To provide the best experiences, we use technologies like cookies to store and/or access device information. Consenting to these technologies will allow us to process data such as browsing behavior or unique IDs on this site. Not consenting or withdrawing consent, may adversely affect certain features and functions.
The technical storage or access is strictly necessary for the legitimate purpose of enabling the use of a specific service explicitly requested by the subscriber or user, or for the sole purpose of carrying out the transmission of a communication over an electronic communications network.
The technical storage or access is necessary for the legitimate purpose of storing preferences that are not requested by the subscriber or user.
The technical storage or access that is used exclusively for statistical purposes.
The technical storage or access that is used exclusively for anonymous statistical purposes. Without a subpoena, voluntary compliance on the part of your Internet Service Provider, or additional records from a third party, information stored or retrieved for this purpose alone cannot usually be used to identify you.
The technical storage or access is required to create user profiles to send advertising, or to track the user on a website or across several websites for similar marketing purposes.
Utangulizi
Je! Unaweza kuhesabu vidole vyako vyote katika Kiswahili? Ni vingapi basi? Sasa hivi ni saa ngapi? Leo ni tarehe gani? Mada hii itakuwezesha kutambua tarakimu mbalimbali katika Kiswahili na matumizi yake katika mazungumzo ya kawaida.
Funzo a: Tarakimu
Stadi: Kusikiliza, Kuzungumza na Kuandika
Shughuli 5.1: Kuhesabu tarakimu
Katika makundi,
maneno
1 .332,700
2 3 443,500
3 554.800
Funzo b: Stadi: Kusikiliza, Kuzungumza na kuandika
Shughuli 5.2: Kutambua tarakimu katika vitu mbalimbali.
Katika makundi.
Funzo ch: Alama za hesabu
Stadi: Kusoma na Kuandika
Shughuli 5.3: Kutumia alama za hesabu mbalimbali kupata matokeo mapya ya tarakimu.
Katika makundi,
I. Someni na kuladlhana kuhusu matumtzi ya atama za hesabu
zifuatazo. Tamka hesabu Vile Inawotendeka pamqa na matokeo yake.
majibu yenu katika maneno.
(i)Muhula wa kwanza ulianza lini?
(ii)Ni tarehe gani wanafunzi walipoenda likizoni ya muhula wa
(iii)Ilikuwa siku gani ya wiki wanafunzi walipofunga muhula wa
(iv)Siku ya Jumatatu tarehe nne Februari, ni nini kilitokea
shuleni?
(v)Ni muhula upi ulioisha katika mwezi wa Agosti. Uliisha
tarehe gani?
(iv)Andika muhula uliokuwa na siku nyingi zaidi shuleni. Ulianza
lini na kuisha lini?
4.
Tamkeni na kuandika tarehe zifuatazo katika maneno
1.12/4/1960
2.6/9/2023
3.22/7/2021
4.1 1-8-2024
5. 9/9/1999
Akisami
Stadi: Kusoma na Kuandika
Shughuli 5.5: Kubainisha akisami mbalimbali na kuzitumia katika
sentensi.
Katika makundi,
I. Someni na kujadiliana kuhusu akisami zifuatazo kisha jazeni mapengo kwa kuandika neno la akisami iliyoachiwa nafasi.
(a) Mama aliwagawia watoto wake watatu tikitimaji kwa usawa. Kila mmoja alipata akisami gani?
(b) Muwa wa pingili sita uligawanywa kwa watoto sita. Kila mtoto alikula akisami gani ya muwa?
Funzo f: Maumbo
Stadi: Kusikiliza. Kuzungumza na kuandika
Shughuli 5.6: Kutambua maumbo mbalimbali.
Katika makundi,
Imla
1 (a) Mwalimu atawapa zoezi la imla. Mmsikilize kwa makini akiwasomea majina ya maumbo. Yaandikeni kwa kuzingatia tahajia sahihi.
(b) Shirikiana katika kutambua maana ya majina ya maumbomliyoandika na kisha kuyaambatanisha na picha za maumbo yafuatayo;
Kukariri shairi: Matumizi ya hesabu
Funzo g:
Shughuli 5.7: Kukariri shairi na kueleza ujumbe kutokana na
shairi.
Katika makundi,
Asiyejua hesabu, amezama aibuni Ukijua kuhesabu, hakuna shida sokoni.
Pesa hautanyanganywa, bidhaa ununuapo, Safro hutodanganywa, pale baada ya malipo,
Kila tarehe najua, chaku/a kipo sifichi, Kila mwaka napakua, mwezi mei hata Machi
Tembe hospita/ini, nikipewa matibabu,
Hesabu ziko kichwani, mara tatu siyo tabu,
Akisami nafahamu, hata niwe nakoroma,
Zote hizo tarakimu, nambari ndiko kusoma,
Dakika ninahesabu, moja mpaka kwa sitini,
Natambua akrabu, muda wote aki/ini,
Ukishajua hesabu, duara uta/ichora,
Maumbo humu kitabu, mufano wake tiara.
2.
Shirikiana katika kujibu maswali yafuatayo
(iii)
(iv)
(v)
(vi)
Pendekeza kichwa cha shairi.
Shairi hili lina beti ngapi?
Andika idadi ya mishororo ya shairi zima.
Ni miezi gani ya mwaka imetajwa katika shairi?
Ni maumbo gani ambayo yametajwa katika shairi?
Andika ujumbe mmoja kutokana na shairi kuhusu; uuzaji
na ununuzi
Ngeli ya Li —Ya
Funzo h:
Stadi: Kusoma na Kuandika
Ngeli hii hujumuisha nomino ambazo hutumia kiambishi
Zingatia
li- katika umoja na ya katika wingi katika upatanisho wa
kisarufi.
Shughuli 5.8: Kutunga sentensi kwa kutumia ngeli ya li-ya.
(a) Upatanisho wa kisarufi kwa matumizi ya vimilikishi na viwakilishi katika ngeli ya Li – Ya
(b) Upatanisho wa kisarufi kwa matumizi ya vionyeshi na vivumishi katika ngeli ya li-ya
4.
5.
Shirikiana katika kutunga sentensi tano zenye maana katika
umoja na wingi kutokana na jedwali mlilojadili hapo juu.
Shirikiana katika kujadili na kuandika wingi wa sentensi hizi;
(i)Shavu lako hilo linametameta.
(ii)Umbo hili ni kama la nyota.
(iii)Jino lako hili linatingika. Litatoka hivi karibuni.
(iv)Gari langu lile linahitaji kusafishwa.
(v)Daraja lile limebomoka.
(vi)Jani hilo limeanguka hapo lini?
Funzo: (i) Vivumishi vya idadi
Stadi: Kusoma na Kuandika
Shughuli 5.9: Kutambua matumizi ya vivumishi vya idadi
Katika makundi.
1 (a) Shirikiana katika kusoma na kujadiliana juu ya maaha- ya
sentensi zifuatazo.
(i) Mwanafunzi mmoja ana simu mbili.
(ii) Wiki moja ina siku saba.
(iii) Jogoo mmoja aliua nyoka wawili.
(iv) Simba mmoja anaweza kukimbiza watu mia moja.
(v) Kuku kumi wana macho ishirini.
(vi) Kiti kimoja kimekaliwa na wanafunzi watatu.
(b) Shirikiana kusoma na kujadiliana juu ya maana ya sentensi
zifuatazo.
(i) Watu wachache wamehudhuria mkutano wa leo.
(ii) Miti michache itapasuliwa kuni halafu mingine itauzwa.
(iii) Nyani wengi walitikisha mwembe na maembe
kochokocho yakaanguka.
(iv) Kuna chakula haba siku hizi, watu wengi wanakula
maramoja kwa siku.
(v) Pesa kiasi zilikusanywa kusaidia wagonjwa na wasiojikimu.
(vi) Tutazungumza na wanafunzi wachache baada ya
mchezo wetu.
(vii) Wanafunzi wengi wameingia katika chama cha Maskauti
shuleni.
(viii) Nimelipwa shilingi laki moja na ushei kwa kazi yangu.
vya idadi dhahiri na tano zenye matumizi ya vivumishi vya idadi
isiyodhahiri.
Funzo i:
Stadi: Kusoma na Kuandika
Shughuli 5.10: Kutambua matumizi ya vivumishi vya sifa
Katika makundi,
sentensi zifuatazo,
(i) Msichana yule mrembo anapika chakula kitamu.
(ii)Sauti nzuri humtoa nyoka pangoni.
(iii)Mwanamume mrefu alioa mwanamke mfupi.
(iv)Mke mpole huzaa watoto werevu.
(v)Mnyama mlafi ni mnyama hatari.
wawili, vitatu, kumi na saba, virefu, mmoja, kirembo, vipya,
tikana.
Fasihi simulizi (Mafumbo)
Stadi: Kusikiliza na Kuzungumza
Shughuli 5.11: Kufumba na kufumbua mafumbo.
Katika makundi,
Fasihi simulizi (Mafumbo)
Stadi: Kusikiliza na Kuzungumza
Shughuli 5.11: Kufumba na kufumbua mafumbo.
Katika makundi,
(i) Mama ana watoto watatu. Anampenda mtoto mmoja zaidi na ana ndizi mbili. Atafanyaje ili anayempenda zaidi apate ndizi nzima?
(ii) Mimi ni akisami, ukinijumlisha mara mbili nitakuwa kitu kizima. Mimi ni nani?
(iii) Kashate ana magunia matatu. Gunia la kwanza lina kilo mia moja za pamba. Gunia la pili lina kilo mia moja za nyama ya
mbuzi na gunia la tatu lina kilo mia moja za kokoto. Ni gunia gani ambalo ni zito zaidi kuliko mengine?
(iv) Eropleni iliyokuwa juu angani ilitoa sauti iliyowafanya kuku watatu wote kuangalia juu. Ni macho mangapi ya kuku wote kwa ujumla yaliyoona eropleni?
(v) Otiko alichinja mbuzi wawili, nguruwe wawili na nglombe wawili. Otiko alipata ngozi ngapi za wanyama wote kwa ujumla?
(vi) Mama Tinka alipika yai moja kwa dakika saba. Kama yangekuwa mayai matatu, mama Tinka angeyapika kwa dakika ngapi?
(vii) Ni mwezi gani wa mwaka ambao unafikisha angalau siku ishirini na nane?
(viii) Kuna mapapai kumi katika kikapu. Ukichukua nane, utakuwa na mangapi?
(ix) Mama Isma ana watoto watano. Ikiwa wanaitwa Juni, Julai, Agosti na Septemba. Basi mtoto wa tano anaitwa nani?
(x) Ukiwa mshiriki katika mchezo wa riadha, halafu umpite aliye katika nafasi ya pili, wewe utakuwa katika nafasi gani?
(xi) Asubuhi, mimi hutembea kwa miguu minne, adhuhuri ninatembea kwa miguu miwili, ikifika jioni natembea kwa miguu mitatu. Mimi ni nani?
(xii) Kondoo mkubwa amefungwa kwa kamba ya mita tatu shingoni. Kond(X) huyu anaweza kunywa maji kwenye kisima kilicho mita sita kutoka pale alipo bila kukata hiyo kamba. Kondoo huyo anafanyaje kun a ma’i ha o?
Funzo k:
Assignment
ASSIGNMENT : Kuandika Insha: Hesabu MARKS : 10 DURATION : 1 week, 3 days