• No products in the cart.

29

Uganda kama nchi mwanachama mojawapo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, inalo jukumu la kuendeleza na kukuza lugha ya Kiswahili. Katiba …

FREE

Uganda kama nchi mwanachama mojawapo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, inalo jukumu la kuendeleza na kukuza lugha ya Kiswahili.

Katiba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, inapendekeza Kiswahili kama lugha ya mawasiliano ya kikanda. Aidha, katiba ya nchi ya Uganda ya 1995 iliyofanyiwa marekebisho mnamo mwaka 2005 pamoja na hati maalumu ya serikali "The government white paper" ya 1992; zinatoa matamko bayana kuhusu uendelezaji wa Kiswahili nchini Uganda.

Kwa hivyo, Wizara ya Elimu na Michezo kupitia Kituo cha Taifa cha Ukuzaji Mitaala, ilifanya mabadiliko katika mtaala wa elimu kwa kiwango cha sekondari ya daraja la chini na kusisitiza mafunzo ya lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki kimeandikwa kulingana na silabasi ya mtaala mpya ambao unasisitiza shughuli za mafunzo kwa ajili ya kumpa mwanafunzi umilisi pamoja na kukuza stadi za kimaisha na maadili katika kila mada husika. Katika kitabu hiki, kila mada kuu imegawanywa katika mafunzo mbalimbali. Mafunzo hayo pia yamehusisha shughuli kadhaa.

Katika kila funzo, stadi za lugha kama vile, Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika, zimesisitizwa. Kwa hivyo, ili kupata umilisi wa stadi lengwa kutokana na kila mada, mwanafunzi anatakikana kusoma maelekezo na kushiriki katika kufanya shughuli zote za kila mada husika.

Kiswahili

Shughuli za mafunzo, zitampa mwanafunzi fursa ya kufanya utafiti na kujigundulia maarifa kuhusu masuala kadhaa hasa yanayozungumziwa katika silabasi. Mwanafunzi anatakiwa kufanya utafiti kwa kutumia mtandao wa intaneti, kamusi, maktaba, magazeti, majarida au kwa njia yoyote nyingine. Aidha, kuna uwezekano kwamba, mwanafunzi ataweza kufanya shughuli za mafunzo kwa kutumia ujuzi pamoja na tajriba aliyonayo kutokana na mazingira yake.

Shughuli za mafunzo kadhaa zinahimiza ushirikiano kupitia vikundi. Kwa hivyo, mwanafunzi atajifunza zaidi kutokana na wenzake wakiwa Katika vikundi darasani. Kutokana na mijadala yao, wataweza kuwa na uwezo wa kushughulikia vipengele mbalimbali vya shughuli za mafunzo bila ugumu wowote.

Udemy style 5

Course Currilcum

  • Mada kuu 4.1: Uzalendo Details 1 year
  • Mfano wa Shughuli jumlishi: Uzalendo 10, 00:00
  • Mada kuu 4.2: Amani na Usalam Details 1 year
  • Amani na usalama ni masuala muhimu yanayopachana. Haya pia ni muhimu sana katika maisha ya binadamu. Hata hivyo, usalama ni suala pana linaloangazia utulivu wa watu, asasi au mashirika mbalimbali na nchi nzima kwa ujumla. Usalama pia unaweza kuzingatia kuwepo kwa chakula, fedha na ulinzi kwa raia.
  • Mfano wa Shughuli jumlishi: Amani na Usalam 10, 00:00
  • Mada kuu 4.3: Migogoro na Maridhiano Details 1 year
  • Umewahi kukosana na mwenzako? Umewahi kumwona yeyote anayechukiana na mwenzake? Umewahi kumwona anayechonganisha wenzake? Umewahi kushiriki katika kuwapatanisha waliokosana? Hali ya migogoro katika jamii ni mbaya sana na haifai kukubalika kwa kila namna.
  • Mfano wa Shughuli jumlishi: Migogoro na Maridhiano 10, 00:00
  • Mada kuu 4.4: Jinsia Details 1 year
  • Utangulizi Jinsia ni hali ya wanadamu kuwa wa kiume au wa kike kwa kuzingatia tofauti za kijamii na kitamaduni badala ya zile za kibiolojia. Je, wewe ni wa jinsia gani? Je, ni majukumu yapi yanayofaa kushughulikiwa na jinsia fulani? Mada hii itamwezesha kutambua na kutumia msamiati unaohusiana na jinsia pamoja na vipengele vya lugha mbalimbali.
  • Mfano wa Shughuli jumlishi: Jinsia 10, 00:00
  • Mada kuu 4.5: Ngoma na Burudani Details 1 year
  • Mfano wa Shughuli jumlishi: Ngoma na Burudani 10, 00:00
  • Mada kuu 4.6: Magonjwa Details 1 year
  • Ugonjwa ni hali ya kukosa afya nzuri na utendaji unaostahiki ndani ya mwili wa mwanadamu. Kuna magonjwa ya aina mbalimbali na kila ugonjwa una dalili zake. Je, ni magonjwa yapi unayoyajua? Je, unaweza kutambua dalili yoyote ugonjwa wowote?
  • Mfano wa Shughuli jumlishi:Magonjwa 10, 00:00
  • Mada kuu 4.7: Rasilimali Details 1 year
  • Mfano wa Shughuli jumlishi: Rasilimali 10, 00:00
banner