulitumia katika kufupisha habari katika sura hiyo? Katika sehemu hii utatambua hatua za kufupisha makala.
    Kutambua viwakilishi vya pekee na kuvitumia
    Shughuli 9.12
    kutunga sentensi
  2. Katika vikundi, tambueni hatua ambazo unaweza kutumia kufupisha neno, sentensi, aya au kifungu cha habari.
  3. Ni mambo gani amabyo ni muhimu sana katika ufupishaji wa habari?

Taz: Umejifunza kuwa ufupishaji ni muhimu sana katika maisha. Kujieleza moja kwa moja ni muhimu sana. Habari inaweza kueleweka zaidi unapotumia mawazo mafupi yasio na maelezo marefu. Ni muhimu kwa
sababu hakuna kujirudia. Hata hivyo umejifunza kuwa katika ufupisho, ni muhimu kutambua ujumbe au wazo linalozungumziwa katika habari. Baada ya kutambua wazo kuu, unaweza kutambua hoja ambazo hujenga wazo kuu. Baada ya hapo unaweza kuunganisha mawazo hayo kwa mtiririko usiokuwa na mzunguko. Unapofupisha habari, hakikisha kuwa unazingatia urefu unaohitajika, yaani idadi ya maneno Stadi za Lugha: Kuandika Funzo Ekufupisha makala

Stadi za Lugha: Kuandika
Funzo j: kufupisha makala
Kufupisha Makala kwa maneno 1 00
Shughuli 9.13

  1. Katika makundi, jadiliana juu ya ujumbe unaojitokeza katika
    2.
    makala yafuatayo:
    Rangi hupendeza sana. Juzi nilikuwa chumbani nikaona upinde wa mvua uliokuwa na rangi za kuvuvia. Zilikuwa rangi nyekundu, chungwa, manjano, janikiwiti, samawati nili na urujuani. Nilipouliza upinde huu ulitoka wapi? Nilielezwa kuwa ulitoka mbinguni. Wengi walisema ulitoka msituni kutafuta maji katika mto wetu. Hayo yakiwa hapo, nilisikia watu wengine wakizungumzia upinde
    wa mvua eti huleta baraka. Wengine waliutoroka kwa kudai kuwa utawanyonya damu na wengi kutoroka na kufunga milango na madirisha kwa madai kuwa shetani ameinga kijijini kuwaangamiza.
    Nilishangazwa sana na imani za watu kuhusiana na miiko na desturi juu ya upinde wa mvua.
    Kilichonifurahisha zaidi ni yale madai ya mwenzangu aliyenidanganya kuwa upinde wa mvua unaonyesha damu walizo nazo watu miilini mwao. Nilipomuuliza kama amewahi kuona damu ya nili au samawati au kijanialicheka na kusema kuwa alielezwa hivyo. Baadaye alinipa hadithi kuwa
    rangi hizo zinatokana na rangi mbalimbali za mazingira ulimwenguni. Mwingine alikuwa ameniambia kuwa upinde wa mvua unatokana na miale ya jua inayopenyeza katika manyunyu ya mvua ikinyesha.
    2.Fupisheni taarifa hiyo kwa maneno 100.

Katika mada hii, umejifunza:
Rangi mbalimbali na kueleza maana yake
Rangi mbalimbali za upinde wa mvua
Rangi zilizo katika taa za barabarani na kueleza maana ya rangi hizo
Rangi zilizo kwenye bendera ya taifa na kueleza maana ya rangi hizo
Kusoma makala na kujibu maswali
Kueleza jinsi ya kuepuka ajali barabarani
Kutunga sentensi kwa kutumia a- unganifu, viwakilishi vya pekee
na vielezi vya mahali na wakati
Kubuni shairi kuhusu rangi tofauti
Kutambua kanuni za ufupishaji
Kufupisha makala

Assignment

Mfano wa Shughuli Jumlishi juu Rangi Mbalimbali

ASSIGNMENT : Mfano wa Shughuli Jumlishi juu Rangi Mbalimbali MARKS : 10  DURATION : 1 week, 3 days

 

Courses

Featured Downloads