• No products in the cart.

22

Uganda kama nchi mwanachama mojawapo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, inalo jukumu la kuendeleza na kukuza Lugha ya Kiswahili. Katiba …

FREE

Uganda kama nchi mwanachama mojawapo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, inalo jukumu la kuendeleza na kukuza Lugha ya Kiswahili. Katiba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, inapendekeza
Kiswahili kama lugha ya mawasiliano ya kikanda. Aidha, katiba ya nchi ya Uganda ya 1995 iliyofanyiwa marekebisho mnamo mwaka 2005 pamoja na hati maalumu ya serikali "The Government White Paper" ya 1992; zinatoa matamko bayana kuhusu uendelezaji wa Kiswahili nchini Uganda. Kwa hivyo, Wizara ya Elimu na Michezo kupitia Kituo cha Taifa cha Ukuzaji Mitaala, ilifanya mabadiliko
katika mtaala wa elimu kwa kiwango cha sekondari na kusisitiza mafunzo ya lugha ya Kiswahili.

Katika kitabu hiki, kila mada kuu imegawanywa katika mafunzombalimbali. Mafunzo hayo pia yamehusisha shughuli za mafunzo.Katika kila funzo, stadi za lugha kama vile, Kusikiliza, Kuzungumza,
Kusoma na Kuandika, zimezingatiwa Pia. Kwa hivyo, ili kupata umilisi lengwa wa kila mada, mwanafunzi
anatakiwa kusoma maelekezo na kushiriki katika kufanya shughuli zote katika kila mada husika. Shughuli za mafunzo, zitampa fursa ya kufanya utafiti na kujigundulia maarifa kuhusu masuala kadhaa
hasa yanayozungumziwa katika silabasi. Mwanafunzi anatakiwa kufanya utafiti kwa kutumia mtandao wa intaneti au kamusi, maktaba, magazeti, majarida au kwa njia yoyote nyingine. Aidha, kuna uwezekano kwamba ataweza kufanya shughuli za mafunzo kwa kutumia ujuzi pamoja na tajriba aliyonayo.
Mwanafunzi atajifunza zaidi kutokana na wenzake wakiwa katika makundi darasani. Kutokana na mijadala, wataweza kuwa na uwezo wa kushughulikia vipengele mbalimbali vya shughuli za mafunzo.

Udemy style 1

Course Currilcum

  • LSC S2: Usafiri Details FREE 11 months, 3 weeks
  • Utangulizi Usafiri ni hali ya watu, wanyama au vitu kwenda kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa miguu au kwa matumizi ya vyombo vya usafiri. Je! Wewe ni vyombo gani vya usafiri ambavyo umewahi kutumia?
  • Kuandika Insha : Usafiri 10, 00:00
  • LSC S2 :Hesabu Details FREE 11 months, 3 weeks
  • Utangulizi Je! Unaweza kuhesabu vidole vyako vyote katika Kiswahili? Ni vingapi basi? Sasa hivi ni saa ngapi? Leo ni tarehe gani? Mada hii itakuwezesha kutambua tarakimu mbalimbali katika Kiswahili na matumizi yake katika mazungumzo ya kawaida.
  • Kuandika Insha: Hesabu 10, 00:00
  • LSC S2: Salamu na Adabu Details FREE 11 months, 3 weeks
  • Utangulizi Je! Unafikiri kwa nini ni muhimu watu kujuliana hali? Je! Ni matendo gani yanayotendwa na watu wenye adabu katika jamii? Mada hii itakuwezesha kutambua salamu mbalimbali na wakati mwafaka napotumika. Pia utaweza kuthamini umuhimu wa kujuliana hali katika jamii. Katika mada hii pia utajifunza mambo na vitendo vya adabu ambavyo vinafaa kutumika au kufanyika kila siku vinavyotimiza matakwa ya jamii
  • Kuandika insha :Salamu na Adabu 10, 00:00
  • LSC S2:Sherehe katika Familia Details FREE 11 months, 3 weeks
  • Utangulizi Sherehe mbalimbali katika jamii ni suala la maana sana. Sherehe hizi huleta wanajamii pamoja kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali. Je! Ni sherehe gani uliyowahi kuhudhuria katika jamii yako? Ilihusu nini? Ilikuwaje? Mada hii itakuongoza kutambua na kutumia msamiati unaohusiana na sherehe mbalimbali pamoja na vipengele vya lugha vilivyoteuliwa katika mawasilianao.
  • kuandika insha: sherehe katika familia 10, 00:00
  • LSC S2 :Afya na Usafi Details FREE 11 months, 3 weeks
  • Usafi ni suala muhimu katika kutunza afya njema kwa binadamu. Je! Unafikiri kwa nini ni muhimu kutunza usafi? Mada hii itakuwezesha kutambua jinsi ya kuendeleza usafi wa rnwili na wa mazingira yako, na jinsi ya kuepukana na magonjwa yanayotokana na uchafu.
  • Kuandika Insha:Afya na Usafi 10, 00:00
  • LSC S2:Uongozi katika Jamii Details FREE 11 months, 3 weeks
  • Uongozi ni muhimu sana katika jamii. Hakuna jamii ambayo inaweza kuwa na amani bila uongozi bora. Kwa hiyo, tunafaa kuwa na uongozi bora katika jamii tunamotoka. Je, jamii yako ina viongozi wanaoiongoza? Viongozi hao wanafanya kazi gani katika jamii yako? Mada hii itakuwezesha kutambua na kutumia msamiati unaohusiana na uongozi pamoja na demokrasia
  • Kuandika Insha :Uongozi katika JamiiKuandika Insha : 10, 00:00
banner