• No products in the cart.

20

Hiki ni kitabu cha Mwanafunzi wa kidato Cha tatu kwa shule za upili nchini Uganda. Kitabu hiki kinaendeleza udhibiti wa …

FREE

Hiki ni kitabu cha Mwanafunzi wa kidato Cha tatu kwa shule za upili nchini Uganda. Kitabu hiki kinaendeleza udhibiti wa umilisi na mawasiliano kwa matumizi ya Kiswahili sanifu.
Kitabu hiki kinakuza na kuendeleza ujifunzaji na upataji wa umilisi kutoka kidato Cha kwanza na pili. Kinazidi kuweka msingi madhubiti wa kuimarisha umilisi unaomwezesha mwanafunzi kutumia Kiswahili fasaha kutokana na upanuzi wa misamiati na tajiriba za kumwezesha mwanafunzi kuwasiliana
katika miktadha mbalimbali kwa mahitaji yake ya kila siku. Kitabu hiki cha mwanafunzi kwa kidato cha tatu ni nguzo imara katika ujifunzaji wa Kiswahili sanifu. Mada za kitabu hiki zimeandaliwa kuakisi na kutosheleza mahitaji na malengo ya mtaala kwa Shule za upili nchini Uganda-Mahitaji ya mwanafunzi katika harakati na mchakato wa ujifunzaji umetiliwa maanani. Mwanafunzi amepewa uhuru wa kufikiri, kuhakiki, na kutatua matatizoya masuala ibuka ya kiuzalendo, kimazingira na kimaisha yanayomkumba
shuleni, nyumbani na katika jamii yake.Kitabu hiki ni ngao ya kujifunzia Kiswahili kwa vile kinavyoakisi na kutoshelezamalengo ya mtaala kwa Shule za upili nchini Uganda. Mahitaji ya mwanafunzikatika harakati zake za kujifunza Kiswahili yanatiliwa maanani. Mwanafunzimwenyewe atapata uwezo wa kufikiri, kuhakiki na kutatua matatizo yanayomkumba shuleni, nyumbani na katika jamii yake. Vilevile, kitabu hiki kitamsaidia mwanafunzi kupata uwezo wa ubunifu na uvumbuzi anapojifunza Kiswahili darasani. Kadhalika, mwanafunzi atapata umilisi wa mawasiliano kwa Kiswahili. Mwanafunzi atajifunza zaidi teknolojia yakisasa kwa mazoezi ya matumizi ya tarakilishi na ukokotaji. Pamoja na hayo,
mwanafunzi atazidi kujiendeleza kimaadili kwa kushirikiana na kufanya kazi pamoja na wenzake. Kwa hivyo, ni jambo muhimu kila mwanafunzi kushirikiana na wenzake darasani katika jozi au vikundi ili kuendeleza ushirikiano, uvumbuzi, usikilizaji, uongeaji na mawasiliano ili kufanikisha mkakati wa ujifunzaji Kiswahili sanifu.

Course Currilcum

  • Madawa ya Kulevya Details 1 year
  • Mfano wa Shughuli Jumlishi juu Madawa ya Kulevya 10, 00:00
  • Majanga Details 1 year
  • Mfano wa Shughuli Jumlishi JUU Majanga 10, 00:00
  • Sherehe za Kitaifa Details 1 year
  • Mfano wa Shughuli Jumlishi juu Sherehe za Kitaifa 10, 00:00
  • Haki za Kibinadamu Details 1 year
  • Mfano wa Shughuli jumlishi juuHaki za Kibinadamu 10, 00:00
  • Uongozi wa Kitaifa Details 1 year
  • Mfano wa Shughuli Jumlishi juu Uongozi wa Kitaifa 10, 00:00
  • Hali ya Anga Details 1 year
  • Mfano wa Shughuli Jumlishi juu Hali ya Anga 10, 00:00
  • Jumuiya ya Afrika Mashariki Details 1 year
  • Shughuli Jumlishi Pendekezwa juu Jumuiya ya Afrika Mashariki 10, 00:00
  • Rangi Mbalimbali Details 1 year
  • Mfano wa Shughuli Jumlishi juu Rangi Mbalimbali 10, 00:00
  • Mavazi na Mapambo Details 1 year
  • Mfano wa Shughuli Jumlishi juu Mavazi na Mapambo 10, 00:00
banner